Hivi wabongo mkuu unawajua ama unawasikia??
Subiri chanjo iletwe hapa halafu uone msongamano kwenye kuchanjwa. Hawa watu waone hivi hivi tu ni vigeu geu hatari ni watu wa kwenda na upepo unakoenda.
Mi nna imani watanzania wengi watachanjwa, hii chanjo haitakua lazima ila itakua lazima kwa namna moja ama nyingine. Inawezekana kuna huduma utazikosa bila kua na chanjo na hivyo kukulazimu uchanjwe, sidhani kama serikali itaileta tu afu iwe hiyari kirahisi namna hiyo.
Ni kama waliposema kujisajili kwa ajili ya vitambulisho vya taifa watu walikua wajajivutavuta, wakagusa panauma kwenye laini za simu, mpaka leo nida kuna watu wanazisakama hizo namba tu mambo yao yaende.