Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?


Aisee inatisha sana wangekuwa wanawaficha wale wengine sio poa kabisa na siwezu shuhudia aiseee
 

Aiseee yaan hapo kwa ng’ombe wanaonea sana mpaka nimelia ,unajua ngombe huwa ana macho fulan hivi yanatia huruma kabisa sijui huwa ana huzuni muda wote na sielewi kwanini iliwekwa tuwale wanyama hawa ambao nao wana roho
 
Dunia ya kupenda wanyama
Nikaumbwa nikimuhusudu mnyama Nyoka ,Nawapenda sana Nyoka maisha tuloumbiwa na huyu mnyama ni kama Vita[emoji28][emoji28][emoji28]

[emoji23][emoji23] nyoka anatisha jamani
 
Hulka iliyorithiwa:
Bundi kasimama juu ya nyumba usiku, ooh! uchuro. Kumbe anajiimbia zake bongo fleva🙁huuu huuuu!! huu huuuu!!)
 
Kuna Hii tabia ya kuwapiga bundi kila Mara,
Uyu ndege kila anapoonekana lazima auwawe TU, amekua Kama nyoka Sasa.

Huu ukatili sijui lini utafika mwisho
 

Hao paka hawana mtu bali huzaliana kwenye sehemu za mlo
Na riziki wanapata hapo hapo
Niliuliza wakasema sio wetu ni kama panya tu
 
Usisaidie Masikini kwani tabia zao ni zakishetani!
Na wengi ndio wenye tabia hiyo.

Afu atakuambia Paka ati anatumwa na wachawi [emoji3][emoji3] huoni hapo kunatatizo la msingi.
Kumhusisha Paka na matatizo yako ni Dalili ya kutojitambua
Point [emoji4][emoji106]
 
embu waza unakula samaki wa kuokwa/ nyama chomaa/ etc halafu paka anakuja anakukodolea macho na yalivyo makaliii hahaaaa lazima nimbamize kwa tonge la ugali

na umtizamapo machoni huruma inakujia unawaza anahisi njaa

Paka nawachukia kwa sababu hawaridhiki hata umpe nini bado atakuzungukia tu
Tofauti kabisa na Mbwa
Mbwa ni wazuri sana maana akishiba atalala zake hakusumbui na wewe utakula kwa amani
 

Ametunga hii story sidhani kama ana roho chafu kiasi hicho ingawa binadamu anafanya mengi

Watoto hawajui kitu wanatakiwa kufundishwa maadili
Yaani umtupie mtoto mbwa je kama angemuua?
Halafu eti Polisi wakaiacha kesi iishe tu

Hakuna ukweli hapo
 
Kuna Hii tabia ya kuwapiga bundi kila Mara,
Uyu ndege kila anapoonekana lazima auwawe TU, amekua Kama nyoka Sasa.

Huu ukatili sijui lini utafika mwisho

Jamaa alijenga nyumba sehemu ilikuwa bado pori na bundi walikuwa wengi sasa ndugu wakija hawalali kwa kelele
Siku moja mshkaji kashindwa kulala katoka na Pistol kauwa mmoja
Mwenyewe katoka akidhani mwizi
Bundi wawili walikufa siku hiyo wengine wakakimbia

Tatizo ndio likaanza
Nyoka waliongezeka sana kwa sababu walipata amani kwa Bundi

Kila kiumbe kina sababu ya uwepo wake
 
Aisee me nisingekuwa na mudA wa Kuna kukuuliza Wala kuendesha kesi ilikuwa ni kuwatia vilema wote wewe na mbwa wako,huwezi linganisha thamani ya mtoto na ya mbwa,never hata kiuumbaji Mungu alimpendelea zaidi binadamu
Lakini usisahau. Unaweza ukaenda na hasira zako kwa nia ya kutia vilema wote yeye na mbwa wake halafu kibao kikageuka na ukajikuta wewe ndo unatiwa kilema. Hilo pia linawezekana au vp. Hasira Hasara.
 
Nakazia.
 
Hongera zako ila jiongeze na kwa upande wa Wadudu uwapende pia usiwatendee jeuri. Utabarikiwa sana mkuu.
 
Kuna Hii tabia ya kuwapiga bundi kila Mara,
Uyu ndege kila anapoonekana lazima auwawe TU, amekua Kama nyoka Sasa.

Huu ukatili sijui lini utafika mwisho
Imani za Kishirikina ndo kisababishi kikuu. Imani hiyo ikiisha basi na Ukatili dhidi ya wanyama hao utakua kwishney.
 
Yani kunguru apite mbele yangu akae site nzuri jiwe linamuhusu
Kwa sababu gani?? Umekosa cha kufanya? Mbona wakipita mbele yako vibaka, wezi, wahuni na watu wa namna hiyo na pengine unawafahamu wana tabia hiyo jiwe haliwahusu?
 
Napenda sana mbwa, hawa viumbe wana mapenzi ya dhati kiukweli, ni wavumilivu sana, wapo tayari kufa ili waukokoe.
Yap! Hongera sana mkuu. Watu wanajisahau sana kiulinzi. Eti mtu ananunua bunduki ili ajilinde lakini anasahau kwamba hapo ni yeye ndiye anageuka kuwa mlinzi wa hiyo bunduki kwani akijisahau kidogo tu "wenyewe" wanakuja kuichukua na wala hiyo bunduki haitapiga kelele kumuamsha kwamba kuna kitu sio cha kawaida huko nje na Polisi watamsumbua atoe maelezo ilikuwaje-kuwaje bunduki kupotea?
Tofauti na Mbwa atakuamsha ili ujiweke tayari kuna kitu huku nje ujiandae na bado haishii hapo tu bali atakuwa bega kwa bega na wewe kwenye mapambano ili akuokoe wewe na mali zako.
NB: Sijasema au kushauri watu msinunue bunduki. La hasha. Nunueni kwa Amani zenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…