Iko hivi
1.Wanaopewa motisha sio hao walio bora kazini, motisha hutolewa kwa mchongo, ukiwa na mahusiano mazuri yakujipendekeza kwa wakuu ndivyo utakavyokula mema ya nchi bila kujali ufanisi wdko kazini.
2.Ukifata taratibu na miongozo inavyotakiwa kazini ndivyo unapotengeneza maadui wengi zaidi, watumishi wengi hawampendi mtu anayefata taratibu sana.
3. Watumishi wengi wa Serikali Hasa Tamisemi hawalipwi stahiki zao kwa wakati mfano madai ya uhamisho, ajira mpya, malimbikizo na motisha nyinginezo, wengi wanategemewa na kundi kubwa nyuma yao hivyo hufanya kazi kwa msukumo huku kila mtu akiwa makini kwa nafasi yake kazini kuondoka na chochote ili kurahisisha ugumu wa maisha,
4. Watumishi wengi hawawezi kusimamia taaluma zao, huogopa sana viongozi wa kisiasa wasije kutia mchanga vitumbua vyao vya ajira, hata wale wenye vyeo hujikuta wanawakandamiza walio chini yao ili kuwaridhisha wanasiasa wachache wasio na shule na wapumbavu.
5. Watumishi wengi hawana vitendea kazi kama walivyovitegemea wakati wanamaliza taaluma zao, huwa na mategemeo makubwa kinyume na wanachokutana nacho kwenye maeneo yao ya kazi.
Kwa sababu hizo lazima wataonekana wajinga wajinga na wasiojielewa, hata wewe mtoa mada utakapokutana na hayo lazima morali yako ya kazi itakata kabisa.