Mi nafikiri hili daraja linalotawala,halina nia ya kuwatoa wananchi kwenye umaskini,kwa ufisadi na wizi uliopo,kila kiongozi anaiba kwa urefu wa kamba,na kunufsisha familia yake,ukiaangalia Hawa viongozi Nyerere,Karume,Mwinyi,Sita,Kikwete,Mkapa,na watoto wao,unajiuliza wakati watoto wa Kikwete wanapata fulsa ya kuwa marubani ktk umri mdogo,watoto wangapi wa maskini walipata hiyo fulsa?
Wakati watoto wa Karume na Mwinyi,wanapata fulsa pendelevu za masomo,na kazi nono,watoto wangapi wa kawaida walipewa hizo fulsa.
Ni watoto wa Nyerere tu ambao hawakubebwa na cheo Cha Baba yao.
Pinda kaachia Jimbo,mtoto wake kachukua,Kikwete aliiacha Jimbo,kijana wake akachukua,Mwinyi alikuwa Raisi,sasa hv,na mwanawe anatafutiwa chance awe Raisi.
Viongozi wetu wa nchi za afrika(nyeusi)hawana maono ya kuzifanya nchi ziwe superpower hata miaka 100 ijayo,Kama Ilivyo kwa India,Philippines,SA,Urusi,Vietnam,Korea,Japan,
Sisi huku ni wizi wizi wizi kwenda mbele,ili familia zao zineemeke,Bora hata ethiopia ina udikiteta lakini serikali inapambana kuhakikisha nchi inakuwa na uchumi mkubwa,wakati sie tunajenga mradi mkubwa wa umeme kwa pesa ya kukopa na kutumia contactor wa nje,ethiopia wanajenga mradi wao wenyewe,wazawa na kwa kutumia pesa yao.