Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Wana forum, ningependa kufahamishwa kujua kwanini Tanzania tu masikini.Haya yote ni wakina nani wamesababisha, kuanzia tupate uhuru hadi leo
Nawasilisha
 
DARASANI.jpgSHULE.jpgMMC.jpg
MMC2.jpg

maendeleo bora kwa kila mtanzania inawezekana.
 
Wana forum, ningependa kufahamishwa kujua kwanini Tanzania tu masikini.Haya yote ni wakina nani wamesababisha, kuanzia tupate uhuru hadi leo
Nawasilisha

masikini wewe mi sio masikini
Acheni kuaminisha watu upuuzi wenu hapa
Yaani mvivu wewe halafu ulaumu wengine kwamba ndo wamekusababishia umasikini .....! shame on u guys
 
Habari zenu wanamtandao
Ebu tujiulize huu umasikini tanzania utaisha lini! Ilifikia hatua nikasema kwakua nchi hii imeongozwa na wanaume kwa miaka 54 sasa bassi tuwape wanawake wasomi waiongoze ingalau tuwaone kwa miaka 5 tu kwakuanzia.
Nchi hii ni tajiri sana lakini rasilimali za nchi zachukuliwa kama shamba la bibi.
Wananchi tuamke sasa na nyie wanawake wasomi wenye kuujua ulimwengu mjitokeze kuwania urais 2015.
Nawasilisha
 
Tuwahimize wanawake wajitokeze kuwania urais 2015. Wanawake wanahofu ya mungu hawataihujumu nchi
 
Si ulishaambiwa kuwa Rais kasema kuwa yeye ndiye atakuwa Rais wa mwisho kuongoza Tanzania maskini ............ Neema inaanza mwakani mkuu!!
 
Umasikini wetu watz sio sababu ya nchi kuongozwa na mwanaume, tuna mawaziri waandamizi wanawake wangapi? je utendaji kazi wao una tofauti na wanaume?
Angalia kwa waziri sophia simba anavyoendesha wizara kibazazi, anasubiri mtu abakwe ndio atoe tamko, je ana tofauti gani na wanaume?
Nenda kwenye sheria, utamkuta angela kairuki, lakini maskini wanalia kila siku kwa kubambikiwa kesi je haoni?
Nenda kwa tibaijuka, angalia jimbon kwake na utendaj wake kwenye wizara ya ardhi nyumba na makaz, uone wamefanya nini.
 
Inawezekana huyu bwana ana nia na uchungu, wasiwasi wangu ni kama kweli ana uwezo wa kuyakabila anayoyazungumza na kuwaza. Nafikiri hana! Na nia peke yake bila uwezo haiwezi kusaidia kumaliza umaskini, utasikitika sana lakini at the end of the day watu hatutampima kwa kiasi gani aliamia na umaskini wetu bali aliweza kupambana nao!

Mkuu Kitila Mkumbo maneno haya uliyasema june 2007 na ni kweli kabisa huyu bwana amedhihirisha miaka saba baadae kuwa hana uwezo wa kuyakabili anayozungumza na kuwaza.
Ila lingine lililo jiweka wazi ni kuwa kumbe hata NIA HAKUWANAYO.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Si ulishaambiwa kuwa Rais kasema kuwa yeye ndiye atakuwa Rais wa mwisho kuongoza Tanzania maskini ............ Neema inaanza mwakani mkuu!!

Atakuwa ameacha mazingira gani hadi hiyo neema ianze mwakani? Mie nadhani hali atakayo mwachia mwenzake ni mbaya sana kwani ataanza na kulipa madeni makubwa yaliyoachwa naye wakati kilichofanyika kwa mikopo hiyo hata hakionekani.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
25% ya Watanzania ni maskini kwa sababu wamezaliwa katika kaya maskini au wametoka mikoa maskini, yasema ripoti mpya ya Benki ya Dunia.

6th December 2012
Imeelezwa kuwa kasi ndogo ya kupungua kwa umasikini nchini inatokana na sekta zinazoendesha uchumi kutoajiri watu wengi.

Hayo yamesemwa na Mshauri Mwelekezi wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Deo Mtalemwa, wakati akizungumza katika warsha ya siku moja ya kutoa maoni ya wadau wa serikali za mitaa na asasi za kiraia juu ya malengo ya milenia (MDG), mjini hapa jana.

Mtalemwa ambaye amefanyakazi na Benki ya Afrika (ADB) kama Afisa Mikopo na Afisa Uhusiano kwa miaka 20, alisema sekta za msingi zinazoendesha uchumi wa nchi kama vile, madini, viwanda, ujenzi na utalii zimeajiri idadi ndogo ya Watanzania ikilinganishwa na sekta ya kilimo ambayo licha ya kuajiri idadi kubwa ya watu lakini imekosa msukumo wa kutosha kuchangia ukuaji wa uchumi.

Sababu nyingine alizotaja kukwamisha jitihada za Tanzania kupunguza umasikini ni, kuwepo kwa migawanyo mibovu ya rasilimali za nchi, baadhi ya mikoa kuwa na rasilimali nyingi na mingine ikiwa haina rasilimali za kutosha na kuwepo kwa mifumo mibovu ya ukusanyaji kodi na usimamizi wake.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo, ni lazima Tanzania ikapanua wigo wa ukusanyaji kodi ili Watanzania wote walipe kodi na kutolea mfano wa posho za vikao mbalimbali kuwa zimekuwa zikitolewa pasipo kukatwa kodi jambo ambalo alidai ni eneo jingine linaloweza kupanua wigo wa kodi.

Aidha, Mutalemwa aliwataka Watanzania kutotumia njia za ujanja ujanja kukwepa kodi badala yake walipe kodi kwa hiari ili kujenga ujasiri wa serikali wa kuhoji pale ambapo wanaona matumizi ya fedha zao hayafanywi kwa usahihi.

Hata hivyo, alisema Tanzania imefanya vizuri katika kukuza uchumi wake kutoka asilimia 6.8 mwaka jana hadi kufikia asilimia 7.1 mwaka huu.

Alisema utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa umebaini kuwa, umasikini nchini umepungua kwa asilimia 5 katika kipindi cha miaka 18 toka mpango wa milenia wa kupunguza umasikini duniani ulipopitishwa na mataifa 189 Tanzania ikiwemo na kuanza kufanyiwa kazi mwaka 1994 mpaka sasa.

Takwimu za umoja huo zinaonyesha uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia 7.1 mwaka huu toka asilimia 6.8 mwaka 2011, huku Uganda ikionyesha uchumi wake kukua kwa kasi zaidi kwa toka asilimia 4.1 mpaka kufikia asilimia 6.0.

Nchi nyingine katika ukanda wa Afrika Mashariki ni Rwanda ambayo uchumi wake umekua kwa asilimia 9.9 kutoka asilimia mwaka 2011 hadi asilimia 8.8 mwaka huu, huku Burundi ukikua kwa 4.8 mwaka huu toka asilimia 4.2 mwaka jana.

Kwa upande wa Kenya, uchumi wake unaonyesha kushuka kwa asilimia 1.6 kutoka asilimia 5.1 mwaka jana hadi asilimia 3.5 mwaka huu.

Chanzo: Nipashe
 
Chadema inawalemaza watu kuwazaa na hawataki Kazi kabisa wanasubiria Kama mana
 
Back
Top Bottom