Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Kuna wakati najiuliza tumemkosea nini Mungu wetu mpaka huu umasikini wa watanzania upo kwa miaka 60 sasa licha ya Mungu kuibariki nchi hii kwa kuipa raslimali karibu kila mkoa lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa?

Raslimali zilizopo Tanzania hakuna nchi ya kufanana nayo Afrika Mashariki na kati.

Viongozi wetu kwa miaka 60 ni wale wale chama ni kile kile lakini wameshindwa kuzitumia raslimali tulizopewa na mungu kuwaondolea umaskini wananchi wake, badala yake wameamua kuwatoza kodi za maumivu na kukopa nje mpaka deni la taifa limefika tril 71 lakini umaskini upo pale pale.

Binafsi naanza kuamini Tanzania tuna tatizo na Mungu ni wakati kama taifa kufanya maombi na kuombana msamaha kwa maovu tuliyofanyiana ili Mungu arudishe upendo wake kwa nchi tupate maendeleo na wananchi wanufaike na kuondokana na umaskini kwa kutumia raslimali alizotupa Mungu.

Kuna watu wapo magerezani kwa miaka kwa kesi za kuonewa, kuna watu wamepigwa risasi, wamepotea, wameuawa kwa uonevu tu.
Yote hayo Mungu hapendi na hasira ya Mungu huwa ni mateso kwa watu.
Raisi wa Kwanza alikuwa na maono na akayaweka wazi umasikini na ujinga ndo vitu vikubwa vinavyoikumba Nchi hii hakuna kingine, Sasa waliokuja ilitakiwa wakomae kwenye hayo mawili hata kwa mijeledi watu wasome na walioelimika wapewe kazi wafanye na walipwe vizuri Ili wajiondolee umasikini kitu ambacho kingefanya wasio soma na wasiopenda shule wasome kwa bidii Ili wapate kazi na walipwe vizuri Sasa hakuna mkazo hapo kwenye kuwapa watu pesa inaonekana ni anasa kitu ambacho kinazidi kuzalisha umasikini, haya huku kwenye ujinga kwa vile upo sana sehemu za kijijini ilitakiwa nguvu kubwa iwekwezwe huko kwa kupeleka umeme na Kila kijiji kifungwe tv kubwa za kutoa elimu na kuuzomea ujinga mbona zamani wasiosoma nasikia walikuwa wanachambwa mpaka wanakosa amani na nyimbo zipo? Eti asiyejuwa kusoma ni mjinga kabisa na akiletewa barua anaitembeza kwa Kila mtu Ili asomewe kilichomo? Ujinga ndo janga kubwa linalosabisha tunashangaa kwanini serikali ikope Kila siku maana wanaoweza kufanya pesa izunguke ni wachache na nisehemu za mjini peke yake napo kwa watu wachache, ukitaka kuamini ni kuangalia ni watu wangapi wanaona fahari kununua nguo nzuri na kuvaa, kula chakula kizuri, kununua bidhaa za umeme za kurahisisha kazi, kupika kwa vifaa vya kisasa, kujenga nyumba za binadamu na siyo za kama wanyama wa kufungwa kama siyo watu wa mjini? Hivyo vijiji vibadilishwe kwa haraka sana kwa kujengewa vitu vya kisasa kwa lazima na elimu itolewe kwa lazima Kila mtu ajue kusoma kwa lazima Ili ajue matumizi ya vitu kitu kitakacholeta kazi nyingi na wale wanaofanya kazi iwe binafsi au serikalini walipwe vizuri na serikali itunge sheria za kuwalipa watu vizuri Ili wajiondolee umasikini.
 
Mkuu huko nikuharibu Ajira za watu
Sasa wakisema wajiendeshe wenyewe hao madereva watakula wapi
Huoni kama utaingeza umaskini?
Acha watanzania wenzako wajipatie kipato kupitia fani yao.
Mkuu, sijasema kuwa madereva wasiajiriwe. Tatizo ni wingi wa madereva. Huko nyuma nilibahatika kufanya kazi serikalini. Tatizo utakuta kuna vitu Bina madereva wengi kuliko idadi ya magari.
 
Nchi nyingi za kiafrika ndivyo zilivyo, iangalia Kongo.
Tatizo ngozi nyeusi bado haijastaarabika. Yaani haijafikia katika hatua ya juu ya ubinadamu.

Hapo hata ichukue CHADEMA au CHAWATA hali inaweza kuwa mbaya zaidi.
Akipatikana kiongozi wa kuwapeleka mpwitempwite mbona wanakaa sawa tu, angalia machinga walivyoambiwa kupangwa mbona wanajipanga Kila sekita ikipelekwa mpwitempwite kwa kupewa probation isiyokoma mbona matokeo yataonekana? Yaani ukishindwa kuperfom unawekwa pembeni unaachia mshahara wengine.
 
Ttzo ni vyama pinzani vya siasa visivyo imara ndo vinasababisha yote haya yatokee
Leo ukiitoa CCm madalakani utampa nchi nan
Chadema chama kina zaidi ya miaka 20 hakina ofisi hakina katiba, chama cha ukanda
TLP ni yale yale
CUF kila sku wanagombea vyeo
ACT bado wapya
NCCR chama ya mbatia na akijui kinataka nn nchi au CCM b
Wala siyo vyama maana kama ni vyama mbona huwa Kuna ilani nzuri mpaka watu wanachachawa? Shida ni ujinga na umasikini basi, hivyo viwili ndo vinaleta shida nakufanya muda upatikane wa kuchezea bila kuzalisha.
 
Ttzo ni vyama pinzani vya siasa visivyo imara ndo vinasababisha yote haya yatokee
Leo ukiitoa CCm madalakani utampa nchi nan
Chadema chama kina zaidi ya miaka 20 hakina ofisi hakina katiba, chama cha ukanda
TLP ni yale yale
CUF kila sku wanagombea vyeo
ACT bado wapya
NCCR chama ya mbatia na akijui kinataka nn nchi au CCM b

Anzisha chako basi mkuu
 
wapo madokta , maprofesa , wataalamu wa ngazi ya Kati na chini wa uchumi waje washauri
 
Kuna wakati najiuliza tumemkosea nini Mungu wetu mpaka huu umasikini wa watanzania upo kwa miaka 60 sasa licha ya Mungu kuibariki nchi hii kwa kuipa raslimali karibu kila mkoa lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa?

Raslimali zilizopo Tanzania hakuna nchi ya kufanana nayo Afrika Mashariki na kati.

Viongozi wetu kwa miaka 60 ni wale wale chama ni kile kile lakini wameshindwa kuzitumia raslimali tulizopewa na mungu kuwaondolea umaskini wananchi wake, badala yake wameamua kuwatoza kodi za maumivu na kukopa nje mpaka deni la taifa limefika tril 71 lakini umaskini upo pale pale.

Binafsi naanza kuamini Tanzania tuna tatizo na Mungu ni wakati kama taifa kufanya maombi na kuombana msamaha kwa maovu tuliyofanyiana ili Mungu arudishe upendo wake kwa nchi tupate maendeleo na wananchi wanufaike na kuondokana na umaskini kwa kutumia raslimali alizotupa Mungu.

Kuna watu wapo magerezani kwa miaka kwa kesi za kuonewa, kuna watu wamepigwa risasi, wamepotea, wameuawa kwa uonevu tu.
Yote hayo Mungu hapendi na hasira ya Mungu huwa ni mateso kwa watu.
Umasikini ni wa mtu binafsi.
Mtu mvivu, masikini wa akili, no ambition, atatajirikaje?
 
Hakuna laana yoyote katika hili. Ni watu tu tumekosa maarifa ya kuendeleza nchi. Miaka 60 ya uhuru maono na malengo ni yaleyale. Hatujawahi kuwa na utaratibu wa kupima tulipotoka tulipo na tunapoelekea. Tumeamini na kuaminishwa kuwa siasa ndiyo kila kitu. Tumekuwa wanafiki na watu wasiojali. Mahodari wa kushangilia kulalamika na kulaumu mambo yasipoenda. Haijawahi kutokea wapiga kura kuwawajibisha wabunge waliowachagua kwa imani na matumaini hata kwa kuwapa maonyo kwa kutotekeleza waliyowatuma. Miaka 60 ijayo kama hatutabadilika tutakuwa palepale na titaendelea kulalamika. Rasirimali bila mipango mizuri hazina maana
 
Kama unampeleka kijana shule kutoka primary, secondary, advanced secondary yapata miaka 14, lakini kijana huyo hatokuwa na ujuzi wa aina yeyote unaohusiana na mazingira yake, kwamfano katoka kijijini kuna shamba, kuna mbuzi au ng'ombe lakini sisi hakuna tulicho mwelewesha juu ya kwenda kuyaendeleza mazingira yanayo mzunguka bali tumemfundisha logarithms na velocity formula ya ndege as if tunahitaji marubani tu, huku hata technologia ya kutengeneza ndege hatuna. ni kwa muujiza upi you expect kijana mwenye miaka ishilini hajapewa skill zozote ataweza kujikwamua kiuchumi?. Pili tumeruhusu aridhi kuhodhiwa na watu kiholela hata kama haiendelezwi lakini vijana wachache wenyebahati wakitaka aridhi waweze kufanya uthubutu imekuwa changamoto na hata wakifuata kwenyemaharimashauli rushwa imewekwa mbele na wakati vijana wetu wanamitaji labda hafifu. Ajira pekee sasa imekuwa bodaboda shughuli ambayo siyo ya uzalishaji. ni kwa namna gani taifa litaendelea?. Education reform and better land management that gives land access to our people its the only options we have for better tanzania
 
Acha chuki polepole ni mbunge Ana Haki Kama makamba, mwache ale mema ya nchi.ndiyo utaratibu tulionao.
Sijajua, mleta mada anataka Serikali isikope - viongozi wajitolee kazini?

Dhana ya umaskini ametumia parameters zipi kuubaini?

(a). Mtanzania wa mwaka 1961 alipata huduma ya elimu kwa kutembea umbali mrefu, leo ipo?

(b). Mtanzania wa mwaka 1961 alitembea umbali mrefu kupata huduma za afya - leo ipo hivyo?

(c). Mtanzania wa mwaka 1961 alisafiri wiki mbili KM 1500 toka Kigoma - Dar, - leo ipo? Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya siasa akina Prof Lipumba kwenye jukwaa walishutumu Serikali ya CCM kuhusu Miundombinu ya barabara kuwa ya vumbi - leo wanaweza?

Dhana ya umaskini ni pana na Serikali ya CCM imejitahidi kujenga Miundombinu ili ichoche juhudi za watu kujikwamua. Lkn pia kukopa si jambo baya labda kama kuna shida ktk matumizi ya mikopo hiyo.
 
Umasikini ni nature, Hakuna mwafrika yeyeto anaeweza mletea maendeleo mwafrika mwenzake.
 
Nchi nyingi za kiafrika ndivyo zilivyo, iangalia Kongo.
Tatizo ngozi nyeusi bado haijastaarabika. Yaani haijafikia katika hatua ya juu ya ubinadamu.

Hapo hata ichukue CHADEMA au CHAWATA hali inaweza kuwa mbaya zaidi.
Nature
 
Hilo kwa kweli ni tatizo kubwa sana. Imagine Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya nk. wote hao utakuta wanatumia zaidi ya gari moja kwa siku. Tena magari ya gharama kubwa ...... Wengine mpaka wanatumia magari ya serikali kupeleka watoto wao mashuleni. Tanzania nafikiri nchi inayoongoza kwa serikali kuwa na madereva wengi .....!!

Personally, huwa anangalia kampuni kama ya TANROAD au TRA hivi kweli hao Maofisa na Mainjinia hawawezi kujiendesha wenyewe. Yaani mtu kwenda lazima apelekwe na kurudishwa naa Driver .... Engineer mzima!!

Kuna watu wanaendeshwa na Madereva mpaka kwenye michepuko yao ..... Yaani ni kama vile serikali imebariki hayo ....Pathetic!!
Tza ndio nchi inayoongoza kwa viongozi vyake kuwa na magari ya kifahari Kazi yake kuu ni kupeleka watoto shule, kiongozi kazini na kwenye ibada. Jumla ya magari 600 yapo. Gari moja si chini ya milioni 200.
Uongozi ni ajira binafsi.
Hakuna mwafrika anaeweza mletea maendeleo mwafrika mwenzake.
 
Back
Top Bottom