Tuna rasilimali lakini hatuna wajasiriamali. Ah yes I know; unaweza ukalaumu mfumo na ukalaumu sheria na ukalaumu mazingira, ukalaumu siasa, ukalaumu mvua, ukamlaumu mkeo/mmeo blah blah blah... The blame game... so easy to play... actually everyone can play it. But solving real world problems? Oh boy... it is for the few; leaders (Definitely not bosses), ambitious, positive minded, persistent, proactive - entrepreneurs. They don't fight a system, they fight in the system.. they don't complain about unfriendly environment/ gvt/ whatever, they innovate, they adapt, they improvise and they deliver under those unfriendly 'factors'. Tunahitaji wajasiriamali wa kweli wa kutosha, na nchi itabadilika ndani ya muda mfupi sana (kiuchumi).Eee si ndio? Asa kumbe nini.
Nchi zilizoendelea zinapalilia sana utamaduni wa Ujasiriamali - kwasababu siku zote mjasiriamali analitazama tatizo kama fursa, anatafuta solution, anapiga pesa... win win situation; yeye na timu yake wanafaidika, nchi inafaidika. Haijalishi ni tatizo gani... nini, rushwa? kwake ni fursa, kwasababu akileta suluhisho la kibunifu la kuondoa rushwa manaake anakuwa milionea! Which makes me believe that saivi tunavyoongea kuna mjasiriamali yuko mahali fulani anabuni solution ya rushwa... and soon tutaisikia na tutabaki tunajiuliza tulishindwa nini kufikiria hicho kitu kabla yake. Wajasirimali ni problem solvers, they never blame anyone. Ni watendaji, wanafanya vitu, tunaona matokeo - mabadiliko yanatokea.
Unawachukulia poa wajasirimali eh? Well, labda hujajua ..FYI hizi ni baadhi tu ya kampuni zilizoanzishwa na wajasiriamali walioamua kutatua changamoto walizoziona kwa wakati huo na wanaendelea kufanya hivyo. What is more interesting ni kwamba hivi sasa wanatatua hadi changamoto za wakati ujao he he he😜😉 Na haya ni mapato yao kwa mwaka uliopita;
FACEBOOK REVENUE (2019) = $17.65 billion
GOOGLE REVENUE (2019) = $ 40.3 billion
AMAZON REVENUE (2019) = $70.0 billion
*Source: Statista
Kumbuka; hizi kampuni nilizoziorodhesha hapa hazina migodi, wala mbuga, wala mashamba, wala makinikia, wala Mlima Kilimanjaro, wala gesi, wala mafuta, wala hazina jeshi lake, wala mahakama zake, wala bunge lake, wala... you name it. Nchi ya Marekani inapata kodi kubwa sana toka kwa haya makampuni. Ajira zinazozalishwa na haya makampuni ndo usiseme... mpaka huku kwetu. Can you see it's ripple effect? Sasa BUDGET YA NCHI ya Tanzania (2019/2020) ni USD 14.3 billion, ina maana kampuni ya FACEBOOK peke yake ina mapato zaidi ya mapato tarajiwa ya nchi ya Tanzania. Naomba nikuulize wewe mwenzangu, Facebook wanauza nini? Google wanauza nini? Labda Amazon, lakini je, wanachokifanya ni rocket science? ....Ivi sijui kuna mtu ananielewa?
I wish vijana tungeacha staili ya wazee wetu ya kukimbilia kutafuta wa kumlaumu kwa kila kitu. Let us take the responsibility, the future is in our hands. Umaskini tumeukuta, sio kosa letu. Lakini kama umaskini utaendelea ni kwasababu tunaacha kuwa watendaji tunakazana kuwa 'walaumuji'(blamers) na tunatarajia kuwa kuna mtu kutoka tusikokujua atakuja kurekebisha mambo. Na nchi hii ina wasomi wengi tu tunaowajua simply kwasababu wanajinadi na PhD zao, masters sijui na mbwembwe kibao - ila matokeo ya hizo ndude zao ndo hatuyaoni - ivi ndugu wasomi mnakwama wapi?🤔🤔🤔 Ah hapana, siwalaumu.. najaribu kuwaza kwa sauti teh teh teh teh tiiiiih!
Kabla hujamlaumu mtu jiulize; (Wewe) Umetimiza wajibu wako katika nafasi yako? Je, unafanya nini kuondoa changamoto zinazosababisha umasikini uendelee kuwepo kwako binafsi kwa kuanzia, kisha kwa familia, halafu jamii inayokuzunguka na hatimaye taifa.
Enough talk, let's get to work - find solutions.
Naomba kuwasilisha.