Hakimu Mfawidhi, Kwa uelewa wako, unaamini kuwa airport kubwa ikijengwa Chato, ndiyo itaondoa umaskini?
Umaskini hauondolewi na serikali bali unaondolewa na mtu mmoja mmoja. Serikali kazi yake ni kujenga mazingira wezeshi.
Najiuliza, hivi shughuli kuu za kiuchumi za wananchi wa Chato na Geita kwa ujumla ni nini? Nahisi ni kilimo, ufugaji na uvuvi. Kama nipo sahihi - cha kujiuliza, airport ya Chato itamsaidia namna gani na kwa kiasi gani mvuvi, mfugaji na mkulima wa Chato? Namna nyingine, uwanja ule ni prestige tu kuliko kuwabadilisha wananchi wa Chato na Geita.
Kwa kadiri ya report ya kitengo cha takwimu, Mikoa mitatu inayoongoza kwa utajiri Tanzania ni
1) Dar
2) Kilimanjaro
3) Njombe
Sasa niambie, mkoa kama Njombe umepewa upendeleo gani na serikali hata ukaweza kuizidi mikoa kama Arusha au Mwanza?
Wanaofikiria kuwa upendeleo wa serikali katika kutoa huduma ndio utaleta maendeleo wanajidanganya.
Ndege zitatua Chato lakini wasafiri hawatakuwa wa Chato. Daraja litajengwa Busisi lakini watakaopita na magari ya kifahari juu yake hawatakuwa wananchi wa Misungwi au Sengerema. Faida kubwa kwao itakuwa kuwa kwanza kila siku kuyaona magari yakipita kwenye daraja refu.
Kama kuna kanda au mkoa ambao ni maskini na wanaamini kuwa ni kwa sababu serikali haikuwapendelea, waende wakawaulize watu wa Njombe ni kwa vipi wanaweza kuwa na vipato vizuri huku Serikali kwa muda mrefu ikiwa imewasahau? Nadhani makanisa yameshirikiana na wanachi vizuri zaidi katika kuyatafuta maendeleo kuliko hata serikali.
Kupendelewa kunadumaza akili, huondoa fikra za jitihada na hujenga utegemezi.