umenikumbusha utotoni nilkua na hyo tabia ya kuwinda mijusi na kuifanyia operation kwa kiwembe, akifa naenda kuzika..nilitenga kabisa makaburi na mochwari ya mijusi.
Nilkua katili kwa wadudu yani walikua wakiniona wanaanza mbio...ila cha kushangaza kwenye ndege na wanyama hawa nilkua na huruma nao sana.Nilkua siwezi kuchinja kuku kabisa, walikua wakichinja kama kuku namjua nilkua nalia hatari 😂 , bora nifuge kuku mpaka afe mwenye kuliko kuchinja.
Siku hizi niko peace na viumbe hai sipendi kuvidhuru, nikiona watu wana piga wanyama najisikia vibaya niko radhi nikule hela uache kumpiga huyo mnyama.
Kuna siku nilkua natoka kwenye mishe zangu maeneo flani hivi nikakutana na mzee fulani alikua watoto wameshika mbwa wawili mmoja mkubwa kengine kadogo, cjui hata hao mbwa waliwakosea nini.
Walikua wanataka kuwaua kwa kuwa nyonga ( just imagine ) kwanza hao mbwa walikua wamesha chapika hatar...pona yao ilikua ni mimi kutokea.
Niliwaomba wasiwadhuru hao mbwa lakin wapi mpaka nikatoa buku ten nikampa huyo, uzur alkua ni choka mbaya alikubali akanipa hao mbwa.
Niliwahudumia hao mbwa asee jinsi nilivyo wakuta na walivyo kuwa ni vitu viwili tofauti.Na huyo mbwa mkubwa kumbe alkua na mimba siku alivyozaa cjui alifuata nini barabarani akapigwa tairi na gari la wagonjwa akafa.Aliacha vitoto 6 vidogo hatar hata havioni kasheshe ikawa ni kuvilea, sema nilipambana navyo mpaka vikakua vikubwa.