Kwanini Watanzania wengi hawamtaki Waziri wa Nishati, January Makamba?

Kwanini Watanzania wengi hawamtaki Waziri wa Nishati, January Makamba?

Nakuona unavyolazimisha,

Hatutaki sasa, Fanya utakalo Ila hatutaki
Nakulazimisha kufanyaje? Nakuonyesha tuu anavyozidi kuupiga mwingi.

Hamtaki wewe na nani? Kwani toka mumeanza kusema hamtaki kipi mumebadili? 😆😆😆😆😆
 
Makamba hata mbingu hazimtaki. Anacheza sana na maisha ya watanzania wengi.
 
Nakulazimisha kufanyaje? Nakuonyesha tuu anavyozidi kuupiga mwingi.

Hamtaki wewe na nani? Kwani toka mumeanza kusema hamtaki kipi mumebadili? 😆😆😆😆😆
Makamba atatoka tuu....ni suala LA muda.
Ukiona mayowe kila kona jua panafuka moshi.
 
Wengi wasiomtaka Makamba Ni kundi la sukuma gang, ambao wameumia kuondolewa msukuma mwenzao Kalemani kwenye hiyo wizara, kwaiyo walitamani arudishwe msukuma mwingine ,

Na wengine wanamchukia Makamba sababu ya dini yake, na pia wanashaka nae huenda kutokana na uchapakazi wake January Makamba na hile hali yakutokuwa na skendo, Kuna uwezekano mwaka 2039 Samia akimaliza muda wake January akasimamishwa na Chama kugombea urais
Hizo ni ndoto za mchana
 
Ana bahati ya watanzania waliokuwa wamelala ndio wameamka kwa hiyo huo muamko ndio umemkuta yeye ofisini[emoji849][emoji849]
 
Hata mti wenye nyoka kupiga mawe pia.
Mkuu hii inatokana na sababu kuwa mti wenye matunda ndio ambao hurushiwa mawe. Pia ni eneo ambalo ndipo wanyama na ndege wala matunda utawakuta hapo.
 
Sababu kubwa ni kwamba January ni mnjamjanja, pia amekua mwepesi wa kutafuta justifications badala ya solutions kwenye matatizo yanayo wagusa waTanzania wenye maisha ya chini moja kwa moja.

Ni waziri kijana anaedhani kwamba anaakili na yupo smart na anawaona waTanzania kama mazuzu.

Nimeona nieleze kwa kifupi kabisa.
Anajiona ni mwenye akili kuzid yeyote apa Bongo,kumbe bure kabsa kichwan,kazi yao ni kulamba asali tu
 
Hata mti wenye nyoka kupiga mawe pia.
Si kawaida kuwakuta nyoka wengi wakiwa wamejazana katika mti mmoja. Na pia kumbuka dhumuni la kuupiga mawe mti wenye nyoka ni kwa kutaka matokeo hasi, yaani kumuua kiumbe huyu hatari kwa maisha ya wanadamu na kisha biashara huishia hapo.

Lakini lengo la kuupiga mawe mti wenye matunda, ni kutaka kupata matokeo chanya, yaani uzidi kutetema na kuangusha chini matunda. Na zoezi hili hujirudia kila msimu wa matunda ukifika.

Cha kushangaza sana, hata msimu wa 2030 badi haujafika, mahasimu tayari wameshaanza kurusha mawe mtini! Je! Ukifika rasmi si watatumia mabomu ya mkono na silaha nzito za kivita!?
 
Back
Top Bottom