Kwanini watu wa kamera wanaruhusiwa kuhujumu ziara ya Rais Samia?

Mods kuna Uzi kama huu humu jukwaani,kwa nini msiunganishe?

Mwisho wapigapicha wake ndio wanapotosha,kama aliwachukua wale wale wa Sukuma gang anategemea nini?

Badili safu hiyo.
 
Hawana sababu ya kuhariri hali halisi.
 
Tatizo la CCM ni kutokuwepo umati na ndiyo sababu hulazimika kubeba washangiliaji toka mji mwingine.
 
Mama amesahau strategy za
Jiwe za kubeba wanafunzi,
malori na ma trecta ya
wakulima kwenye mikutano.
Yaani mkutano wa Mbeya mjini
anaanda malori kutoka
Chunya, mbalizi, njombe🤣🤣
Ina maana gani hiyo ni kwamba watu wanataka kwenda ila shida usafiri ndio maana wanawapelekea magari au watu wa hilo eneo hawatoshi ndio uenda kuchukua watu wa sehemu zengine huko ili kuja kujaza?
 
Kwani ccm ishawaki kuwa na
hiyo Political Influence??
Nakwambia hivi bila vyombo
vya dola ccm ni sawa na
Chauma tu.
Ingekuwa hivyo mkuu upinzani usingekuwa inasumbuka kutafuta wagombea wa urais wenye ushawishi kiasi cha hadi kuchukua watu waliyotoka huko ccm, kwa maana kusingehitajika mtu mwenye ushawishi ili kushindna na ccm ambayo ni sawa na chauma.

Ni mtazamo wangu tu.
 
aache kujitutumua, kama anaendeleza kazi ana wasiwasi gani?
 
Ni suala tu la kufanya kazi ionekane, watu sasa hivi wanabadilika hawataki maneno mengi, huwezi kushinda muda wote unamwangalia kiongozi ilihali mtu anatakiwa kutafuta mkate, kiongozi anayefanya kazi nzuri hata njaa au kukosa pesa kwa muda huo unaweza ukaridhika tu ili mradi umsikilize.
 
I always say she is incompetent.
Mifumo ya nchi ikiwa perfect haijalish tatizo ni kusafiri kwenye mifumo mibovu.
Kuna watu wameathiriwa na kuvuli cha mtangullizi wake na hao ndio hawaishi kumlaumu.
Kiukweli mama ni binadamu na rais wa nchi. NI RAIS
 
Inaonesha Jiwe alikuwa na watu wengi sana.
Jiwe alipanga kikosi kweli kweli,hata Msigwa ni Jiwe alimuweka na Wana undugu wa kuoleana..

Ikulu na kila sehemu kulikuwa timu Jiwe na bado wako wengi Sana..

Kuwa na watu wengi ni sahihi kwa sababu alikaa miaka 5 so hata wewe lazima uweke timu yako..

SSH hawezi pangua wote at par ila atawang'oa taratibu.
 
11 Agosti 2022
Lupembe, Njombe
Tanzania 🇹🇿

Mh. Rais Samia Hassan awapiga kijembe waandishi wa habari

Watu ni wengi lakini mitandao inasema vingine, hivyo waandishi wa habari wapewa changamoto kuonesha ukweli ya kinachojiri katika safari yake ndefu ya kikazi kukagua maendeleo nyanda za juu kusini mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa
Source : mwanahalisi TV
 
Hatogombea Hilo liko wazi, tatzo Hasa ni muda uliobaki Hadi kufika 2025 pareeeefu sana, ni safari inayochosha akili na mwili.

Ameanza kukosa USINGIZI kama uncle.
Ameanza kukosa usingizi kama Uncle!!?

Umejuaje!!?

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…