#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

Hizo chanzo zilivumishwa kuwa ni namba ya mpinga kristo, mara ikavumishwa zinaingia kwenye DNA.

Zina uzushi mwingi ambao umewatisha wananchi.
Lakini ukweli ni kwamba zinasaidia kujikinga na covid kwa asilimia nyingi.

Leo nimekaa sehem huku ughaibuni ,,kuna jamaa kainuka ghafla na kuanza kushangilia baada ya yeye na familia yake kuruhusiwa kupata chanjo. Kimoyomoyo nikasema watanzania wanaweza mwona mwehu huyu jamaa.

Huku chanjo bado ipo kwenye magroup maalaum hivyo vijana inawawia vigumu sana kuchanjwa.
 
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19,
Kwa hali Hii serikali inatakiwa iangalie kwa namna nyingine kwa Maana nchi na uongonzi wake ni watu ambao ni watanzania wala siyo kulazimisha ,naamini kupitia Rais wetu itaangalia zaid maoni ya Watanzania
Mapendekezo yangu
1)Serikali iwe na Msemaji Mkuu wa Covid 19 ambaye ni Dr hasa kama katibu Mkuu prof Abel Makubi , awe siyo Mwanasiasa
2)Swala la chanjo huwezi lipinga kwa maana ndio Suluhisho la Kudhibiti ugonjwa tunakoelekea
3) Kwa Hali ya uelewa chanjo kwa sasa serikali isilazimishe ielewee wananchi wengi wako kwanin hawaitaki chanjo
4)Serikali iendele kusimamia njia za kujikinga na ugonjwa ichukue hatu kali bila kujali watanzania wanasemaje kwa ajili ya faida ya afya wengi
Hii nchi wajinga ni wengi, hivyo unashangaza kushangaa kuwa wengi wamekataa chanjo. Hata hawajui wanakataa nini. Hakuna mjanja anaikataa chanjo....[emoji851]
 
Chanjo iliyotengenezwa ndani ya mwaka mmoja, hakuna conclusive research iliyofanyika kuweza kupata final approval, hakuna data za mid- and long-term effects. Short-term effects zimeshaonekana, efficacy ipo chini lazima uchanje kila miezi 6, ni teknolojia mpya ya utengenezaji wa chanjo inayohusisha vinasaba DNA/RNA imeshaleta complications za autoimmunity kama blood clots, autoimmune thrombocytopaenia, sijui tunakimbizana kwenda wapi? au ndo presha za mabeberu hizi.....
Hizo zingine ulizozipata zilikaa muda gani baada ya kutengenezwa ndipo zikatumika? Mmejazwa mawazo ya mtu mmoja na wafuasi wake, kiasi hamuwezi kufikiri independently. Aliwakamata sana.
 
Technology ya mRNA hiyo hiyo ndio inatumika kutengeneza chanjo ya haraka ya HIV na imeonyesha mafanikio makubwa sana katika awamu ya kwanza ya majaribio.

Na inatumika pia katika kutengeneza chanjo cha magonjwa mengine.

Tatizo watanzania hatukutumia wataam wa afya tuliwasikiliza watu ambao sio wataalam, kutoka katika hali hii itachukuwa muda mrefu.

Mungu hawezi kuwapenda TZ peke yake na kuwaangamiza wengine Dunia mzima tuache ujinga huo vile vike Corona imeua watu wengi TZ na bado wave la 3 hatujui litakuwaje.
 
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19,
Kwa hali Hii serikali inatakiwa iangalie kwa namna nyingine kwa Maana nchi na uongonzi wake ni watu ambao ni watanzania wala siyo kulazimisha ,naamini kupitia Rais wetu itaangalia zaid maoni ya Watanzania
Mapendekezo yangu
1)Serikali iwe na Msemaji Mkuu wa Covid 19 ambaye ni Dr hasa kama katibu Mkuu prof Abel Makubi , awe siyo Mwanasiasa
2)Swala la chanjo huwezi lipinga kwa maana ndio Suluhisho la Kudhibiti ugonjwa tunakoelekea
3) Kwa Hali ya uelewa chanjo kwa sasa serikali isilazimishe ielewee wananchi wengi wako kwanin hawaitaki chanjo
4)Serikali iendele kusimamia njia za kujikinga na ugonjwa ichukue hatu kali bila kujali watanzania wanasemaje kwa ajili ya faida ya afya wengi
corona ipo, "heri kuzuia kuliko kuponya"
 
Yule mkemia aliwamisha watu vibaya kwa kusema papai lina Corona,
 
Random research mie. Nimeifanya kwa majirani,ndugu,marafiki na ofisini kama watu 30 hivi wanaokubali chanjo kati ya wote ni wawili tu....ni wazi kuwa watu hawajaikubali kiukwel...
 
EaniE
Kama ulisikiliza siku ya kukabidhi report ya Covid 19, serikali haikusema chanjo ni lazima, ilisema chanjo ni hiari. Wanajua bado kuna watu wako na njozi za mwendazake, kwa hiyo hawawezi kulazimisha. Muda utafiki hata wale wenye mawazo ya mwendazake wataelewa na maisha yatakwenda vizuri. Wapewe muda maluweluwe yawatoke kichwani

Kama ulisikiliza siku ya kukabidhi report ya Covid 19, serikali haikusema chanjo ni lazima, ilisema chanjo ni hiari. Wanajua bado kuna watu wako na njozi za mwendazake, kwa hiyo hawawezi kulazimisha. Muda utafiki hata wale wenye mawazo ya mwendazake wataelewa na maisha yatakwenda vizuri. Wapewe muda maluweluwe yawatoke kichwani.
Niambie nchi moja duniani ambapo hii chanzo ni lazima?
Japan nchi tajiri inayotegemea kupokra ugeni mkubwa wa michezo ya Olympic imechanja 3% tu ya watu wake!
Wewe jipeleke ugeuzwe panya wa majaribio, ukimiona Biden anachanjwa kwenye tv unaamini eti?
 
Wazazi waliopewa taarifa kuwa watoto wao watapata chanjo shuleni jumatatu ya wiki hii(bahati mbaya taarifa haikusema chanjo gani) waligoma watoto wao kwenda shule hiyo siku, wilaya nzima shule zilikuwa tupu, baadae ikabidi walimu waeleze kuwa watoto watapewa dawa za kichocho ndipo wazazi wakawaruhusu watoto kwenda shule!
Kama wazazi wamefikia hatua hiyo unadhani kuna mtu atakubali chanjo hizo hivi hivi?
 
Shida iko wapi? Chanjo iletwe anayetaka atumie asiyetaka aache. Tusiwanyime watu fursa ya Kinga kwa hofu zetu
Hivyo sivyo ambavyo serikali inatakiwa kudeal na hili suala kwa sababu serikali ya awamu ya tano ambapo viongozi wake ndio hawa hawa wa awamu ya sita ndio hao wanahusika moja kwa moja na hili la wananchi kutilia mashaka chanjo au kukataa kabisa, kama waliwaambia wananchi kuwa hakuna corona wao kama serikali na wakatilia shaka chanjo basi hilo wanapaswa kulifix kwanza ila sio kusema walete chanjo halafu et atakayetaka achanjwe na asiyetaka basi.
 
Hizo zingine ulizozipata zilikaa muda gani baada ya kutengenezwa ndipo zikatumika? Mmejazwa mawazo ya mtu mmoja na wafuasi wake, kiasi hamuwezi kufikiri independently. Aliwakamata sana.
Mimi nimeongea swala kitaalamu wewe unakuja na porojo, unapataje approval ya chanjo ndani ya mwaka mmoja!? ume establish vipi mid- and long-term effects kwenye huo mwaka mmoja. Wewe ni mgeni dunia hii hadi hujasikia madhara ya hizo chanjo, kuganda damu, vifo nk. na kwamba watu waliochanjwa bado wanaweza kuugua. Chanjo unayohitaji booster ndani ya miezi sita? hiyo haiwezi kuwa chanjo, labda kitu kingine.....
 
Nimetabiri tu mkuu, sidhani kama itakua hiari to that extent. Labda tusubiri tuone itakuaje ila lazma tu kuna kanguvu katatumika kupush hiyo chanjo, kuhusu kusambaza elimu zaidi kibongo bongo ni wachache watakaoikubali hiyo elimu ndgu.
Haiwezi kuwa lazima..!
 
Chanjo iliyotengenezwa ndani ya mwaka mmoja, hakuna conclusive research iliyofanyika kuweza kupata final approval, hakuna data za mid- and long-term effects. Short-term effects zimeshaonekana, efficacy ipo chini lazima uchanje kila miezi 6, ni teknolojia mpya ya utengenezaji wa chanjo inayohusisha vinasaba DNA/RNA imeshaleta complications za autoimmunity kama blood clots, autoimmune thrombocytopaenia, sijui tunakimbizana kwenda wapi? au ndo presha za mabeberu hizi.....
Wewe kilaza usiyeweza hata kutengeneza dawa ya minyoo wa mbuzi leo hii unawafundisha wataalam namna ya kutengeneza na ku-approve chanjo! Jikalie kimya acha wanaotaka kuitumia wafaidike.
 
Ni vyema ukaweka hiyo evaluation imefanyaa na nan au taasisi gan na kugundua watanzania weng hawataki chanjo
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19.

Kwa hali Hii serikali inatakiwa iangalie kwa namna nyingine kwa Maana nchi na uongonzi wake ni watu ambao ni watanzania wala siyo kulazimisha ,naamini kupitia Rais wetu itaangalia zaid maoni ya Watanzania.

Back
Top Bottom