The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Watu wanahoji kwa nini Rais Magufuli anapeleka maendeleo kwao, Chato na Geita kwa ujumla, kama vile watu wa Chato au Geita hawastahili kupata maendeleo, sasa asipeleke Chato apeleke wapi?
Unapokuja kwenye rasilimali za nchi hii haziko kwenye mgawanyo sawa, kuna mahala pengine utafikiri sio Tanzania hii na mahala pengine utafikiri ni gerezani.
Mfano, Serengeti ndio mbuga maarufu kuliko zote Tanzania, kwa takwimu za Tanapa, zaidi ya 80% ya watalii na mapato ya utalii nchini yanatokana na mbuga ya Serengeti ila nenda Serengeti kwenyewe uone watu wake wakoje, wanaoneemeka ni wengine kabisa. Hata chuo tu cha utalii au chuo cha wanyamapori hakikujengwa Serengeti, vyuo vikajengwa mahala ambapo hata panya hayupo. Hata Hotel moja ya kueleweka haipo Mugumu, na hili sio bahati mbaya, lilifanyika makusudi kabisa.
Ukienda Kanda ya Ziwa kwa ujumla hakuna chuo kikuu chochote cha serikali ukiachana na Chuo Kikuu Huria, sehemu nyingine vyuo vya serikali vimejaa eneo moja kama siafu. Hili pia halikuwa linafanyika kwa bahati mbaya, ni makusudi kabisa. Mwaka huu NBS walitoa takwimu za mikoa masikini zaidi, miwili ilitoka Kanda ya Ziwa, Geita na Kagera, unajiuliza kanda tajiri kwa rasilimali kiasi kile inakuaje masikini, jibu ni moja tu, mgawanyo usio sawa wa rasilimali za nchi.
Sasa pale Rais anapojaribu kuwakumbuka watu waliokuwa wamesahaulika kwenye keki ya taifa hili, maneno yanakuwa maneno, kwamba awaache wale ambao hawakuwa na kitu awakumbuke wale walionavyo vimejaa, haiwezekani.
Watu mnapata wapi ujasiri kuhoji watu wa Chato na Geita kukumbukwa kwenye keki ya taifa?