Said Stuard Shily
JF-Expert Member
- Jul 18, 2017
- 2,396
- 2,108
MAKAMBA HANA NIA NJEMA NA NCHI HII
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona sababu nyingi tu zilishatolewa humo kwenye mitandao, bungeni na sehemu nyingi mbali mbalikuhusu under perfomance ya huyu waziri. Sababu hizi ni pamoja na zifuatazo:Mawaaziri ni wengi, lakini kwa nini iwe ni Makamba pekee asiyetakiwa na watanzania wengi?
Kama walivyokuwa wakati wa Jiwe. Nitumbue nisitumbue, Tuuumbuaaa!! Hatujabadilika.Watanzania wengi wanapenda majungu na kufuata mkumbo tu
USSR
Hatari snNakubaliana na wewe
Ukweli ni kwamba January hana makosa.Watanzania wengi wanapenda majungu na kufuata mkumbo tu
USSR
hahahaaaa . . . . . eti bogus maandaziShida ya makamba nikujiona smart sana kuliko mawaziri wote wakati watanzania tunamuona ni bogus maandazi tuu.aswa pale anapojifanya kuea anamudu majukumu yake huku ana bolonga
Comment Bora KABISA Hii,Mbona sababu nyingi tu zilishatolewa humo kwenye mitandao, bungeni na sehemu nyingi mbali mbalikuhusu under perfomance ya huyu waziri. Sababu hizi ni pamoja na zifuatazo:
1. Amesema kukatika katika kwa umeme kutaendelea hadi mwaka 2025 watakapomaliza kununua na kufunga transformers na vikombe kwenye line zote za tanesco. Na kwamba hii ni sayansi ambayo wananchi hawapaswi kuhoji.
2. Hayo matransformers na vikombe vinanunuliwa kutoka ulaya kwa matrillion ya pesa badala ya kuyanunua kutoka kwenye viwanda vya hapa nchini hususani vile vya TANLEC kama tulivyokuwa tunafanya hapo awali. Hata nguzo sasa zinanunuliwa kutoka nje badala ya zile za Mufindi ambazo sasa wanasema hazina ubora wa kimataifa.
3. Kakodi software ya tekohama kutoka kwenye kampuni ya magari ya Mahindra iliyo nchini India kwa gharama ya dola 30 milioni kila mwezi/ mwaka (?). Hii haina tofauti na capacity charges tulizokuwa tunakamliwa na makampuni ya umeme.
4. Kanunua nje winch la mabillion ya pesa la kubeba milango ya tani 26 kwa ajili ya kufungwa kule kwenye bwawa la umeme la Nyerere (JNHPP) ili bwawa hilo lijazwe maji mwezi Novemba 2021. Hadi sasa winch hilo halijafika na sasa anasema hata likifika halitaweza kufanya kazi hiyo kwani msingi wa pale mageti hayo yanapopaswa kuwekwa haufai. Msingi huo unahitaji matengenezo makubwa na hivyo bwawa hilo litaanza kujazwa maji mwaka 2024 kwani haya ni mambo ya sayansi!
5. Katika mikoa mingi tu hapa nchi wananchi hawaoni hayo mavikombe na matransfomer yakifungwa. Sana sana wanaona yale ya zamani yakitengenezwa pale panapotokea hitilafu kama zamani. Hata CAG hataweza katika ukaguzi wake kubainisha vikombe na transformers za zamani na zile mpya zilizonunuliwa kutoka ughaibuni.
6. Uzalishaji kwenye viwanda vyetu umekuwa wa kusuasua kwa sababu ya ukosefu wa umeme. Hii inapelekea bidhaa nyingi kupanda bei. Pia inazuia wawekezaji wapya wa viwanda kuja nchini kwetu. Hivyo ile ilani ya ccm ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025 inakuwa ni ndoto ngumu kuwa kweli.
7. Adhima ya kuwa na umeme kwa vijiji vyote na vitongoji vyote ifikapo 2022 imeshindikana kwani umeme hautoshi.
8. Installed capacity ya mitambo yetu ya kuzalisha umeme tuliyo nayo ni MW 1,700 kwa siku. Matumizi yetu hayazidi MW 1,200 kwa siku. Sababu zinazotolewa kwa nini tuna uhaba wa umeme tangia Januari na Maharage wachukue uongozi hazieleweki na zimekuwa zinabadilika kila kukicha.
9. Huko kwenye nishati ya mafuta nako hakufurahishi. Mpango wa kufufua au kujenga oil refineries zetu hapa nchini umetupiliwa mbali. Mpango wa kuchimba mafuta yetu kwenye maeneo yaliyokwisha kubainika hapa nchini nao umetupiliwa mbali etc etc. Pia wananchi hawaoni namna bora inayochukuliwa na wizara hii kukabiliana na upandaji mkubwa wa bei ya mafuta uliosababishwa na mlipuko wa uviko kumalizika na vita ya Urusi vs Ukraine.
Sukuma gangKwa hiyo ndiyo sababu watu wengi wanampinga mtandaoni? Nakumbuka miaka ya nyuma kulikuwa ni migawo ya umeme ya kufa mtu lakini watanzania walikuwa kimya tu. Leo kaja Makamba, umeme umekatikakatika kidogo imekuwa nongwa juu ya nongwa! Kwetu huku Kisiwani tungesema Makamba ana damu ya kunguni na siyo kwamba si mtendaji mzuri!
Mh. Makamba anavyochukiwa ni kama ilivyo kwa Mh. Rais Mama yetu mpendwa Samia. Makosa aliyoyafanya Mh. Makamba yameanzia kwa Mh. Rais Mama Samia. Mtiririko wa makosa iko kama ifuatavyo:Ndiyo,
Napitia michango mingi kutokea mitandaoni, karibu Mitandao yote inayotumiwa na watanzania,
Wengi wao hawataki uongozi wa Waziri Makamba, ni kwa nini?
Mawaaziri ni wengi, lakini kwa nini iwe ni Makamba pekee asiyetakiwa na watanzania wengi?
Hata hivyo, wizara hii anayoiongoza, mawaziri wengi waliopita hapa, hawakuwahi kuzimaliza changaoto zilizopo hata Leo, licha ya hivyo, hakukuwa na kelele nyingi kama zinavyppigwa Leo kwa mh Waziri, kwa nini Makamba na sio kina Mhongo na kina ngeleja ambao hawakukataliwa waziwazi kama ilivyo leo
Je, Waziri analifahamu hilo,?
Na kama analifahamu anangoja nini kuachia madaraka, kunaumaana gani kufanya kazi ambapo watu wengi hawakutaki?