Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umaskini wa Tanzania wamduwaza Balozi EU
Na Muhibu Said
11th May 2010
Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Balozi Tim Clarke, amesema hajaona mabadiliko yoyote katika juhudi zinazofanywa kuikwamua nchi katika umaskini na kuwaletea wananchi maendeleo katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Balozi Clarke alitoa kauli hiyo kwenye kongamano la kuwapa sauti watu waliosahaulika, waliotambuliwa kama "makundi ya watu walioko pembezoni", lililofanyika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii, jijini Dar es Salaam jana.
Kongamano hilo liliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kwa kushirikiana na EU, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu Umoja huo uanzishwe.
Kongamano hilo lililenga kutoa fursa ya kuyafahamu makundi ya watu hao, mahitaji yao, namna wanavyojisaidia na namna EU itakavyowasaidia kuondokana na umaskini."Nilikuja Tanzania miaka 20 iliyopita, baadaye nikaondoka. Hali ya kilimo niliyoiacha vijijini tangu kipindi hicho, bado iko vilevile. Hatuwezi kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kuondokana na umaskini bila kuleta mapinduzi katika kilimo," alisema Balozi Clarke.
Aliyataja mambo ambayo yanapaswa kufanyika ili kuondoa umaskini kuwa ni pamoja na kuyatambua makundi yaliyoko pembezoni, kuwa na muono mmoja na kuunganisha sauti katika kudai na kuleta mabadiliko dhidi ya hali hiyo nchini.
Kauli hiyo ya Balozi Clarke iliibuliwa katika kongamano hilo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Ananilea Nkya, baada ya kuteta na balozi huyo wakati wa mapumziko mafupi yaliyotolewa na muongozaji wa kongamano kwa kila mshiriki kuweza kubadilishana mawazo na mwenzake aliyeketi jirani yake jinsi ya kuwakwamua watu hao na umaskini.
Awali, akizungumza katika kongamano hilo, Balozi Clarke alisema programu ya EU nchini inalenga zaidi kuisaidia serikali kupunguza umaskini.[FONT="[COLOR=red]]"Hivi kweli tunafanikiwa? Swali muhimu la kujiuliza, je, maskini wanazidi kuwa maskini? Na matajiri kuwa matajiri?" alihoji.[/FONT][/COLOR]
Aliwataka washiriki wa kongamano pamoja na Watanzania kwa jumla kuueleza bayana Umoja huo pamoja na wabia wengine wa maendeleo namna watakavyoweza kuboresha maisha yao."Hili ni kongamano lenu. Tuambieni ni kwa jinsi gani sisi na wabia wengine wa maendeleo tutaweza kuboresha maisha yenu," alisema Balozi Clarke.
Akiwasilisha mada kuhusu "rushwa inavyomuathiri mwanamke albino" katika kongamano hilo, Mjasiriamali kutoka kundi la albino, Nasra Mbonea, alisema rushwa imekuwa chanzo kikubwa cha mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) nchini kutokana na baadhi ya wenye fedha kuwahonga watu ili kuendesha vitendo hivyo vya kikatili.
Alisema mbali na kuuliwa kikatili, baadhi ya watu katika jamii wamekuwa na tabia ya kuwanyanyasa albino kutokana na shinikizo na mila potofu, huku mafuta yanayowasaidia kutunza ngozi zao (albino), yakiuzwa kwa bei kubwa.
Nasra alisema manyanyaso dhidi ya albino yamefikia hatua mbaya kiasi ambacho miili na ngozi zao, vimekuwa vikitumiwa na baadhi ya watu kama miradi ya kujinufaisha kiafya na kiuchumi kutokana na imani potofu."Albino wakiingia kwenye biashara, kama vile ya kuuza chakula, watu hawachangii. Wanamnyima hata lifti ya gari njiani kwa kuhofia kwamba ikipatikana ajali aliyetoa lifti ataonekana alikuwa anampeleka kumuuza au kumuua. Hivi sasa kuna imani imeibuka katika jamii kwamba, eti ukitembea (kufanya ngono) na albino unapona ukimwi au unakuwa tajiri, tunanyanyasika sana," alisema Nasra.
Alisema kama angekuwa Rais wa Tanzania, angetoa adhabu kwa mtu yeyote ambaye mahakama ingemtia hatiani kwa kosa la kumkata mkono albino, naye kukatwa mikono yote miwili, badala ya kumhukumu kifungo cha jela, ambacho alisema kinamnufaisha kwa vile huko anapata chakula cha bure kinachonunuliwa kwa kodi za wananchi.
Akiwasilisha mada kuhusu "elimu kwa wasioona Tanzania", Shella Gailos alisema hali halisi ya elimu haiendani na ubora unaohitajika kwani wanawake wasioona hawajanufaika, huku wakikabiliwa na changamoto ya kuwa na vifaa hafifu vya kujifunzia na kufundishia; kadhalika alisema masomo ya Hisabati na Sayansi hayafundishwi katika shule za sekondari za wasioona.
Akiwasilisha mada kuhusu "hali ya watu wenye ulemavu katika uchumi", Mjasiriamali kutoka kundi la Seba lililopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam, Cecilia Masika, alisema uchumi wa mtu mwenye ulemavu ni duni kulinganisha na asiye mlemavu, hasa mwanamke, kutokana na wengi wao kutopata elimu japo ya msingi.
Pia, alisema ajira kwa watu wenye ulemavu bado ni tatizo kutokana na dhana kwamba, hawawezi.
Alisema takwimu za walemavu walioajiriwa serikalini zikionyesha ni watu 736 tu na kwamba, waliwahi kutembelea viwanda 51 vya usindikaji na kushuhudia mlemavu mmoja tu ndiye aliyeajiriwa.
Alisema hali hiyo imesababisha wenye ulemavu waliosoma kulazimika kuingia kwenye sekta binafsi, ambako wanashindwa kuzimudu kutokana na kutokuwa na elimu ya sekta hizo.
Naye mwanamuziki wa Bendi ya The Seven Blind Beats, Boniface Kiyenzi, alisema kama angekuwa Rais wa Tanzania, angeanzisha wizara ya watu wenye mahitaji maalum kuliko ilivyo sasa ambayo ipo kama idara tu ya ustawi wa jamii na haitoi huduma kikamilifu kwa vile haipewi ruzuku ya kutosheleza mahitaji ya makundi ya wahusika.
Kongamano hilo lilichangiwa na washiriki wengi ambao walipendekeza kutiliwa mkazo elimu kwa makundi ya watu wenye ulemavu; wakiwamo walemavu wa viungo, wasioona, viziwi na albino. Pia, kuimarisha mawasiliano kati yao na watoa huduma mbalimbali, kama vile mahakama, polisi na hospitali.
CHANZO: NIPASHE
They're both mkuu,sorry for that.
But which dominates? They can't be equal, unless they are cursed!
Ukifika mjini huko ni balaa. Kuna watu wanashinda chini ya mwembe kuanzia asubuhi hadi jioni siku saba za week. Ila kuna wale ambao wanaonekana kama wametoka kidogo nao wana vituko vyao. Leo nimekutana na mama mmoja mfanyabiashara, akiwa benki anaweka karibia shs milioni 30 taslimu.
They're both mkuu,sorry for that.....those stuff most of da time goes hand to hand,its like a butter n bread....they facilitate each other.