Kwanini watu walioajiriwa serikalini wengi wana uwezo mdogo wa akili?

Kwanini watu walioajiriwa serikalini wengi wana uwezo mdogo wa akili?

Sio hawana akili

Hawa watu Wana akili sana tu, maana hata wamiliki wa consultants firms nyingi ni hao hao watu wa Serikali

Tatizo kubwa nilionalo Kwa watu wengi wa Serikali ni kufanya kazi Kwa mazoea, kukosa vitendea kazi na mazingira duni ya kufanyia kazi.

Nina jamaa zangu wanafanya kazi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Lakini hawana vitendea kazi, wapo na wanalipwa Mishahara Kila mwisho wa Mwezi na Serikali hiyo hiyo
 
Serikali Ina useless people wengi Sana .


Hakuna kitu wanaweza hawa watu wa serikalini .

Huduma zao 90% ni ovyo Sana .
Akili zimefungwa kwenye ka mshahara ka mwezi na magendo, hawa huwa hawawazi nje ya boc pia waajiriwa wengi wapo vijijini huko directly akili huwa zinakufa kabisa na kuwa na akili za kipori kama ngedere
 
Tatizo sio uwezo mdogo bali kukatishwa tamaa na mambo yanayoendelea maofisini hadi serikalini. Na mishahara kiduuunchuuu
 
Serikali Ina useless people wengi Sana .


Hakuna kitu wanaweza hawa watu wa serikalini .

Huduma zao 90% ni ovyo Sana .
Inatakiwa watu kama nyie wenye akili na uwezo wa kutoa huduma vizuri muombe hizo kazi ili mtuonyeshe mfano na kuisaidia serikali na watanzania kwa ujumla. La sivyo miaka nenda rudi tutabaki na malalamiko.
N.B Malalamiko hayasaidii chochote
 
Tatizo sio uwezo mdogo bali kukatishwa tamaa na mambo yanayoendelea maofisini hadi serikalini. Na mishahara kiduuunchuuu
Mshahara kiduchu ni kisingizio tu. Huko private ni wangapi wanalipwa vzr?
 
Wengi na pia juhudi zinawaletea tija. Serikalini unatakiwa kuwa robot na ndio mzee za kutosha,uchawa wa kumwaga. Hutakiwi kutumia akili zako kwa asilimia 100
Mshahara kiduchu ni kisingizio tu. Huko private ni wangapi wanalipwa vzr?
 
Iko hivi

1.Wanaopewa motisha sio hao walio bora kazini, motisha hutolewa kwa mchongo, ukiwa na mahusiano mazuri yakujipendekeza kwa wakuu ndivyo utakavyokula mema ya nchi bila kujali ufanisi wdko kazini.

2.Ukifata taratibu na miongozo inavyotakiwa kazini ndivyo unapotengeneza maadui wengi zaidi, watumishi wengi hawampendi mtu anayefata taratibu sana.

3. Watumishi wengi wa Serikali Hasa Tamisemi hawalipwi stahiki zao kwa wakati mfano madai ya uhamisho, ajira mpya, malimbikizo na motisha nyinginezo, wengi wanategemewa na kundi kubwa nyuma yao hivyo hufanya kazi kwa msukumo huku kila mtu akiwa makini kwa nafasi yake kazini kuondoka na chochote ili kurahisisha ugumu wa maisha,

4. Watumishi wengi hawawezi kusimamia taaluma zao, huogopa sana viongozi wa kisiasa wasije kutia mchanga vitumbua vyao vya ajira, hata wale wenye vyeo hujikuta wanawakandamiza walio chini yao ili kuwaridhisha wanasiasa wachache wasio na shule na wapumbavu.

5. Watumishi wengi hawana vitendea kazi kama walivyovitegemea wakati wanamaliza taaluma zao, huwa na mategemeo makubwa kinyume na wanachokutana nacho kwenye maeneo yao ya kazi.


Kwa sababu hizo lazima wataonekana wajinga wajinga na wasiojielewa, hata wewe mtoa mada utakapokutana na hayo lazima morali yako ya kazi itakata kabisa.
 
Back
Top Bottom