Mkuu leo ni Christmas ujuwe, kunawakati hii jamii inaingiliwa na wachovi hadi naamuwa kupotezea tu. Crucial knowledge is very important and mostly needed to resolve issues that matter to everyday people’s lives, however you seem to be confusing between war crimes and Genocide, may be this lecture is for another day… lakini hivi msomi mwenye akili zake kama wewe ni namna gani hili jambo linakupiga chenga? Unachanganya ICTR ambayo kazi yake ni kuwasurubu wauwaji wa kimbali(regardless of their failures) wasted a lot of resources to deliver disappointments. War crimes are completely a different story brother unless you are new Madam Ingabire mouth piece… haya kasheherekee bwana Yesu kazaliwa, furahisha roho yako bingwa alafu ukale pilau… Kumbuka shida kubwa ni kwamba haya mambo ya Rwanda yaliletwa na walimu wako (wazungu)[emoji30] hadi pale utakapoweza kutofautisha nyakati na nchi na mabara ntarudi hapa na herimu dhatiti itakayo tuwezesha sisi miafrika kubadili fikra zetu kwa maendeleo ya kudumu.
Acha upumbavu Mchambaima1, wewe ni msomi uliyeenda shule na sitegemei kuona umekuwa na unazi wa namna hii kiasi kwamba unaleta hisia za kitoto kwenye mijadala.
Wewe Layman unapotaka kunifundisha mimi Lawyer ambaye nimehusika na ICTY, ICTR, ICC na SCSL kuhusu sayansi ya jinai za kimataifa (The Jurisprudence of Core International Crimes) napata ukakasi. Nahisi kama ndugu yangu umegeuka kuwa mpiga ramli kama ndundami wa mganga, kama walivyo wajinga wengi wanaoleta ukasuku hapa jukwaani.
Ila kukupasha tu ambacho hukifahamu au labda umekaririshwa ni hiki: Genocide (Mauaji ya kimbari) kwa miaka yote ilikuwa ni sehemu ya uhalifu dhidi ya ubinadamu (Part and Parcel of Crimes Against Humanity). Mahakama za Leipzig, Nuremberg na Tokyo zote zilisema hivi wewe Mnyarwanda ni nani hadi utake kubisha na kuleta yako ???
Hili kosa lilikuja kutengwa na kuanza kujitegemea kama lenyewe baada ya kina Professor Raphael Lemkin, Myahudi kulalamika na kuandika tasnifu ndefu kuhusu hili baada ya vita ya pili ya dunia. Ndiyo tukapata vitu The United Nations Genocide Convention, Treaty of 1948.
Kiufupi, ili kosa la mauaji ya kimbari (Genocide) liweze kufanyika ni lazima kuwa na kosa la uhalifu dhidi ya ubinadamu (Crimes Against Humanity) au Uhalifu wa kivita (War Crimes). Mara zote kosa la Genocide limetokea ndani ya utendwaji wa haya makosa mawili ya War Crimes na Crimes Against Humanity.
Sasa basi: kinachotofautisha Genocide kutoka kwenye War Crimes na Crimes Against Humanity ni kitu kiitwacho NIA/LENGO (Genocidal Intent). Mfano, mwanajeshi anapolipua kombora hovyo dhidi ya raia, kisheria huu ni uhalifu wa kivita (Targeting Civilians who do not take direct participation in hostilities).
Lakini, kama ulipuaji huu wa makombora umelenga kuumiza jamii ya watu fulani kisheria hilo kosa litakuwa ni mauaji ya kimbari (Genocide), au vyote. Yaani kosa la kwanza (First Count) litakuwa ni uhalifu wa kivita na kosa la pili (Second Count) ni kuratibu mauaji ya kimbari.
Kukusaidia tu, kule ICTR kuna watu wengi walishitakiwa kwa kosa la Genocide, lakini baada ya muendesha mashitaka kushindwa kuthibitisha NIA OVU/LENGO OVU (Genocidal Intent) watuhumiwa walibadilishiwa kosa na kuwa Uhalifu dhidi ya ubinadamu, au uhalifu wa kivita au kuachiwa.
Moja ya watu waliokutwa na hii kadhia, ni Mzee wenu Casimir Bizimungu ambaye aliwahi kuwa waziri wenu wa mambo ya nje. Pitia kesi yake kule ICTR iitwayo Prosecutor v Casimir Bizimungu. Hii kesi ilileta utata mwingi mno, na nashangaa.
NB: Ikumbukwe kabisa ICTR ndiyo mahakama ya kwanza kabisa duniani kusikiliza kosa la Mauaji ya Kimbari (Crime of Genocide) kama kosa linalojitegemea nje ya Uhalifu dhidi ya ubinadamu. Kesi ya kwanza ikiwa ni ile ya Kaka yako na ndugu yako Bwana Jean Akayesu.
Japo, hii siyo mara ya kwanza kosa la Genocide kusikilizwa kama sehemu ya kosa la Uhalifu dhidi ya ubinadamu (Crimes Against Humanity). Kule Nuremberg na Tokyo walisikiliza hivyo.
Huu ndiyo ukweli mchungu, Hutaki Unaacha.
Jingine muhimu ni kwamba, binafsi huwa nakuheshimu mno hapa jukwaani, kwasababu naamini wewe ni kati ya watu wenye uelewa mkubwa na waliokomaa kihisia. Ila kama ukiendelea na huu upumbavu unaoufanya hapa wa kuleta hisia, unazi na majungu-majungu ni dhahiri ntakupuuza na kukudharau.
Binafsi, nawapenda sana Wanyarwanda, Warundi na Wakongo tokea ndani ya moyo wangu. Nawachukulia kama ndugu zetu wa damu kabisa, na hivi ndivyo ilivyo. Napenda kuona tukifika mbali pamoja na huenda tukawa taifa moja huko mbeleni, endapo Mungu akipenda.
Ila huu upumbavu wenu wa kutaka kuchinjana hovyo kama wanyama kila siku na siasa za kinazi usipobadilika utakuja kuwagharimu. Mimi nilitegemea wasomi wa kizazi chetu kama wewe na mimi ndiyo tukae, tufanye mijadala na tathmini kwamba tulikosea wapi huko nyuma na tufanyaje sasa ili tuweze kusonga mbele.
Nasikitika kuona Bwana Mchambawima1, unaanza kuniita mimi majina ya kipumbavu. Mara Mhutu, Interahamwe, Genocidal Maniac, Mzungumzaji wa Ingabire n.k jambo ambalo limenichefua mno nyongo.
Ila uhalisia mchungu ni huu: Matatizo na mafanikio ya Rwanda (Tutsi + Hutus) hayaihusu Tanzania hata kidogo, hapa tupo tunafanya mijadala kama Pan-African Ideologues na Future African Leaders tu. Lolote jema au baya likitokea Rwanda siyo mzigo wetu, binafsi huu ndiyo msimamo wangu siku zote.
Hivyo mkuu tuheshimiane bila kukwaruzana....
Ahsante.