Ukweli ndo utakaokusaidia, ukijua ukweli basi unaweza kujipanga na kukubali hali halisi ili uweze kwenda mbele, lkn ukiishi kwa kujidanganya kwamba wewe ni una upekee maalumu ambao wengine hawana utakuwa na maisha magumu siku zote!
Dunia hii yote imebarikiwa na kila kitu na kila nchi ina upekee wake, kama TZ inapakana ana Kenya, Uganda, Msumbiji, kongo, Zambia hakuna sababu kwa nini sisi tu ndo tuwe na upekee wa kuwa na vitu ambavyo wengine hawana huko ni kujidanganya, isitoshe mipaka imewekwa na Binadamu, hivyo kama Gesi ipo Mtwara itakuwepo Msumbiji pia, kama Makaa ya Mawe yapo Ziwa Nyasa yatakuwepo Malawi pia n.k.!