Mkuu, watu wa namna hii USA wa mamilioni kwa mamilioni tena huku wamekuja wenyewe tu sio kwa mjomba au ndugu kama huyo muhindi wako. Mfano, Shahid Khan mzaliwa wa Pakistan, Billionaire na owner wa Jacksonville Jaguar na PL tema Fulham.
US mtu yeyote anaweza kuwa yeyote
Hili ni panga linalokata kote kote yes mtu yoyote anaweza kuwa yoyote including
-Homeless wasio na nyumba wanaolala nje na kwenye madaraja
-masikini wasio na uwezo hata wa kujitibu ama kupata elimu nzuri
-wagonjwa wanaokuwa Exploited na System (1/3 ya kila mtu anaefariki Usa ni sababu ya lishe mbovu)
-wanajeshi wanaojiua kila baada ya dakika kadhaa etc.
Mtu anaetoka Ulaya anaweza kutembea kifua mble vs Middle East nchi za Ghuba ila Usa hapana, kila bilionea mmoja unayeoneshwa kuna masikini kibao ambao amewakanyaga na kuwadhulumu haki zao akisaidiwa kisheria.
Hizo Nchi kama Saudi, Dubai (Uae), Qatar na nchi nyingine za Asia kama Singapore, Brunei, Malyasia na wengineo wamefanikiwa kiasi kikubwa kutokomeza umasikini, hakuna mabilionea wengi lakini pia hakuna masikini.
Saudia na Nchi nyengine za Ghuba kama ilivyo Ulaya ukiwa huna kazi umetoka Chuo unalipwa Sar 2000 kila mwezi kama Pocket money hii ni kama 1,200,000 ya Tanzania.
Mimi Binafsi nina ndugu wengi tu walizamia Usa, ila hakuna hata mmoja aliebakia baada ya kupata Uraia wa Usa wengine wamekwenda Nchi za Kiarabu na wengine wapo Canada wanatafuta maisha bora,
, case in point Obama. Huko Dubai au China unaweza kuta mtu ambaye ana damu ya nje kwenye uongozi?
Hukuti, same kwa Usa, huwezi kuta mjamaa ama mtu mwenye philosophy Tofauti na wanayoiamini akawa Raisi, Kila nchi ina namna yake ya kutafuta kiongozi, na sidhani kama mtu anazamia Usa akawe kiongozi.
Si Obama tu, watu wengi sana wapo in the political sphere ambao wamezaliwa nje ya US kabisa. Omar Ilhan kazaliwa Somalia ila sasa ni congresswoman wa Minnesota. UK wana PM mhindi. Hata bongo hatuwezi mpa mgeni uongozi wa juu.
Pia jambo jengine ufahamu viongozi wengi ni puppets hasa Usa, kuna kuwa na watu nyuma wanaorun show, nitakupa mfano hapo Usa silaha zinanunuliwa kama Karanga, mwanafunzi akifikisha miaka 18 kashavuta ngada yake anaenda dukani anaunua Bunduki anaenda shule anamiminia risasi wanafunzi wenzake na walimu.
Ingia hii website wana record events
Gun Violence Archive (GVA) is a not for profit corporation formed in 2013 to provide free online public access to accurate information about gun-related violence in the United States. GVA will collect and check for accuracy, comprehensive information about gun-related violence in the U.S. and...
www.gunviolencearchive.org
Kuanzia tarehe 1 mpaka 3 siku 3 tu hizo kuna Mass shooting 8, yani karibia kila siku mtu ananunua bunduki na kumiminia wenzake risasi,
Kwa akili tu ya kawaida kwanini wanaruhusu watu kuuana hivyo? Ukifuatilia zaidi Viwanda vya silaha vina nguvu kushinda hao maraisi na wabunge, Vinauza silaha hadi kwa maadui wa marekani na maisha yanaendelea kama kawaida. Hio ni Nchi inayoendeshwa na Mabilionea ndio maana hadi kesho Kodi wengi hawalipi.
Huwezi fananisha usawa wa fursa kwa kila mtu in the western countries na nchi zingine that's a fact nikianza kuorodhesha hapa sitamaliza. If given the chance watu wote wangekuwa in the western countries ni vile visa za huko ni ngumu compared to sehemu kama middle east ila kwa fursa ni mbingu na ardhi.
Ingekua Fursa zote zipo huko Leo hii wasingekimbilia China Kupeleka viwanda, wasingekuja Africa Kufuata Rasilimali, wasingeenda Middle East kufuata Mafuta etc.
Kama unakaa unasubiria TV na Internet ikusaidie ubongo wako kufikiri of course utakuwa na mawazo kama haya, ila kama unafikiria Nje ya Box utajua Fursa na Opportunity zipo wapi duniani, Hasa kwa Wanaume ma Fighter.