Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Swali hili limekuwa likiumiza kichwa wadau wengi for years,Rais Incumbent yeye huuuliza"hivi watanzania tumelogwa na nani?aliyepita bwan Jk yeye hakutaka makuu alijisemea tu sijui ni kwanini Tanzania ni masikini
Sasa leo mtaalamu na genius aitwaye ZE NDINDINDI amegundua tatizo linalofanya hii nchi iende kibashite bashite
NI ALAMA YA MNYAMA WA TAIFA AITWAYE TWIGA:kuji associate na limnyama lirefu lijinga lisilo na faida,lenye urefu usio na faida linaloweza kuliwa hata na panya ni ujinga wa hali yajuu
Nchi kama nchi na wananchi wake ime reflect tabia za kibwege za bwana twiga na hata mashirika yenye kiherehere yaliyoamua kumuweka bwana twiga kwenye logo zao yamejitengenezea albadiri,embu angalia tanesco na wazee wa bombardier,useless kabisa
Narudia tena tubadilishe mnyama wa taifa awe hata fisi,sungura au nungunungu
Nawasilisha hoja hii ya kiufundi kabisa baada ya utafiti wa muda mrefu
 
Hilo tunalijua siku nyingi...na huyo mnyama aliwekwa na wakoloni kwa sababu zao kwani kabla ya uhuru wakoloni waliweka picha za wanyama mbalimbali kny bendera za makoloni yao kwa sababu tusizozijua sisi...hivyo basi kabla ya kumtoa huyu mnyama kwenye utambulisho wa nchi yetu tujiulize ana faida au hasara gani kwa nchi yetu..isijekuwa kama ile ya mabutu/loraa kabila alivyobadilisha bendera iliyokuwa na mwenge na kubadili jina la zaire hadi DRC na mara tu ya kubadilisha mambo yakabadilika na hadi sasa hakuja tengamaa.
 
The calcurosis of the human brain is phynomerous.
Yet I do conchur, to why merender can convey such deminer.
Cc PLO Lumumba
Cc Profesa matumbo
 
Swali hili limekuwa likiumiza kichwa wadau wengi for years,Rais Incumbent yeye huuuliza"hivi watanzania tumelogwa na nani?aliyepita bwan Jk yeye hakutaka makuu alijisemea tu sijui ni kwanini Tanzania ni masikini
Sasa leo mtaalamu na genius aitwaye ZE NDINDINDI amegundua tatizo linalofanya hii nchi iende kibashite bashite
NI ALAMA YA MNYAMA WA TAIFA AITWAYE TWIGA:kuji associate na limnyama lirefu lijinga lisilo na faida,lenye urefu usio na faida linaloweza kuliwa hata na panya ni ujinga wa hali yajuu
Nchi kama nchi na wananchi wake ime reflect tabia za kibwege za bwana twiga na hata mashirika yenye kiherehere yaliyoamua kumuweka bwana twiga kwenye logo zao yamejitengenezea albadiri,embu angalia tanesco na wazee wa bombardier,useless kabisa
Narudia tena tubadilishe mnyama wa taifa awe hata fisi,sungura au nungunungu
Nawasilisha hoja hii ya kiufundi kabisa baada ya utafiti wa muda mrefu
Wataalam fuatilieni hilo wazo msilidharau, maana nchi hii kama fisi wanagombana na kuongea kama binadamu kwa nini hili lisiwezekane?
 
KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI

1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.

2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.

3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa
ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.

4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.

6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.

7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.

8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.
Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa
Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).

9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k

10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa
na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.

11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),
Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).

12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.

13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.

14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.

15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na
Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na
kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.

16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na
Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.

17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).

18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.

19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.

20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana
hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.

21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya
kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.

24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.

24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).

25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.

26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.

Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.

TATIZO NI NINI? NANI ANAFAIDI HUU UTAJIRI? NANI WA KUMLAUMU? NANI NI SABABU?
KWA NINI TUNASHINDWA KUTUMIA HUU UTAJIRI?
 
Usijidanganye kila nchi hapa Duniani iko hivyo, kila nchi unaweza kuorodhesha sifa ambazo inazo hivyo hatuna upekee wowote ule!

Hivyo kama ni Umaskini sisi ni masikini kwa sababu ambazo wengine ni masikini na wengine ni matajiri na siyo zaidi ya hapo!

Wewe kutompeleka mwanao shule unasema mbona hata flani hajampeleka mwanae, baba yako kajenga nyumba ya nyasi nawe unajenga ya nyasi unasema mbona baba nae alijenga nyumba ya nyasi.
 
Usijidanganye kila nchi hapa Duniani iko hivyo, kila nchi unaweza kuorodhesha sifa ambazo inazo hivyo hatuna upekee wowote ule!

Hivyo kama ni Umaskini sisi ni masikini kwa sababu ambazo wengine ni masikini na wengine ni matajiri na siyo zaidi ya hapo!
Barbarosa siamini kama hii comment ni yako!!! Labda mtu ameiba password yako?!!
 
Usijidanganye kila nchi hapa Duniani iko hivyo, kila nchi unaweza kuorodhesha sifa ambazo inazo hivyo hatuna upekee wowote ule!

Hivyo kama ni Umaskini sisi ni masikini kwa sababu ambazo wengine ni masikini na wengine ni matajiri na siyo zaidi ya hapo!
Nchi zote zina Tanzanite nasikia ata kwenu Rwanda zipo!?
 
Back
Top Bottom