Tender ilitangazwa na kampuni zili bid, wakati wa kufungua technical proposals zao ulifanyika kwa uwazi tena kwenye Tv last month na kipindi kilikuwa live. Ni vyema ungeuliza kuliko kuhitimisha kwa vitu ambavyo huna ufahamu navyo.
Pili, Je tenda hii ya Azam ina faida kwa mpira wetu wa Tz, jibu ni ndio, sponsor mkuu Vodacom anatoa 3bn kwa mwaka saivi wakati Azam yeye ni broadcasting right tu amekubali kutoa 22bn kwa mwaka, kabla Azam alikuwa anatoa 23bn kwa miaka mitano ( 4.5bn kwa mwaka) hivyo kupanda hadi 22bn kwa mwaka ni ongezeko kubwa hata clubs zenyewe hazikutegemea, tujifunze kushukuru.
Je, kwa nini TFF na Bodi ya ligi wamekubali mkataba wa miaka 10 badala ya mkataba mfupi, mazingira ya Tz ni tofauti na nchi zilizoendelea, huku viwanja vyetu camera sio plug and play, kuna uwezekazaji mkubwa inabidi ufanyike ili viwanja vyetu vyote uweze kuona camera kwa angles zote, mtu hawezi kuwekeza pesa nyingi halafu mkataba unaisha kabla hata hajamaliza kurudisha pesa yote.