Kwanini watu weusi ni vigumu sana kuwa Top 10 ya matajiri na kujenga utajiri wa vizazi (generational wealth)?

Kwanini watu weusi ni vigumu sana kuwa Top 10 ya matajiri na kujenga utajiri wa vizazi (generational wealth)?

Hao watu weusi unaowaongelea hizo biashara wameanza miaka ya 1990. Unataka kuwafananisha na waarabu na wahindi walioanza miaka ya 1900. Kuna mengi ya kujifunza, tuje kuuliza haya maswali in 2100, kutakuwa na Wakinga wengi tu na generational wealth
 
Wengi huwa wanapenda kuwaita mabilioniea lakini kiuhulasia bilionea Tanzania mpaka sasa ni mmoja tu Mo Dewji, wengine wote pia wanaotajwa tajwa sana katika hiyo list ya matajiri kumi 10 Tanzania ni Watanzania wenye asili ya waarabu au Wahindi, labda Bakheresa anaweza kuwa na asili ya blacks ila anaonekana amechanganya damu.

Tangu Reginald Mengi atetereke kibiashara na baadaye kufariki hakujatokea mtu mweusi mwingine katika listi ya matajiri wakubwa Tanzania.

Pia kwa nini utajiri wa wahindi na Waarabu umetembea kutoka kizazi kimoja na kuendelea kukuzwa na kizazi kinachofuata ila kwa weusi tajiri mwanzilishi akifa na utajiri unakufa hapo hapo au taratibu na kinachobaki ni kesi za mirathi na vita za wanafamilia!
Hamuwashirikishi Watoto/familia zenu Toka Wakiwa wadogo Ili kujua thamani ya Mali na mbinu za kuendekeza na kuondoa roho ya choyo.
 
Matumizi yetu ni beyond means.

Si Tanzania hata Ulaya na Marekani familia za watu weusi ziko nyuma kwenye vipato lakini ziko mbele kwenye Matumizi
Pili waafrika wengi huamini kwenye ubinafsi changu n9 changu tu mwingine atafite chake hata akiwa mwanawe au mtoto hawashikishwi kikamilifu kwenye biashara kama wanahisa

Wenzetu watoto hupewa hisa na kuwa sehemu ya umiliki na uendeshaji kampuni ndio maana hudumu .Unakuta mtoto mdogo tu anajua vyote kuhusu biashara ya mzazi hata kiwanda kikubwa au biashata kubwa

Tatu uaminifu wamefundishanana kuheshimiana,uaminifu na kuaminiana Kwenye famikia wote unakuta wanaheshimiana,kuaminiana na waaminifu

Nne watoto na ndugu huandaliwa waje kushika biashara ya familia sio kwenda kuajiriwa serikalini au kokote

Tofauti na waafrika baba anamiliki.mabasi mia Dar mtoto.anamsomesha ualimu wa shule ya msingi akaajiriwe serikalini kijijini Katavi huko.Halafu unakuta anajisifu ohh ajira ngumu ila nadhukuru mwanangu kapata ajira Katavi ya ualimu
 
Kanye West alisema,

"You know, white people get money, don't spend it
Or maybe they get money, buy a business
I rather buy 80 gold chains and go ignorant"

Nasty C alisema,

"— "Black people share cigarettes and beer, but never share opportunities."
 
Hao watu weusi unaowaongelea hizo biashara wameanza miaka ya 1990. Unataka kuwafananisha na waarabu na wahindi walioanza miaka ya 1900. Kuna mengi ya kujifunza, tuje kuuliza haya maswali in 2100, kutakuwa na Wakinga wengi tu na generational wealth
Hakuna watu weusi walioanza biashara miaka ya 1900??
 
Back
Top Bottom