#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

Sababu ya ujinga uliojazwa vichani mwao ni incompetent magu
 
Wewe kilaza usiyeweza hata kutengeneza dawa ya minyoo wa mbuzi leo hii unawafundisha wataalam namna ya kutengeneza na ku-approve chanjo! Jikalie kimya acha wanaotaka kuitumia wafaidike.
Kilaza ni wewe ambaye huna hata akili ya ku comprehend nilichokiandika zaidi ya kutukana......argument unazoweza kuzimudu ni za kwenye vijiwe vya kahawa...
 
Tanzania kinachoisumbua ni elimu. Watu wengi hawajaenda shule na wale walioenda shule elimu zao ni za kukariri. Pia exposure inawasumbua sana. Nchi zilizoendelea ni wachache wanapinga hii chanjo. Nashangaa tapeli kama Gwajima anawafundisha watu ''sayansi'' ya matango pori na baadhi ya watu wanakubali.
 
Kilaza ni wewe ambaye huna hata akili ya ku comprehend nilichokiandika zaidi ya kutukana......argument unazoweza kuzimudu ni za kwenye vijiwe vya kahawa...
Sijatukana labda matusi kwenu iwe ni kuambiwa ukweli. Kilaza ni mtu aliyeenda shule lakini elimu haimsadii. Nimekuuliza wewe una utaalam wa kutengeneza chanjo? Umewahi kutengeneza? Kitu ambacho huna utaalam nacho unaweza kukitolea elimu?
 
au ndo presha za mabeberu hizi.....
Utaambiwa wewe ni mmoja wa wale wanotaka Tanzania iwe imara kwa kila sekta (MATAGA), utadhani MATAGA ni dhambi. Sasa unajiuliza hawa kama hawataki Tanzania kuwa imara wao tutawaaminije kwa kutushauri tuchanje chanjo ambayo hata huko ilikotengenezwa wanaishuku chanjo hiyo..!

Ukiona mtu anachukia kusikia Tanzania kuwa imara yaani iwe Great Again, ujue kuna shida mahali yawezekana si mtanzania mwenye nia njema na Tanzania.
===
Turuhusu wataalamu wetu wa tiba wajiridhishe na usalama wa chanjo bila bughudha. Na tuache kutiliana mashaka katika suala la chanjo.
 
Sijatukana labda matusi kwenu iwe ni kuambiwa ukweli. Kilaza ni mtu aliyeenda shule lakini elimu haimsadii. Nimekuuliza wewe una utaalam wa kutengeneza chanjo? Umewahi kutengeneza? Kitu ambacho huna utaalam nacho unaweza kukitolea elimu?
Process ya kutengeneza chanjo inapitia hatua za utafiti na kila hatua lazima utoe publications wataalamu mbalimbali dunia nzima wasome na wajiridhishe, sasa hiyo chanjo iliyopita kama mbio za mwenge nani ataiamini, ni chanjo ipi iliyowahi kupata approval ndani ya mwaka mmoja...
 

Kwasababu mwaka jana waliingiza siasa za uongo na itachukuwa muda kubadilika. Chanjo hata hazipo watu wakianza kupiga watabadilika
 
Hizo zingine ulizozipata zilikaa muda gani baada ya kutengenezwa ndipo zikatumika? Mmejazwa mawazo ya mtu mmoja na wafuasi wake, kiasi hamuwezi kufikiri independently. Aliwakamata sana.
Huyu Nyumisi ni kilaza per se. Nikimwamia anasema namtukana. Hajiumizi hizo chanjo nyingine zinazotumika sasa hivi ambazo na yeye amechanjwa zilitengenezwa zikawekwa stoo tu mpaka miaka mingi ilipoisha ndiyo zikatumika? Hajui mara baada ya majaribio ya mwanzo kuonekana zinafaa zilianza kutumika?
 
Hayo majaribio waliyafanya wapi, unazo hizo data? maana zimetengenezwa ndani ya mwaka mmoja na zikaanza kutumika moja kwa moja kwa watu.
 
Hizi chanjo zimepitia hatua zote na wataalam wamejiridhisha ndiyo maana wakapitisha. Maendeleo ya teknolojia na utaalam yamewezesha hayo. Sasa mazee wewe umekariri mambo ya zama za mawe 🤣 🤣 🤣. Unashangaza sana. Hapo pengine uko Bongo unachati na mimi pengine niko USA, zamani ilikuwa inawezekana? Wewe endlea kujifungia kwenye blanketi la kukariri wenzako wanachanja mbuga.
 
Hayo majaribio waliyafanya wapi, unazo hizo data? maana zimetengenezwa ndani ya mwaka mmoja na zikaanza kutumika moja kwa moja kwa watu.
Mazee ulikuwa unaishi dunia gani kwa mwaka mmoja ulipita? Yaani unajitoa ufahamu kuwa hukuwa unasoma habari za majaribio ya chanjo tangu mwaka mwaka jana? Unaelewa kiingereza? Kama unaelewa basi google kuna makalana papers nyingi kuhusu majaribio tangu mwanzo mpaka dawa ilipopitishwa kutumika.
Haya angalia uone majaribio yalivyoanza
 
Chanjo ni mojawapo ya kujikinga.
 
Ni hawa hawa Al jazeera walitutahadharisha kuwa kimbunga Jobo kitaimaliza Dar es Salaam na viunga vyake. Lakini siku walizotabili kimbunga hicho kitatua Dar es Salaam ndiyo muda wa Shehena la mihadarati la uzito wa karibu tani mbili lilikamatwa na vijana wetu imara. Na habari za kimbunga JOBO zikawa zimepotea!!!

Kwa hiyo hoja yako inaweza kuwa ni ya msingi lakini references ulizotumia zinavuruga kabisa umuhimu wa hoja. Ulitakiwa kutuwekea "reviewed publications" hizo za wataalamu waliodhibitisha ubora wa chanjo.

Sidhani kama kuna mtu anakataa chanjo kama kweli chanjo hiyo ni salama. Kinachotia wasiwasi..ni kuwa hata waliochanjwa huko ughaibuni bado wanalazimishwa kuwa under stern measures za kujikinga na korona jambo ambalo halifanywi kwa watu wanaotumia chanjo nyingine. Tuondoleeni utata huu na mambo yatakuwa mazuri.

Natanguliza shukran.
 
Wapambe wa jiwe waliimba hizo propaganda kwa lengo la kumfurahisha ili waendelee kupata mkate wao. Hilo sasa limewakaa vichwani hata baada ya yeye kuondoka. Ni suala la muda tu, you will come back to your senses.
 
Bila shaka hujui ni kwanini nimemwekea hiyo link. Hii ni kwa sababu umedandia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…