Kwanini watu wana chuki na Uislam na Waislam kwa mabaya ya Waarabu?

Kwanini watu wana chuki na Uislam na Waislam kwa mabaya ya Waarabu?

Status
Not open for further replies.
Chuki au ubaguzi dhidi ya Waislamu mara nyingine unaweza kutokana na kutokuelewa na miseducation, pamoja na sababu nyingine kama vile vyombo vya habari, matukio ya kihistoria, na hali ya kisiasa. Ni muhimu kutambua kwamba kuenea kwa maoni hasi au chuki dhidi ya jamii fulani haikubaliki na inakwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu na utofauti wa tamaduni na dini.

Hapa kuna sababu kadhaa zinazoweza kuchangia chuki dhidi ya Waislamu:

1. Ubaguzi wa Kidini:
- Baadhi ya watu wanaweza kuwa na upendeleo au hata chuki dhidi ya dini tofauti, na hivyo wanaweza kuwa na maoni hasi kuhusu Waislamu kwa msingi wa dini yao.

2. Ubaguzi wa Kikabila na Kitamaduni:
- Waislamu wengi wanatoka katika jamii tofauti na za kitamaduni, ikiwa ni pamoja na Waarabu. Ubaguzi wa kikabila au kitamaduni unaweza kuchangia maoni hasi.

3. Ugaidi na Vyombo vya Habari:
- Matukio ya kigaidi yanayofanywa na makundi fulani yanaweza kutoa taswira hasi ya Uislamu kwa jumla. Vyombo vya habari mara nyingine vinaweza kuchochea hofu na chuki kwa kuripoti matukio haya bila kuzingatia muktadha kamili.

4. Ukosefu wa Maarifa:
- Kutokuelewa kuhusu imani za Kiislamu na tamaduni za Waislamu kunaweza kusababisha maoni potofu au ya kupotoshwa.

5. Mzungumzaji wa Kujitenga (Othering):
- Mara nyingine, watu wanaweza kuhisi kutengwa au kuwaona Waislamu kama "wengine," ambao ni tofauti nao. Hali hii inaweza kuchangia kutoelewa na kuleta chuki.

Ni muhimu kukuza elimu, kuelimisha, na kufanya mazungumzo yenye heshima kati ya jamii na dini tofauti ili kupunguza chuki na kusaidia watu kuelewa tofauti zilizopo na kuheshimu utofauti wa tamaduni na dini. Kuelimisha jamii juu ya ukweli wa dini mbalimbali na kukuza mazungumzo ya kuheshimiana ni njia ya kujenga jamii inayokubali na kuheshimu utofauti.
Hii haipo kwa bahati mbaya

vyombo vya magharib vimekuwa msitari wa mbele kuzungumzia chuki hii bila kuweka mipaka wala kujali athari yke nn

na kuonekana uisilam km ni tatizo kwa ulimwengu na jamii za kiarabu lkn ajabu kadiri ya chuki zidi ya uislam inavo enea na ndivo uisilam unavo kua

Ajabu hata hp nchi yt kuna watu wanaamini kumpeleka mtoto madrasa ni km mtoto anapoteza muda kwani anaenda kujifunza lugha ya kiarabu tu hatokuwa la manufaa lolot hivyo sio jambo sahih kwk .
Watu wengi wanaaminishwa(kasumba) jamii za kiisilam ndio jamii maskin kwani hawa wek kipao mbele elimu ya shule, kwngu mm Hilo siamini mfn ukiangalia nchi za masharik ya kati baadhi ya jamii zao zinawapeleka wtoto wadogo kusoma qur an madrasa na wanasoma shule za kawaida vizur tu na maendeleo ya jamii hizo ya kichumi yanakua vzr

lkn hili kwa kwetu limekuwa km ni fimbo inotumika na badhi ya wtu kuwerejeha nyuma jamii za kiislam kusema madrasa ni kuzoretesha maendeleo yao kwa jamii hizo jambo ambalo sio kweli ukiangalia kiundani ndio jamii zilokuwa bunifu kutotgemea kuajiriwa kulingana na elimu ya shule na zinachangia sekta binafsi za kiuchumi kwa asilimia kubwa lkn na hili linatokana mfumo mbovu wa elim .
kosa kubwa waislam linowasumbua vyombo vya habari vya kimataifa vimechukua nafasi kubwa kuwachafua ndio zao ya chuki unazo ziona ulimwengu mzima zidi ya waislam lkn hili ni swala la muda tu saiv wtu wameshaanza kuelewa ukweli na ndio mana unaona mabadiliko makubwa ulaya zidi ya uislam na ulimwengu kwa jumla
 
Sio lazima kitoke kitabibu, tumeona kuanzia Al Qaeda,Isis ,boko haram na wengineo wakitumia Allahu Akbar baada ya kufanya matendo yao ya kigaidi. Jambo hilo linafanya watu waamini kwamba uislam na ugaidi ni pande mbili za kwenye sarafu 1.
Ujinga hauna kawaida yakuonekana hovyo tafadhali usiudhihirishe
 
Hio nchi ya kiislam iliyomuua mtu kwa kurtadi ni ipi?

Utaweza kusema nchi fulani ni ya kiislam if iko full gear kwenye matumiz ya sheria za kiislam unless ni kutafuta ujiko usio na msingi.Saudia sio nchi ya kiislam bali ni nchi ya waislam ndio maana kuna ruhusa ya pombe na mambo mengine ambayo uislam umeyakataza.


Katiba ya saudi arabia ni quran na sunnah.

Uislamu umeanzia saudi arabia na hata nguzo ya tano ya uislamu inafanyika kwenye ardhi ya saudi arabia

Makao makuu ya uislamu ni saudi arabia

Nchi ya saudi arabia inaua watu kwa kuritadi
 
Katiba ya saudi arabia ni quran na sunnah.

Uislamu umeanzia saudi arabia na hata nguzo ya tano ya uislamu inafanyika kwenye ardhi ya saudi arabia

Makao makuu ya uislamu ni saudi arabia

Nchi ya saudi arabia inaua watu kwa kuritadi
Lete uthibitisho acha bla bla.Kama inafata qur an na sunnah njoo na uthibitisho qur an na sunnah zimeruhusu pombe
 
Siyo kweli. Haiwezekani mtu mzima na akili timamu akaoa katoto kadogo hivyo. Atakafanya nini sasa? Hii ni kumchafua mtume. Mtaenda motoni nyie. Mtoto wa miaka 6? Daaah.... Huo si ushetani, ubakaji na unajisi.
Hata wenyewe hawabishi, si unamuona mwamba hapo juu anatetea kabisa akiuliza kwani "hawawezi kuolewa?"
 
Kulikua na ulazima gani wa Mtume kua Mwaraba na kutumia lugha ya kiarabu kuforce Uislam? Na kwaninin mkacopy dini za watu? matunguli ya Babu zenu mnamwachia nani?
 
Yani jamii zote duniani ikiwemo watu weusi kuna wenye matatizo ya akili, kuna wwasio na dini na kuna wahuni.

Lakini jambo akifanya Muarabu: basi huyo moja kwa moja ni muislam, hakuna muarabu asie na dini, hakuna muarabu mhuni au katili au mjinga, chochote anachofanya muarabu basi anafanya kuiwakilisha dini ya kiislam, kwanini?

Ni ujinga kutafsiri uislam kutoka kwa waarabu (generalized), hata waliomganyia madhila makubwa Mtume walikua ni waarabu hao hao tena wengine wa kabila lake alipozaliwa.

Uhusiano wa waarabu na Uislam ni mambo mawili tu:

1. Mtume alikua muarabu
2. Quran imeandikwa kwa kiarabu, tofauti na hapo, muarabu ni muarabu na muislam ni muislam

Acheni chuki za kijinga
Chuki ni uchafu wa moyo
 
Kulikua na ulazima gani wa Mtume kua Mwaraba na kutumia lugha ya kiarabu kuforce Uislam? Na kwaninin mkacopy dini za watu? matunguli ya Babu zenu mnamwachia nani?
Wewe unafikiri hao wakina Musa waliongea kiswahili ??waliongea kiebrania , watu wote walitangaza imani kwa lugha zao za asili, ila vihere here ndio wakatafisiri ili wajue kuna nini
 
Wewe unafikiri hao wakina Musa waliongea kiswahili ??waliongea kiebrania , watu wote walitangaza imani kwa lugha zao za asili, ila vihere here ndio wakatafisiri ili wajue kuna nini
Kwahiyo unataka kusemaje? Chuki iendelee dhidi ya Waislam na kiarabu chao au waabudu kiswahili na waache kujinasbisha na waarabu?
 
Maneno yako wazi TUMEITEREMSHA KWA LUGHA YENU KIARABU ila unabadilisha kwa uongo uongo. Sikushangai maana Quran imewaruhusu kusema uongo. Kudanganya ili kuulinda uislamu

Uongo huo Mnaita Taqiyya
Qur an imeteremshwa kwa kiarabu sas nataka sehem kweny hio aya unioneshe neno la kiarabu lenye maana LUGHA YENU.
 
Kwahiyo unataka kusemaje? Chuki iendelee dhidi ya Waislam na kiarabu chao au waabudu kiswahili na waache kujinasbisha na waarabu?
Quran iliandikwa kiarabu, na Biblia iliandikwa kiebrania, ni kichaa pekee ndio anaweza kufikiri vitabu viliandikwa kiingereza au kiswahili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom