Kwanini watoto wengi wanaua mama zao?

Kwanini watoto wengi wanaua mama zao?

Notorious thug

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2021
Posts
2,817
Reaction score
10,667
Kumekua na ungezeko la watoto kuua mama zao wa kuwazaa hivi karibuni jambo linaloibua huzuni na hofu kwenye jamiii.

Asilimia kubwa imekuwa wahanga ni kina mama zaidi ya kina baba nimewaza jambo hili kwa kina ndani ya siku mbili hizi kuna mambo nayohisi yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa zaidi ya tamaa ya mali na kupenda starehe.

1-Maneno ya kina Mama kwa watoto.Wanawake wengi ni watu wa maneno wanapenda kuongea sana wanapokasirika na kutoa maneno mabaya kwa watoto wao kama kusema ndiyo maana huolewi,mbona mtu fulani kapata kazi wewe huna au mzazi wa kike anamwambia mtoto wake hapa nyumbani sio kwako hamna utakachokipata hapa hata tukifa/nikifa unategemea apo mtoto unamweka kwenye hali gani.

2-Kumnyima mtoto uhuru.Kina mama wengi wanapenda kuona watoto wao wanashinda nyumbani mtoto haruhusiwi kujichanganya na wengine.Mtoto saa kumi na mbili awe nyumbani mtoto anakosa furaha hamna kitu mtoto anapoanza kukua anakasirika kama kuona ananyimwa haki ya kua na watoto wengine au vijana wenzake tunajua dunia imeharibika ila sio sababu ya kuwanyima vijana kua na wenzake watoto wanachoka kukaa nyumbani na kuwachoka pia wazazi kutokana na masharti yao mengi yakiwa ni kuwanyima uhuru wao.

3-Wazazi kuwa wabinafsi.Kuna kina mama ukimwona anavyovaa na gari analoendesha na ukimwangalia na kijana wake tofauti iliyopo ni mbingu na ardhi hii inasababisha mtoto kuhisi mama hampendi na anajipenda yeye tu hiii huamsha hasira kali sana kwa mtoto na kuleta roho ya kisasi.

4-Chuki.Watoto wengi hua muda mwingi wanashinda na Mama zao kutokana na maisha ya kila siku kuna mambo hua yanatokea kati ya mama na mwanae mama anakua anamtishia mwanae akifanya kosa labda baba akija leo nitamwambia akuchape au leo hutakula hapa nyumbani hiii huleta chuki sana kwa watoto na kumchukia sana mzazi wake.

5-Msukumo kutoka kwa marafiki.Vijana hupenda kua na marafiki wa rika lao kuanzia mashuleni hadi mtaani hapa hukutana na mambo mengi na kulinganisha maisha yake na wengine mbona huyu mama yake anampa gari,mbona huyu anaruhusiwa kwenda kumbi za starehe hiii huleta chuki na ushauri kutoka kwa marafiki kwamba mama yako anakunyima gari, anakunyima kwenda club.

N:b haya ndio mambo niliyoyawaza mimi karibuni wengine kwa mengi au ushauri kuhusu mambo haya yanayoendelea kwenye jamiii hakika yanaleta huzuni kubwa
 
Acheni kupeleka watoto wenu boarding wakiwa wadogo..eti kitoto kina 2 yrs kinakaa shule..mpk kinafika chuo hakina hata bond wala mapenzi na mzaz wake. KAENI NAO WALEENI..KTK MAADILI sio mnawaachia walelewe na janii eti kisa mko busy, ona sasa wanawaua hawana bt uchungu
 
-Tamaaa
-Migogoro ya kifamilia .
N.K
Lakini unge edit kidogo Uzi wako ,weka paragraph kabla kabla hawajakuja wapiga spana
 
wazazi wamekua wabinafsi sana unakuta anajenga nyumba 7 na maduka kibao ila kukupa mtaji anaona nomaaa kila siku kiswahili hlf anapiga cmu kwa watu wampe mwananae kazi.

wakati roho yake ngumu kutoa mtaji sasa nani akupe kama tu weww huwezi kutoa cha kutosha mwisho wake ndo huo kwa watoto wasio na uvumilivu.
 
Na wewe uwe unauliza swali vizuri. Umewahi sikia mtoto kutoka Mpitimbi au Matimila Songea ameua mzazi wake?

Uliza hivi kwa nini watoto wa maeneo maeneo wanaua wazazi wao?
 
Hapa utakuwa unaongelea watoto wa kishua na wenye pesa ambao ni wachache Tanzania kiuhalisia.

Nimeona hapo sijui gari, club na uhuru haya mambo ni mageni kwangu na kwa wengi waliokulia mazingira na uchumi wa kipato cha kati.

Watoto waliolelewa kwenye mazingira ya uchumi wa kawaida au wa kati kamwe hawawezi kuwa na uwezo au fikra za kuua mzazi.
Sababu tangu mtoto anakuwa anamuona mama ndio msaidizi na mtetezi wa kila kitu kwenye shida na nafuu na kama baba ni mjinga ndio kabisa.

Mama anakuwa rafiki na mshauri pia kunakuwa na mipaka vilevile, kutokana na ukaribu na mwanae mtoto anakuwa motivated kupambana kwa ajili ya mama no matter what na heshima kwa mama isiyoteteleka wala kuvunjika.

Hakuna kitu ninachokiheshimu duniani kama mzazi wa kike.

Hayo yote ni sababu ya malezi tu.

Lakini hawa jamaa wa kishua na pesa wazazi wao wanaishi kama wazungu.

Hakuna mipaka kati ya mzazi na mtoto, hii inapelekea kukosekana heshima.

Hakuna ukaribu kati ya mzazi na mtoto, hii inapelekea mtoto kutokujali kuhusu mzazi.

Na kutokana na malezi yao na tabia za wazazi, watoto wanakuwa hawajui wala hawaoni umuhimu wa mama kwenye maisha yao.
Anamuona kama mshikaji wake tu, matokeo ndio hayo.

Na hata hivyo hakuna sababu yoyote ya kuhalalisha mauaji ya mzazi hata kama makosa ni ya wote au upanda mmoja, lakini hii iwe fundisho kwa wazazi juu ya malezi ya watoto.

Mimi nipo tayari kufa kwa ajili ya mzazi, wengine wanawapiga mapanga.

Yote ni malezi tu.
 
Acheni kupeleka watoto wenu boarding wakiwa wadogo..eti kitoto kina 2 yrs kinakaa shule..mpk kinafika chuo hakina hata bond wala mapenzi na mzaz wake....KAENI NAO WALEENI..KTK MAADILI sio mnawaachia walelewe na janii eti kisa mko busy....ona sasa..wanawaua hawana bt uchungu
Kwa mbali naona kama kuna uhalisia hapa,mitoto mingi siku hizi inajuwa shule tu ikifikia umri fulani hivi wa kutaka kuwa huru zaidi inawaza kwenda kula bata kwenye kumbi kubwa za starehe na wanakuwa hawana uchungu na wazazi wao hata hali zao za maisha ndiyo maana wanafanya maamzi magumu na mabaya kama haya
 
Kwa mbali naona kama kuna uhalisia hapa,mitoto mingi siku hizi inajuwa shule tu ikifikia umri fulani hivi wa kutaka kuwa huru zaidi inawaza kwenda kula bata kwenye kumbi kubwa za starehe na wanakuwa hawana uchungu na wazazi wao hata hali zao za maisha ndiyo maana wanafanya maamzi magumu na mabaya kama haya
Kabsaaa kiongoz
 
Mbona haya Matukio ni Kanda ya KASKAZINI TU!!! Halafu Wanawake wote wanaouawa hawana waume zao????????[emoji23][emoji23][emoji23][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

La Mirembe hujasikia?
 
Umetoa sababu za kijinga Sanaa

Hakuna sababu yoyote ya KU justify mauaji..kuua tu kosa iwe ulikerekwa au iwe vipi mauaji ya kukusudia ni mbaya Sana tena hasa Hawa wanao ua wazazi wao kisa Mali (Kama inavyodaiwa)
 
Back
Top Bottom