Kwanini Yesu anaitwa Mungu? Sababu na ushahidi huu hapa

Mwanzo unaozungumzwa ni wa mbingu na nchi. Kabla ya mwanzo huo Mungu alikuwepo, maana Yeye hana mwanzo
Sawaaaa je! Kabla ya hiyo mbingu yeye alikuwa wapi? Au yeye hayupo ndani ya mbingu.
 
Kumbe mwanadamu ana uungu?
(Zaburi 82:6)

Mimi nimesema ninyi miungu, na Wana wa aliye juu, nyote pia.

Tumepewa kutawala vyote duniani, chini ya mbingu, shetani akiwemo Yu chini yetu,

Muhimu tuishi maisha MATAKATIFU.

Hukujua sisi ni miungu?
 
Duh! Kumbe binadamu wote sisi ni miungu
 
Swali lako nililijibu nikidhani umeuliza kuhusiana na kitabu cha Mwanzo(Genesis). Hata hivyo kitabu cha Yohana 1:1 hakisemi kwamba Yesu alianza kuwepo wakati huo, bali kinaeleza kwamba Yesu(Mungu Mwana) alikuwepo hata wakati wa huo mwanzo wa uumbaji wenyewe, akiwa pamoja na Mungu Baba.

Hayo maneno ya Yohana 1:1 m, anayesema hayo ni nani ??
 
Miungu ni mingi,

Mungu ni MMOJA tu,

Na Jina la Mungu huyo mmoja,Jina tulilopewa WANADAMU liwezalo kuokoa, ni Yesu Kristo/YESHUA HAMASHIACH
Vipi kuhusu Jehova yeye siye Mungu ama
 
Vipi kuhusu Jehova yeye siye Mungu ama
Maana ya YEHOVA ni YAHWEH,

Ni sawa na kusema BWANA Mungu, BWANA,ni title za office za Mungu kulingana na KAZI, mission husika.

Lakini Jina la Mungu personal la Mungu huyo mmoja ni YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH.
 
Sasa Mungu ambaye yesu anadai alimtuma kwa wana wa Israel ni yupi
 
Wana wa Mungu ni tofauti na uzao wa nyoka.

Sasa sijui u katika kundi lipi?

Katika Injili za Mathayo, Marko na Luka, Yesu ameitwa mara 22 kwa jina la "Mwana wa Mungu", lakini hata mara moja yeye mwenyewe hakujiita kwa jina hilo.

Katika Mathayo 27.43 yanatajwa maneno ya wakuu wa makuhani wa Kiyahudi pamoja na waandishi na wazee waliokuwa wakimdhihaki, si maneno yake yeye Yesu.

Hao walikuwa wakimzulia kuwa anadai uwana wa Mungu, na anadai kuwa ni Mfalme wa Israeli. Mara nyingi waliokuwa wakimwita Mwana wa Mungu walikuwa ama wendawazimu, wenye pepo wachafu, au askari wa Kirumi ambao tokea hapo wao ni washirikina, mapagani.

Ama mwenyewe Yesu alikuwa daima akipendelea kujiita mwana wa Adamu kwa Kiebrani, lugha yake, Bin Adam, yaani ni binaadamu, mtu tu.

Katika Injili jina hili la Yesu kuitwa mwana wa Adamu limetajwa yapata mara 80. Mahasimu zake wa Kiyahudi walimzulia kuwa alidai kuwa ni Mfalme wa Mayahudi ili kumchongea kwa watawala wa Kirumi, na kuwa alidai kuwa ni Mwana wa Mungu ili apate kuchusha kwa Mayahudi.
 
Miungu ni mingi,

Mungu ni MMOJA tu,

Na Jina la Mungu huyo mmoja,Jina tulilopewa WANADAMU liwezalo kuokoa, ni Yesu Kristo/YESHUA HAMASHIACH

Lete ushahidi wa aya kuthibitisha maneno yako
 
Katika Injili za Mathayo, Marko na Luka, Yesu ameitwa mara 22 kwa jina la "Mwana wa Mungu", lakini hata mara moja yeye mwenyewe hakujiita kwa jina hilo.

Katika Mathayo 27.43 yanatajwa maneno ya wakuu wa makuhani wa Kiyahudi pamoja na waandishi na wazee waliokuwa wakimdhihaki, si maneno yake yeye Yesu.

Hao walikuwa wakimzulia kuwa anadai uwana wa Mungu, na anadai kuwa ni Mfalme wa Israeli. Mara nyingi waliokuwa wakimwita Mwana wa Mungu walikuwa ama wendawazimu, wenye pepo wachafu, au askari wa Kirumi ambao tokea hapo wao ni washirikina, mapagani.

Ama mwenyewe Yesu alikuwa daima akipendelea kujiita mwana wa Adamu kwa Kiebrani, lugha yake, Bin Adam, yaani ni binaadamu, mtu tu.

Katika Injili jina hili la Yesu kuitwa mwana wa Adamu limetajwa yapata mara 80. Mahasimu zake wa Kiyahudi walimzulia kuwa alidai kuwa ni Mfalme wa Mayahudi ili kumchongea kwa watawala wa Kirumi, na kuwa alidai kuwa ni Mwana wa Mungu ili apate kuchusha kwa Mayahudi.
Kidogo naanza kukuelewa
 
Sasa Mungu ambaye yesu anadai alimtuma kwa wana wa Israel ni yupi
Ndio ujasusi huo.

Mungu aliye Roho,kuja katika mwili wa mwanadamu, lazima ajishushe na kusema ametumwa, wakati katika Roho, ndiye huyo huyo Mungu aketiye katika KITI Cha enzi Mbinguni.

Mungu ni MMOJA tu, na Jina lake ni YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH
 
Kwa hiyo alikuwa anadanganya tu
 
Back
Top Bottom