Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Wazungu waliwabagua Sana na kuwaua Wayahudi huko kwao miaka ya nyuma, kwa Sasa wanawatetea kwa nguvu zote Kama njia ya kujisafisha na madhila ya nyuma ndio maana wanafumbia macho yanaowakumba Wapalestina.
Sikupenda kujiingiza kwenye mjadala juu ya ugaidi na mauaji ya kimbari vinavyotokea Gaza, ila kinachoendelea kinatisha.
Sikupenda kwa sababu Waafrika yanapotukuta haya, huwa wenzetu hawajali ukiachia mbali kutubagua tunapokwenda kwao ingawa hatuwabagui wajapo kwetu.
Sijui kwanini wazungu wanawachukia hawa jamaa wasio na nchi kiasi hiki na kuwapenda na kuwakumbatia makaburu wa kiyahudi.
Je alichofanya marehemu sorry rais Joel bin Laden kweli kinafaa kwa mtu wa umri ule? Je nini kitafuatia baada ya watu kuchoka na kujua kuwa kumbe haki za binadamu wanazoimba hawa wanafiki ni uongo na mkenge mtupu?
Je wao watakuwa salama katika uonevu huu? Nalalamika tu
Kwa ufupi Israel ya sasa imekuwa zaidi ya Africa Kusini ya kina Botha (makaburu) na dunia ipo kimya na haina ubavu mbele ya ubeberu wa kimagharibi.
Arab league ndio hiyo imekuwa Kama AU tu
zitto junior JokaKuu FRANC THE GREAT The Boy Wonder T14 Armata