Kwanini watoto wa Mzee Mchonga hawana nyadhifa kubwa Nchini?

Hali itakuwa hivo hivo hata kwa watoto wa Magufuli. Save this comment for future use.
 

Watoto wa Karume na Mwinyi walibebwa na system wakati watoto wa Nyerere hawajawahi kubebwa popote. Huyu Mwinyi alitoka shule tu na kupewa unaibu waziri baada ya baba yake kuondoka madarakani, na tangu hapo hajawahi kufanya kazi nyingine yoyote zaidi ya kuwa anateuliwa uwaziri miaka yote hadi sasa anakuwa rais. Alisomea udaktari lakini hajawahi kuandika prescription yoyte hata ya kutibu mafua.
 
Kwani Tanzania ni nchi ya kifalme?

Maana nchi ya kifalme ndiyo lazima mwana mfalme aje kuwa mfalme.

Hujawahi kufikiri kwamba kinachotakiwa kuhojiwa si watoto wa Nyerere kukosa urais, bali watoto wa Mwinyi na Karume kupata urais?
 
Ni demokrasia inafanya kazi tu mkuu

Niliwahi kuwa kwenye mahusiano na binti wa kizanaki, akadai kuwa Makongoro amewahi kumtaka kimapenzi nikahisi ni uongo, ila nimeanza kumuamini baada kuona comment yako. Watoto wa wakubwa huwa wanakuwa na tabia ambazo sio nzuri.
 
Una uhakika na unachoandika? Mhe. Hussein Mwinyi amefanya kazi Kairuki Memorial Hospital kabla hajaingia serikalini. Taarifa zingine tafuta mwenyewe.
 
Watoto wa mwl ni mazuzu
 
Una uhakika na unachoandika? Mhe. Hussein Mwinyi amefanya kazi Kairuki Memorial Hospital kabla hajaingia serikalini. Taarifa zingine tafuta mwenyewe.
Alifanya kwa miezi mingapi? Kwa sababu aliteuliwa waziri mdogo mwaka 1995- ambapo alikuwa bado angali anasoma uzamili kwani alihitimu uzamili mwaka 1997. Baada ya miaka mitano ya uwazili mdogo ndipo akaenda kugombea Mkuranga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…