Hatujadharau wanawake,vitabu vyote vya dini mwanamke amepewa hadhi ya kipekee na utukufu usioelezeka ,Cha kushangaza yanayohubiriwa kwenye madhabahu ni tofauti na aliyofundisha Yesu kuanzia Kwa madam Mchungaji Rwakatare ,Zumaridi mpk Kwa Don Davie ,,,mmeitoa wapi hiyo amri ya kutuletea wachungaji na mitume ya kike Hali ya kuwa Yesu hakuwa expose wanawake??
Kupitia mwanamke Hawa/Eva dhambi iliingia ulimwenguni na kupitia mwanamke Mariam mwanamke alirudishiwa heshma kwa kumbeba Kristo Yesu
Na adhabu ya hiyo dhambi ndio ilimfanya mwanamke ashindwe kufanya baadhi ya majukumu
ADHABU YA MWANAMKE
MWANZO 3:15-16
15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
LUKA 1:28-35
28 Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.
29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?
30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?
35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.