Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Return Of Undertaker Usijidanganye kila nchi hapa Duniani iko hivyo, kila nchi unaweza kuorodhesha sifa ambazo inazo hivyo hatuna upekee wowote ule!

Hivyo kama ni Umaskini sisi ni masikini kwa sababu ambazo wengine ni masikini na wengine ni matajiri na siyo zaidi ya hapo!
Du!! Kwanin tusiitwe shithole!!! Kama akilizenyewe ndizo hizi.kwahiyo kama wengine ni masikini ni lazima na wewebuwe masikini?
 
CCM imetawala nchi hii tangu 1961 chini ya uongozi wa Mwalimu hadi 1985. Hapa hatuwezi kulaumu sana maana hadi Mwalimu anang'atuka kulikuwa bado madini hayajaguswa kwa kiwango kikubwa. (Country minerals was virgin)

Tatizo limetokea kuanzia mwaka 1990 hadi 2018 mwaka wa Makininia, ni takribani miaka 28 imepita; hapa kwa kweli ndipo tatizo lilipoanza tulipoamua ubinafishishaji pamoja na uchimbaji wa raslimali zetu bila kufuata maono ya mwalimu kwamba hizi mali msizigunse kama mpaka nchi itakapokuwa na watalaam wazalendo.

Sasa tuwaulize hawa CCM haya maswali maana ndiyo wao walikuwa wanatunga hizo sera na kusisimamia kupitia Bunge ambalo wao ni majority.
 
Return Of Undertaker Usijidanganye kila nchi hapa Duniani iko hivyo, kila nchi unaweza kuorodhesha sifa ambazo inazo hivyo hatuna upekee wowote ule!

Hivyo kama ni Umaskini sisi ni masikini kwa sababu ambazo wengine ni masikini na wengine ni matajiri na siyo zaidi ya hapo!
Mkuu una madini sometime basi tu! anyway mi naamini uwezo wa kufikiri ni muhimu zaidi kuliko rasilimali za asili, jamii yenye watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri ni rahisi sana kupata maendeleo!
 
Ukweli ndo utakaokusaidia, ukijua ukweli basi unaweza kujipanga na kukubali hali halisi ili uweze kwenda mbele, lkn ukiishi kwa kujidanganya kwamba wewe ni una upekee maalumu ambao wengine hawana utakuwa na maisha magumu siku zote!

Dunia hii yote imebarikiwa na kila kitu na kila nchi ina upekee wake, kama TZ inapakana ana Kenya, Uganda, Msumbiji, kongo, Zambia hakuna sababu kwa nini sisi tu ndo tuwe na upekee wa kuwa na vitu ambavyo wengine hawana huko ni kujidanganya, isitoshe mipaka imewekwa na Binadamu, hivyo kama Gesi ipo Mtwara itakuwepo Msumbiji pia, kama Makaa ya Mawe yapo Ziwa Nyasa yatakuwepo Malawi pia n.k.!
nahisi ww ndio uliewaita waTZ malofa pale jangwani na hapa unajitahidi kuwaaminisha hivyo,
umeFail Barbar waTZ wa ss sio wale wa 60's
 
Unaona mnazidi kujidanganya, ni nali alikwamba kwamba Tanzanite ina thamani kubwa? Unajua soko la tanzanite Dunia kote ni kiasi gani? Ni 500 milion USD tu, sasa hiyo ni sawa na karibia thamani ya Mgodi mmoja tu wa Buzwagi na nusu yake!
Kumbu kumbu zangu zinaniambia Buzwagi thamani yake ni zaidi ya milion 300 USD!
[emoji35][emoji35][emoji35]
 
Wewe kama umeviona hivyondio vigezo vyakuwa tajiri sawa ila kumbuka unaweza kuwa na hela jinsi yakutumia ndio shida mpe chizi hela uone atatumia vp nafikili kwamfano huo umeelewa
 
Nafikiri nimeelewa kwamba sisi tuna upekee hapa Duniani na kwa nini ni masikini wakati nchi yetu ni kipekee? Au siyo hivyo? Na kama ni hivyo ndo nikasema siyo kweli kwamba nchi yetu pekee yake ndiyo ina upekee bali nchi zote Afrika na Duniani zina upekee wake ambao pia unaweza kuuorodhesha kama mleta mada alivyofanya!
hebu ondoa ilo neno upekee halafu soma tena uelewe, usisome ili ujibu...
 
With JPM things will change....keep on praying for him...Tanzania mpya inakuja na umaskini utabaki kuwa historia.
 
Kuna wimbo wa Lil Wayne unaitwa You ain't Know akiwa anauimba kwa Live Show kwenye BET akawa anawaambia mashabiki

"E'erbody say, off where we going?"

Sisi hata kuuliza tunapoenda ni mtihani badala yake kuna mbuzi wanataka kuburuzana kuwe kwa miaka saba
 
wakuu mie nilikua naona serikali yetu igawanye Tanzania ki zone,kila zone ijitegemee,kuwe na kiongozi ila wote wawe chini ya Rais,hii itasaidia kila zone kuexploit kila resources kwa maendeleo yao ya kizone,,,,,na pia kutaleta ushindani baina ya zones,sio sasa hivi hata viongozi wa juu wanamuogopa mkuu,wako passive.....
serikali ya nani atakaeweza kufanya hivyo!!
kila mtu anatamani kile kiti cha juu ili ajinufaishe yeye mwenyewe, japo idea ni nzuri na ndio kinachofanyika USA.
 
Ukweli ndo utakaokusaidia, ukijua ukweli basi unaweza kujipanga na kukubali hali halisi ili uweze kwenda mbele, lkn ukiishi kwa kujidanganya kwamba wewe ni una upekee maalumu ambao wengine hawana utakuwa na maisha magumu siku zote!

Dunia hii yote imebarikiwa na kila kitu na kila nchi ina upekee wake, kama TZ inapakana ana Kenya, Uganda, Msumbiji, kongo, Zambia hakuna sababu kwa nini sisi tu ndo tuwe na upekee wa kuwa na vitu ambavyo wengine hawana huko ni kujidanganya, isitoshe mipaka imewekwa na Binadamu, hivyo kama Gesi ipo Mtwara itakuwepo Msumbiji pia, kama Makaa ya Mawe yapo Ziwa Nyasa yatakuwepo Malawi pia n.k.!
Wewe ukiwa na mshahara mnono kuliko jirani yako unataka ujilinganishe naye!! eti kwa vile fursa ni tofauti!
Ni lazima uangalie raslimali na fursa zako uweze kujitathmini kwa nini hujazitumia!! Hivi tunajifunza nini kwa Botswana ambao madini yao yana mikataba tofauti na yetu/mirahaba! Na sasa Botswana iko dunia ya pili! matajiri. Hivi tunajifunza nini kwa Norway ambao mafuta yao wameamua waweke akiba kwa vizazi vijavyo -Heritage- Wakati sisi tumemaliza Tanzanite na tumebakiwa na mashimo ya kuonyesha watoto wetu? Hili bandiko siyo la kukejeli!!! Ni la kutafakari!!
 
Nimesahau jina la kitabu ila kimeandikwa na Shivji, akawa anaonyesha jinsi maendeleo yanavyoenda na hatua zake. Hapa achana na claiming za yule mzungu na theory yake ya development.

kwa stages ziliotajwa huwezi amini sisi bado tupo kwenye ujima halafu viongozi wanataka waruke shortcut ati viwanda.

Viwanda huku huna malighafi wala wataalamu ni komedi nyingine hii
 
serikali ya nani atakaeweza kufanya hivyo!!
kila mtu anatamani kile kiti cha juu ili ajinufaishe yeye mwenyewe, japo idea ni nzuri na ndio kinachofanyika USA.

mkuu umegusa penyewe,tatizo la Tanzania na Africa kwa ujumla ni ubinafsi,corruption kila mahali,mpaka hapo tutakapopata kiongozi mzalendo ndio tutamove forward,ambaye kusema ukweli ni hard to find,huyu wa sasa alikuja na matumaini ,tukadhani tumepata,two years down the line,kila mtu anabaki anajiuliza did we?
 
Katiba tu ndio suluhisho, tuweke sheria kiongozi akihusika na uhujumu uchumi afilisiwe na kutumikia kifungo.

washenzi hawa wanatuchezea sharubu ss hivi sababu katiba inawaFavor sana.
 
Back
Top Bottom