Kwanini Yesu anaitwa Mungu? Sababu na ushahidi huu hapa


Hivi hizi Habari Yohana aliziandika kutoka kwa nani ?

Hapo bado hujathibitisha sababu hiyo ni falsafa tu ambayo haina uhalisia zaidi ya kucheza na maneno.

Naomba unipe ushahidi hayo maneno Yohana alyapata wapi ? Je aliyapata toka kwa Yesu mwenyewe au ilikuwaje ?

Yesu inajulikana alikuwa na wanafunzi wake, je kuna sehemu yoyote ambayo wanafunzi wa Yesu wamenukuliwa wakisema Yesu ni Mungu au mwana wa Mungu ?
 
Alikufa akafufuka. Wakati anakufa alikuwa ameuvaa mwili wa kibinadamu ili damu imwagike tupate ondoleo na msamaha wa dhambi.

Haya maneno ni Yesu mwenyewe aliyasema au wewe ndio unayasema ?

Lakini hizi ni sifa za udhaifu, wakati Mungu wa kweli ameepukana na udhaifu kwa sura zake zote.

Inamaana hakukuwa na namna bora ya ondoleo la msamaha mpaka afe ? Lakini kuna uhusiano gani kati ya dhambi na kufa ?
 
Inasema ametokana na neno lake la "kuwa" Na akawa
Acha porojo wewe 😃

Halafu mimi nimemuuliza namna yeye kalijua hilo kupitia biblia
Waislam tuacheni kupindisha Aya, "alisikika kiongozi wa kiislamu akiwaambia viongozi wenzake😂😂
 
Kwa hiyo yesu ndiye huyohuyo mungu baba
Sahihi ndiyo maana kuna mwanafunzi wake mmoja anaitwa Filipo... alimwambia Yesu tuonyeshe 'Baba' yatosha, Yesu akamjibu kwa kumshangaa kuwa 👉filippo umekuwa nami siku zote usinijue! anionaye mimi kamwona Baba, mimi na baba ni kitu kimoja...mwisho wa kunukuu.
 
Haya tupate matangazo kidogo kutoka studio
 

Attachments

  • 6d4bb2de4bcbc3b254d4f4853ef2396d_1740810709650.mp4
    10.1 MB
Wanaomuita yesu ni Mungu hao wote ni katika watu waliokufuru, na ibada za watu hao waliokufuru huomba kwa jina la mwanadamu huyo anaeitwa yesu badala ya kuomba kwa jina la Mungu mmoja aliemuumba huyo yesu.
Hapo ndo wananichanganya Mungu ni Yesu au nani
Mara alisema Niko kabla Ibrahim kwani kipindi Cha Ibrahim shetani hakuwepo
Hebu watueleze vizuri Mungu ni Yesu au Yesu ni Mwana wa Mungu au ni mtume wa Mungu na alizaliwaje Yani Mungu akakaa tumboni kweli na akaanza Kujifunza kukaa kutembea
 
Kwahiyo alimaanisha yeye ndio Mungu au alimaanisha anayofanya ametumwa na Mungu hivo wataomfata ni sawa wsmefuata maagizo ya Mungu
 
Kwahiyo alimaanisha yeye ndio Mungu au alimaanisha anayofanya ametumwa na Mungu hivo wataomfata ni sawa wsmefuata maagizo ya Mungu
Yeye ndiyo mungu ...ndiye mfalme wa mbinguni na mfalme mbinguni ni mmoja tu ndiyo maana anayo mamlaka ya kusamehe dhambi na kuhukumu siku ya kiama na kufufua wafu wote siku ya kiama
 
Nafsi ya mungu ipo milele nafsi ya mungu ilishuka duniani kipindi cha mtume Musa kama mti uwakao moto na musa alikili kuwa huo mti uwakao moto ni Mungu mwenyezi ...na nafsi ya mungu imekuja duniani kwa kutwaa mwili wa mwanadamu na kuitwa Yesu....mungu ni mmoja tu na nafsi yake ni moja tu ...mnajifanya amuelewe kasomeni injili kwa makini.
 
Yesu ni NENO ...naye neno akatwaa mwili akaja duniani amejaa neema na rehema...nasi tukauona utukufu wake kama mwana pekee wa mungu atokaye katika kifua cha baba ...hapo ni alionekana kama mwana...maana yake siyo mwana ni Mungu mwenyewe pia aikusema neno alitamka neno bali imeandikwa yesu ni huyo neno mwenyewe amekuja ulimwenguni.
 
Soma vizuri ulichoandika
 
Haya tupate matangazo kidogo kutoka studio
Dini ya kweli ya mwafrika ni ile iliyokuwepo kabla ya ujio wa watu weupe. Tutapigana,tutachukiana,na kupalangana Sana na hatuelewi hizo chuki zatoka wapi. Tunapigana na kuchukiana bure tu...🏃
 
Soma vizuri ulichoandika
Sijakosea tatizo lako unabisha bila ya kwanza kuisoma injili ...waislamu wanasema yesu alitokana na neno la mungu la "KUWA"kitu kikawa kama alivyo umbwa Adamu ...ila kuna tofauti ya 👉NENO kutamka kuwa na kitu kikawa na huyo NENO 👉 kutwaa mwili wa binadamu na kuwa mwanadamu
 
Yesu sio Mungu
Yohana 14:28 – “Mlisikia jinsi nilivyowaambia, ‘Ninakwenda zangu, nami nitarudi kwenu.’ Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuniliko.”

Yohana 17:3 – "Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma."

Mathayo 27- 46 "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…