Kwanini Watanzania wengi hawaiamini Mahakama?

Kwanini Watanzania wengi hawaiamini Mahakama?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Leo nilikuwa mahakamani ambapo nilikutana na mtu mmoja aliyenimbia kuwa ana kesi yake mahakamani lakini hana Imani kama mahakama itatenda haki.

Kwa uzowefu wangu ni kwamba watu wengi hawana Imani na mfumo wa mahakama ila hawana la kufanya kwa kuwa ni lazima mashauri yao yaamuliwe mahakamani.

Ni kwa nini watanzania wengi hawana imani na mifumo ya mahakama?
 
Rushwa ...

Mahakama inaendeshwa na mamraka kutoka juu,na upendeleo wa "huyu ni mtoto wa nan au familia ya Nan" ....

Kama huna pesa za kuhonga kesi yako itapuuzwa hata Kama unahaki ....
Kwa kweli hata ripoti ya Jaji Warioba iliitaja mahakama kama mojawapo ya taasisi zinazoendekeza RUSHWA nchini!!
 
Haki imegeuka bidhaa, inauzwa na kununuliwa.

Kwa upande wa siasa ndiyo kabisaa, maana mahakama imekuwa kama tawi la chama tawala
 
Mahakama zinatumiwa vibaya na wanasiasa, viongozi wa serikali na watu wenye uwezo wa kifedha kupindisha sheria

Kuna kitu wanaita technicalities 🤔(kama nakosea naomba kurekebishwa) wanatumia kukukomoa
Hata Rostam Aziz, ingawa aliomba msamaha, alichokisema ndo uhalisia. SIMU moja tu inabadili kila kitu
 
Leo nilikuwa mahakamani ambapo nilikutana na mtu mmoja aliyenimbia kuwa ana kesi yake mahakamani lakini hana Imani kama mahakama itatenda haki.

Kwa uzowefu wangu ni kwamba watu wengi hawana Imani na mfumo wa mahakama ila hawana la kufanya kwa kuwa ni lazima mashauri yao yaamuliwe mahakamani.

Ni kwa nini watanzania wengi hawana imani na mifumo ya mahakama?
1693998787648.png
 
Mahakama na police ni wamoja ndiomana hakuna imani. Ni taasisi za machokoraa ndiomana ofisi zao za kazi ni za hovyo
 
Kuna mtu kesi yake imekaa miaka mitatu hata kutajwa tu hakuna.

Akapewa ushauri kwamba nenda kwa makarani mwaga rupia kesi yako itatajwa hata wiki ijayo yeye akakaza fuvu.

Wenzake walikuwa na kesi tofauti na yeye kesi zikaisha.. yeye kabaki sijui haki yangu inacheleweshwa.

Yaani Tanzania hata kama hupendi rushwa utajikuta unatoa bila kupenda. Mifumo yetu imekaa leta kidogo nikusaidie.

Kama huna connection au hufahamiani na viongozi wa kisiasa na una kesi mahakamani. Ujue hiyo kesi utazungushwa mpaka uchoke.
 
Back
Top Bottom