Kwanini Watoto wa Kike wa Marehemu Mafuru hata hawalii Msibani na hawana Wasiwasi tofauti na Misiba yetu Sisi Uswahilini ambapo hulia kwa Kukufuru?

Ukaribu katika malezi, mfano nyakati hizi mtoto bado mdogo, miaka yake yote analelewa shuleni, huyu lini atakuwa na uchungu/ukaribu na wazazi wake?​
 
Matusi ya nini tena ndugu?
Hio kauli yako imeniudhi sana kwasababu nimepitia kufiwa pia. Mkumbuke maghufuli mkapa alipofariki magu na ubabe wake wote alilia, siku kijazi anazikwa magu alilia pia,

Kumbuka pia mzee Zahir zoro.alikuwa ni mtu mwenye furaha maunda zoro. Alipofariki Huyu mzee hawezi tembea Tena

Kwahiyo mkuu kuwa Makini cha zaidi jifunze tu kwa sisi wengine tumevukaje hizo stage ngumu
 
Kila mtu anahaki yakuelewa atakacho ili Hali havunji Sheria au kufunja heshima ya mtu hapa tunatoa mawazo Yani hoja kwa hoja (argumentation) sioni haja ya ku_panic. Mimi ninavyo elewa watu hatufi ni mwili ndio unaharibika ila roho inaishi. Duniani tupo ku perform certain things then tunaondoka hivyo.
 
Ni Sawa nikutake radhi Ila Nina experience ya kuondokewa na mtu na mpaka sijawahi kuwa Sawa moyoni

Ni vile tu tunajikaza kiume alafu Nimejifunza kumiliki mali. Alafu wapendwa wako hawapo inatia upweke achana na wale wanakupenda sababu hauna kitu
 
Ni Sawa nikutake radhi Ila Nina experience ya kuondokewa na mtu na mpaka sijawahi kuwa Sawa moyoni

Ni vile tu tunajikaza kiume alafu Nimejifunza kumiliki mali. Alafu wapendwa wako hawapo inatia upweke achana na wale wanakupenda sababu hauna kitu
Hata Mimi nimefiwa naelewa, hebu vutapicha kama watu tusingekua tunakufa ilihali tunazaliana na bado miili inazeeka ingekuaje. Ndio maana tuliandaliwa kuchukua majukumu tokea wadogo na tunajukumu lakuanda wengine kuchukua majukumu thus it.
 
Ni huzuni, yaani watu wanaongea kuhusu pesa. Pale jamaa kaacha vaccum kama yote. Baada ya msiba kwisha ndo unajua wafiwa strong na wasio strong. Hapo wanapokuwa na watu wengi wanatiwa faraja. Subiri kuwe kimya ndo utajua kwamba baba anahitajika. Regardless kuna hela au hapana. Pesa hailingani na uhai wa Mafuru ata kidogo kwenye hiyo familia.
 
Akifa baba ambaye ndio bread winner, mke Ni mama wa nyumbani, nyumba ya kupanga vyumba vitatu, watoto lazima walie Mara mbiki.
Kwanza kuondokewa na mpendwa
Pili kuondokewa na mleta chakula na mlipa kodi ya pango.
Sasa wale nyumba ipo, mama anatanya kazi isitoshe serikali itatoa mkono wa pole si chini ya milioni Mia.
 
Na ndio sababu ya wanaume kufa mapema kuacha wajane, wanaume wa hizi familia za kawaida wamegeuzwa punda wa familia, yani mtu ni kama anasindikiza wengine duniani.

Kudadeki kesho ni ijumaa lazima nitoke out nikakemee pepo la umaskini.
Ni kweli mkuu, jamii zetu zimetengenezwa namna hiyo kuwa mwanaume atapigana na kuteseka kwa ajili ya watu wengine..

Ukipata nafasi ya kujispoil mkuu, fanya hivyo maana dunia haina huruma kwa mwanaume asiye na kitu
 
Kuna Mkuu hapo juu Kasema labda kwa sababu ya bond,true familia nyingi zakiswaz zinabond na watoto utakuta watoto toka wanakua wapo home shule home anatoka home akijaaliwa kwenda chuo/kazi tofaut na get kali Toka nursery wapo boarding school wazaz wapo busy nyumban analelewa na dada wa kazi hiyo bond itatoka wapi
 
Tujitahidi san kujenga bond na Madogo popote pale tuwapo na Chance mimi kwenye Holiday za wanangu huwa najitahidi kadri niwezavyo Nipate muda wa kukaa nao na Incase nikawa na Jambo sensitive huwa nasafiri nao walau Kujenga Bond mana unakaa Miezi ata minne hujawaona madogo ni hatari
 
Kulia haimaniishi MTU kaumia au kaguswa na msiba .

Kwa watoto ambao wapo well trained wanakuwa wanafunzwa how to handle the situation .

Maumivu huwa wanakuwa nayo Ila kulia Kama wafanyavyo waswahili ile inakuwa haipendezi we need to be strong.
 
Unajiliwaza tu
 
Kulia haimaniishi MTU kaumia au kaguswa na msiba .

Kwa watoto ambao wapo well trained wanakuwa wanafunzwa how to handle the situation .

Maumivu huwa wanakuwa nayo Ila kulia Kama wafanyavyo waswahili ile inakuwa haipendezi we need to be strong.
Huwezi ku train hisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…