Wanabodi, Salaam!
Kwa wabobezi wa saikolojia na sosholojia naombeni mniambie kwa nini tangu tupate Uhuru kisha kuungana Zanzibar na Tanganyika familia za Mwinyi na Karume tushapata marais mara mbili (Ally Hassan Mwinyi, Hussein Ally Hassan Mwinyi na Abeid Karume na mwanaye Aman Abeid Karume
Kwa familia ya Mwl Nyerere tangu ang'atuke nadhani mwaka 1985 hadi leo hakuna mtoto hata mmoja aliyeweza hata kufurukuta na kuingia kwenye tatu bora ya wagombea urais nchini - hata Madaraka Nyerere juzi tu kura za maoni kwa nafasi ya ubunge zilimtupa mbali kisha kamati kuu ya CCM haikurudisha jina lake.
Sasa, hii hali ya watoto wa mwasisi wa taifa hili kutopenya kwenye vinyanganyiro vya nafasi za uongozi zinatokana na nini?