Kwanini Watanzania wengi hawamtaki Waziri wa Nishati, January Makamba?

Paulsylvester

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2021
Posts
1,464
Reaction score
3,379
Ndiyo,
Napitia michango mingi kutokea mitandaoni, karibu Mitandao yote inayotumiwa na watanzania,

Wengi wao hawataki uongozi wa Waziri Makamba, ni kwa nini?

Mawaaziri ni wengi, lakini kwa nini iwe ni Makamba pekee asiyetakiwa na watanzania wengi?

Hata hivyo, wizara hii anayoiongoza, mawaziri wengi waliopita hapa, hawakuwahi kuzimaliza changaoto zilizopo hata Leo, licha ya hivyo, hakukuwa na kelele nyingi kama zinavyppigwa Leo kwa mh Waziri, kwa nini Makamba na sio kina Mhongo na kina ngeleja ambao hawakukataliwa waziwazi kama ilivyo leo

Je, Waziri analifahamu hilo,?

Na kama analifahamu anangoja nini kuachia madaraka, kunaumaana gani kufanya kazi ambapo watu wengi hawakutaki?
 
Sababu kubwa ni kwamba January ni mnjamjanja, pia amekua mwepesi wa kutafuta justifications badala ya solutions kwenye matatizo yanayo wagusa waTanzania wenye maisha ya chini moja kwa moja.

Ni waziri kijana anaedhani kwamba anaakili na yupo smart na anawaona waTanzania kama mazuzu.

Nimeona nieleze kwa kifupi kabisa.
 
Je Waziri analifahamu hilo,?

Ninajibu para ya mwisho.

Aache utamu wa uwaziri - thubutu!!!!
 
Watanzania wengi wanapenda majungu na kufuata mkumbo tu

USSR
 
Sababu kubwa ni kwamba January ni mnjamjanja, pia amekua mwepesi wa kutafuta justifications badala ya solutions kwenye matatizo yanayo wagusa waTanzania wenye maisha ya chini moja kwa moja.
Ni waziri kijana anaedhani kwamba anaakili na yupo smart na anawaona waTanzania kama mazuzu.
Nimeona nieleze kwa kifupi kabisa.
Kwa hiyo ndiyo sababu watu wengi wanampinga mtandaoni? Nakumbuka miaka ya nyuma kulikuwa ni migawo ya umeme ya kufa mtu lakini watanzania walikuwa kimya tu. Leo kaja Makamba, umeme umekatikakatika kidogo imekuwa nongwa juu ya nongwa! Kwetu huku Kisiwani tungesema Makamba ana damu ya kunguni na siyo kwamba si mtendaji mzuri!
 
Aisee!

Damu ya kunguni ndo nini mkuu
 
Wajibu wa viongozi ni kutatua changamoto katika Taifa na siyo kutangazia uma kuwa maisha yatakuwa magumu kutokana na changamoto.Taifa la Tanzania linaongozwa na vibaka.
FOeB-xHWQAwQwM7.jpg
 
Hii wizara tukiacha ukabila na udini Kalemani alipaweza sn kupita kiasi hata kama alikuwa na madhaifu yake lakini siyo kama Makamba

Kalemani ukiacha dhambi yake ya kunyofoa camera CCTV tukio la Lissu alifanya mambo makubwa Wizara ya Nishati.

Tatizo lake kubwa au dhambi yake kuu kwasasa ni kabila lake na dini yake.Kabla ya mwezi March 2021 hiyo ilikuwa ni sifa kuu na kigezo muhimu za kuwekwa Wizara nyeti na muhimu.

Tanzania bila Katiba mpya sifa za mtu zinabadilika kulingana atokako kiongozi mkuu wa Nchi.

Ngongo kwasasa Dodoma.
 
Hiki ndio ninachofikiri !

Si kwamba watanzania wa hali ya chini hawamtaki Makamba Jr bali wanakereketwa na namna anavyoshughulikia kero katika wizara husika .

Kwa mfano ; Kukatika katika kwa umeme na kuathiri zaidi watanzania wa hali ya chini sababu inaweza kuwa uchakavu wa miundombinu ambayo inaweza kuwa na mantiki kabisa ! Au kupanda kwa bei/gharama za nishati sababu inaweza kuwa kuongezeka kwa gharama za uzalishaji na soko la nishati duniani na hoja hii kuleta mantiki kabisa .

Sasa ndugu Makamba Jr yeye anaishia hapa na kukubali hizi sababu kama kizingiti cha mwisho ! Watanzania wengi ni masikini yeye kama kiongozi anatakiwa kutafuta na kufanya kila jitihada kwa kutumia “Leverages” zilizopo kwenye wizara yake ili kuweza kuleta nafuu kwa mtanzania wa chini .

Si kwamba watanzania hawaoni kuwa maisha yamepanda hata katika nyanja ya kiulimwengu bali wanataka kuona juhudi zaidi,ubunifu zaidi na kujitoa kwa dhati kwa viongozi .
 
Back
Top Bottom