Raisi wa Kwanza alikuwa na maono na akayaweka wazi umasikini na ujinga ndo vitu vikubwa vinavyoikumba Nchi hii hakuna kingine, Sasa waliokuja ilitakiwa wakomae kwenye hayo mawili hata kwa mijeledi watu wasome na walioelimika wapewe kazi wafanye na walipwe vizuri Ili wajiondolee umasikini kitu ambacho kingefanya wasio soma na wasiopenda shule wasome kwa bidii Ili wapate kazi na walipwe vizuri Sasa hakuna mkazo hapo kwenye kuwapa watu pesa inaonekana ni anasa kitu ambacho kinazidi kuzalisha umasikini, haya huku kwenye ujinga kwa vile upo sana sehemu za kijijini ilitakiwa nguvu kubwa iwekwezwe huko kwa kupeleka umeme na Kila kijiji kifungwe tv kubwa za kutoa elimu na kuuzomea ujinga mbona zamani wasiosoma nasikia walikuwa wanachambwa mpaka wanakosa amani na nyimbo zipo? Eti asiyejuwa kusoma ni mjinga kabisa na akiletewa barua anaitembeza kwa Kila mtu Ili asomewe kilichomo? Ujinga ndo janga kubwa linalosabisha tunashangaa kwanini serikali ikope Kila siku maana wanaoweza kufanya pesa izunguke ni wachache na nisehemu za mjini peke yake napo kwa watu wachache, ukitaka kuamini ni kuangalia ni watu wangapi wanaona fahari kununua nguo nzuri na kuvaa, kula chakula kizuri, kununua bidhaa za umeme za kurahisisha kazi, kupika kwa vifaa vya kisasa, kujenga nyumba za binadamu na siyo za kama wanyama wa kufungwa kama siyo watu wa mjini? Hivyo vijiji vibadilishwe kwa haraka sana kwa kujengewa vitu vya kisasa kwa lazima na elimu itolewe kwa lazima Kila mtu ajue kusoma kwa lazima Ili ajue matumizi ya vitu kitu kitakacholeta kazi nyingi na wale wanaofanya kazi iwe binafsi au serikalini walipwe vizuri na serikali itunge sheria za kuwalipa watu vizuri Ili wajiondolee umasikini.Kuna wakati najiuliza tumemkosea nini Mungu wetu mpaka huu umasikini wa watanzania upo kwa miaka 60 sasa licha ya Mungu kuibariki nchi hii kwa kuipa raslimali karibu kila mkoa lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa?
Raslimali zilizopo Tanzania hakuna nchi ya kufanana nayo Afrika Mashariki na kati.
Viongozi wetu kwa miaka 60 ni wale wale chama ni kile kile lakini wameshindwa kuzitumia raslimali tulizopewa na mungu kuwaondolea umaskini wananchi wake, badala yake wameamua kuwatoza kodi za maumivu na kukopa nje mpaka deni la taifa limefika tril 71 lakini umaskini upo pale pale.
Binafsi naanza kuamini Tanzania tuna tatizo na Mungu ni wakati kama taifa kufanya maombi na kuombana msamaha kwa maovu tuliyofanyiana ili Mungu arudishe upendo wake kwa nchi tupate maendeleo na wananchi wanufaike na kuondokana na umaskini kwa kutumia raslimali alizotupa Mungu.
Kuna watu wapo magerezani kwa miaka kwa kesi za kuonewa, kuna watu wamepigwa risasi, wamepotea, wameuawa kwa uonevu tu.
Yote hayo Mungu hapendi na hasira ya Mungu huwa ni mateso kwa watu.