Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Tanzania nchi yangu

(Kakai Kalonzo voice )

Ule wimbo wake penye Kenya, Weka Tanzania

Utaipenda nchi tu mbona
 
Wakuu salaam,

Kuna hisia miongonni mwa watanzania kuwa uduni wao katika maendeleo umesababishwa na wazungu ambao pia huitwa mamepari.

Mimi nasita kukubaliana na hisia hizi kwa sababu sisi tumejaliwa akili kama wao na zaidi ya hapo tumezungukwa na raslimali tele na mazingira ambayo tukiyatumia hata kwa maarifa madogo tuliyo nayo tunaweza kuendelea sana tu. acha nichukue mifano michache kuthibitisha hoja yangu.

kwanza tuna ardhikubwa na nzuri na nyingine haijawahi kuguswa tangu kuumbwa. Kwangu mimi ardhi hii ni sawa tu na dhahabu kwani ni utajiri mkubwa unaoweza kutupa kila kitu. tujiulize tunaitumia kwa kiasi gani! ajabu vijana wanaikimbia na kwenda kuzamia meli, kugeuka machinga na hata ukabaji.

Pili tuna vyanzo vya kutosha vya maji kwa matumizi mbalimbali kama uvuvi, umwagiliaji,usafirishaji nk. nk. Ajabu watu walioko karibu na vyanzo hivi wanahangaika kutafuta mboga!

Tatu, tuna baraka ya mvua maeneo mengi ambayo maji yake licha ya kutumika kwa kilimo yanaweza kuhifadhiwa kwa matumizi mengi tu. Si ajabu mvua ikanenyesha na inapoisha tu ukamwona mama anabeba ndoo kutafuta maji ya kisima!

Nne tuna misitu ambayo ni vyanzo vya nishati, mvua, maji nk. lakin badala ya kuitumia kama kufuga nyuki na matumizi mengine endelevu ndo kwanza tunanunua mashoka kuifyekelea mbali na kuchoma mkaa! Maji na mvua vikikosekana tunaingia nyumba za ibada kukesha kuomba mvua badala ya kupanda miti.

Sasa wazungu wanainigiaje hapa kama hatuendelei?

Tunaenda kwa wazungu tunaomba watusaidie katika elimu, afya barabara, maji, umeme nk. Chukulia magonjwa mazito kama Ukimwi, kifua kikuu, Kannsa nk. yote haya tunapata madawa kama ARV kwa ufadhili.

Je, nikweli hatuendelei kwa sababu ya wazungu? Ni ipi nafasi yetu ya kuendelea bila kupeleka lawama kwa wazungu?

Inawezekana? Kuna haja ya kutoa boriti kwenue macho yetu badala ya kibanzi kwenye jicho la ...
 
Wanatuhujum kwanini wao wana akili kuliko sisi . Sisi tuko radhi kuyakimbia matatizo yetu kuliko kutafuta uvumbuzi

Waafrika sisi ni wajinga na nadhani ujinga ni asili yetu iko damuni
 
Wanatuhujum kwanini wao wana akili kuliko sisi . Sisi tuko radhi kuyakimbia matatizo yetu kuliko kutafuta uvumbuzi

Waafrika sisi ni wajinga na nadhani ujinga ni asili yetu iko damuni
Kwanini unadhani tu wajinga?
 
Wakati wa Mjadala wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vingi kuna mchango ulisikika ukisema Vyama Vingi ndio vimetufanya Watanzania tuwe Maskini je wadau kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati wa Mjadala wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vingi kuna mchango ulisikika ukisema Vyama Vingi ndio vimetufanya Watanzania tuwe Maskini je wadau kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Simbachawene alishajibu swali jana au juzi na alipigiwa makofi na waliowengi. Pia sina shaka mzee wa magogoni alifurahia jibu!

Wacha wengine tupambane na hali zetu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya mwaka 1992 kurudishwa mfumo wa vyama Vingi ,nini kilizuia Tanzania kupata maendeleo kama sio ccm na ufisadi wao .
 
Majibu ya wengi ni hasira tu ila umaskini wetu haujaanza leo. Katika maadui aliowaona Baba wa taifa ni Ujinga, maradhi na umasikini. Alijua hivi kama vikimtoka mtu hakika mbele ataenda. Vyama vingi vikiondoka nadhani haya maadui yataturudia fasta kuliko
 
Wakati wa Mjadala wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vingi kuna mchango ulisikika ukisema Vyama Vingi ndio vimetufanya Watanzania tuwe Maskini je wadau kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app


Na wewe nawe! Yaani unamsikiliza Simbachawene? Huyu huyu ambae akiwa waziri alitoa "ufafanuzi" akisema "serikali haijawahi kusema itatoa elimu bure isipokuwa iliahidi kutoa elimu bila malipo"!
 
Watanzani hebu tujiulize toka CCM izaliwe ni miaka 42 lakini hali ya maisha ya Watanzania ni ya Umaskini mkubwa licha ya Raslimali tulizonazo. Naomba Tujiulize tatizo ni nini? Tumekosea wapi? Nini kifanyike?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom