1. Ushahidi wa Kibiblia
Yohana 1:1 – "Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu."
Tito 2:13 – "Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo."
Yesu mwenyewe alikiri kuwa ni Mungu:
Yohana 10:30 – "Mimi na Baba tu umoja."
Yohana 8:58 – "Amini, amini, nawaambia, Kabla Abrahamu hajakuwako, Mimi niko."
2. Sifa za Kimungu alizo nazo Yesu
Uwepo wake wa milele – Mika 5:2
Uwezo wa kusamehe dhambi – Marko 2:5-7
Uwezo wa kutoa uzima wa milele – Yohana 10:28
Uwezo wa kuhukumu ulimwengu – 2 Wakorintho 5:10
3. Miujiza inayodhihirisha Uungu wa Yesu
Kubadili maji kuwa divai (Yohana 2:1-11) –
Kutembea juu ya maji (Mathayo 14:25-27)
Kutuliza dhoruba (Marko 4:39)
Kufufua wafu (Yohana 11:43-44)
Kupaa mbinguni (Matendo 1:9-11)
4. Unabii wa Agano la Kale ulitimia kuhusu Uungu wa Yesu
Katika Isaya 9:6 – Yesu anaitwa "Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele."
Katika Mathayo 1:22-23, tunasoma jinsi unabii huo ulivyotimia:
"Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa njia ya nabii, akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, Naye watamwita jina lake Imanueli; yaani, Mungu pamoja nasi."
5. Watu Walimwabudu Yesu na kukiri kuwa ni Mungu
Mathayo 28:9,17 – Wanafunzi wake walimsujudia.
Yohana 20:28 – Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yesu alipoambiwa na Tomaso kuwa ni Mungu, hakukanusha.
Kama unadai Yesu sio Mungu, toa sababu zako hapa
YESU SI MUNGU:
KWA SABABU MUNGU NI MMOJA TU
Baadhi ya Wakristo wanatafuta sababu na udhuruwa kumfanya Yesu kuwa Mungu. Kwa mfano husema kwamba Yesu ni Mungu au mwana wa Mungu au Yesu ni Mungu mdogo au Yesu ni nafsi moja ya Mungu.
Mambo haya yote ni kufuru tupu iliyovuka mipaka. Kwa sababu sawa na Biblia Mungu ni mmoja tu. Hakuna
Mungu mdogo wala Mungu mwana.Biblia inasema:-
1. Wewe naam, wewe peke yako ndiye Mungu wa falme zote za dunia; wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi.
(2 Wafalme 19:15).
2. Kwa kuwa ndiwe mkuu, wewe ndiwe mfanya miujiza, ndiwe Mungu peke yako. (Zaburi 86:10).
3 Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma, (Yohana 17:3).
Sasa wakati Mungu wa pekee ni mmoja, hivyo Mungu zaidi ya mmoja ni wa uwongo.
4. Mwawezaje kuamini ninyi, mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti? (Yohana 5:44).
5. ...Hakuna Mungu ila mmoja tu. Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni au duniani; kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi. Lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu. aliye baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake.
(1 Wakorintho 8:4-6).
Sawa na aya hizi hakuna MunguSawa na aya hizi hakuna Mungu ila mmoja tu.
Ingawa miungu wa bandia wanatajwa tajwa mbinguni na ardhini. Basi sasa ambaye anaamini mungu minghairi ya Mwenyezi Mungu anatoka katika imani na anaingia katika ushirikina kwa sababu ya kuwaita miungu zaidi ya mmoja ambaye ni wa kweli na wa pekee.
6. ..Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu. (Marko 2:7). Aya hii inathibitisha
kwamba mwenye kufuta na kuondoa dhambi ni mmoja tu ambaye ni Mungu. Yaani hakuna mungu wa pili wala
45:21-22, 46:9; Marko 12:32; Luka 18:19; Mathayo 4:10; Warumi 3:30; Timotheo 1:17, 2:5.
Hakuna aya hata moja inayosema kwamba Yesu ni Mungu.