Kwanini watu wanahoji Rais Magufuli kupeleka maendeleo Chato na Geita kwa ujumla?

Kwanini watu wanahoji Rais Magufuli kupeleka maendeleo Chato na Geita kwa ujumla?

Kqa hiyo unatuambia kuwa magufuli naye ameamua kupendelea kwao ili kuuenzi utamaduni huo? Tutamtofautishaje na wengine walioulea utamaduni huo?au nae ni wale wale?
 
Marais waliopita wametokea Mara, Pwani, Mtwara, Pwani ...Kuna mkoa hata mmoja hapo uliopo top 5 ya wenye ahueni?
 
Kilimanjaro inayosakamwa Sana na watu wa lake zone, haijawahi hata kutoa Rais jamani. Tofauti kubwa ni akili na Elimu. Lake zone somesheni watoto wenu Sana. Jengeni shule badala ya viwanja vya ndege na madaraja. Hayo madaraja mnatujengea sisi Wapare, Wachagga, Wameru, Wambulu na Waarusha. Tutaleta mitaji huko kujenga hotel, migahawa, bar, yard za magari, Sheli halafu mtaishia kuwa watumwa wetu.
 
Lake zone somesheni watoto na kupeana tafu. Piganeni tafu. Hiyo ndio tofauti na ndio itaondoa umaskini. Madaraja hayaondoi umaskini wa watu Ila huondoa umaskini wa Serikali na kuleta fahari kwa viongozi. Mtakuja kuhamia mapori ya Rukwa, Katavi na Sikonge na kutuachia sisi wa Kanda ya kaskazini na Nyanda za Juu kusini, tukiendeleza mahotel katika hifadhi ya burigi, katika uwanja wa kimataifa wa Chato, tukivuka daraja la busisi, tukitibu watu katika hospital ya mkoa wa Geita na hospital ya rufaa ya Chato na pia kuwauzia madawa katika famasia zetu kubwa kubwa huko.
 
Hizi ni takwimu za tanapa na wizara ya utalii, sasa ningetegemea ukaja na takwimu kupinga hili, sijaziona.

..mbuga za Serengeti + " XXX " zinachangia 85% ya mapato ya utalii Tz.

.."XXX" nitaihifadhi kwa leo, kwasababu nikiitaja baadhi yenu mtafura kwa hasira.
 
Mtoa mada anasahau kwamba kinachosababisha watalii kuegemea ukanda wa kaskazini na hata wawekezaji kupenda Arusha kuliko Mara na Mwanza ni kwa sababu kuna vivutio vingine sio Serengeti tu. Kuna Ngorongoro, Tarangire, Lake Manyara, Arusha National Park, Mlima Kilimanjaro na Mkomazi. Unadhani mtalii ataenda Mwanza ili aende Serengeti tu? Wakati akifika Arusha kunakuwa na chances kibao za kufika mbuga na hifadhi zingine?
 
Mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi na Rukwa ni mikoa pekee ambayo kwa kiwango kikubwa sana imetelekezwa na awamu zote.

Ukifika mikoa hiyo unafiikiri wanaoishi huko siyo watanzania, viongozi hufika wakati wa kampeni tu.
Katika hiyo list yako, Tabora iondoe
 
Mkuu ulitaka mkoa wa Mara usiwepo? Au uwe mwanza? Unataka serengeti iwe Arusha au Kenya?

Siyo swala la mimi kutaka au kutotaka kwani sijawahi hata kufika huko Mara, ila ni kwamba Mkoa wa Mara haukuwepo na ulianzishwa na Nyerere ambaye Mara ni kwao, kama vile Mwinyi alivyoanzisha Kisarawe kwao.

Sasa hizo sababu za kuanzishwa kwake kila Raisi pia atakupa sababu za kupendelea kwao, Mwinyi na Kisarawe, Mkapa Mtwara corridor, daraja la Mkapa, Daraja la Umoja, Kikwete Bagamoyo, Magufuli Geita.
 
Hii lini mkuu, maana nilisikia majuzi barabara ilifunga

Ila kigoma ingekumbukwa lol

Maana ndo mkoa pekee ambao mpaka sasa haujaunganishwa na lami
Watu wa Kibondo kwa nini nao wasihoji kutokana na ubovu wa barabara zao hasa nyakati za mvua? Huku wakisikia na kuona ktk vyombo vya habari ya kuwa wenzao wanakula mema ya nchi.View attachment 1285596
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu atawekeza kwenye mikoa hiyo ya kanda ya ziwa na mikoa kama Tabora n.k
Kwani wapiga kura wasukuma na wanyamwezi ni zaidi ya theruthi mmoja ya wananchi wote wa Tanzania wanaostahili kupiga kura.Wengi wape.
Kila kitu, kuanzia kuwaanzishia Mkoa wao wa Mara ambao haukuwepo wakati anakabidhiwa nchi mpaka kupendelea na kunyanyua watu wake kama Mkono, Warioba na wengineo.
Hivi unaofahamu Tanzania vizuri au ni zile story wakati ukiwa Gisenyi?
 
Siyo swala la mimi kutaka au kutotaka kwani sijawahi hata kufika huko Mara, ila ni kwamba Mkoa wa Mara haukuwepo na ulianzishwa na Nyerere ambaye Mara ni kwao, kama vile Mwinyi alivyoanzisha Kisarawe kwao.

Sasa hizo sababu za kuanzishwa kwake kila Raisi pia atakupa sababu za kupendelea kwao, Mwinyi na Kisarawe, Mkapa Mtwara corridor, daraja la Mkapa, Daraja la Umoja, Kikwete Bagamoyo, Magufuli Geita.

..mengine UMEONGOPA.

..daraja la mto Rufiji lilianza kujengwa wakati wa Mzee Mwinyi.

..pesa za mradi wa barabara ya Kusini zilitolewa na Kuwait Fund na waziri wa ujenzi wakati huo alikuwa Nalaila Kiula.

..baadaye Kuwait Fund wakalegalega wakaja wafadhili wa Saudi Fund.

..Ujenzi wa barabara ya kusini uliendelea wakati wa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete.
 
Kilimanjaro inayosakamwa Sana na watu wa lake zone, haijawahi hata kutoa Rais jamani. Tofauti kubwa ni akili na Elimu. Lake zone somesheni watoto wenu Sana. Jengeni shule badala ya viwanja vya ndege na madaraja. Hayo madaraja mnatujengea sisi Wapare, Wachagga, Wameru, Wambulu na Waarusha. Tutaleta mitaji huko kujenga hotel, migahawa, bar, yard za magari, Sheli halafu mtaishia kuwa watumwa wetu.
Shell ndiyo nini? Au unamaanisha filling stations au petrol stations?
 
..mengine UMEONGOPA.

..daraja la mto Rufiji lilianza kujengwa wakati wa Mzee Mwinyi.

..pesa za mradi wa barabara ya Kusini zilitolewa na Kuwait Fund na waziri wa ujenzi wakati huo alikuwa Nalaila Kiula.

..baadaye Kuwait Fund wakalegalega wakaja wafadhili wa Saudi Fund.

..Ujenzi wa barabara ya kusini uliendelea wakati wa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete.

Labda ni kweli sina data sahihi, lkn kwa nini linaitwa daraja la Mkapa?
 
Back
Top Bottom