Kwanini zabuni ya kuonesha Ligi Kuu Tanzania Bara haikutangazwa, kapewa Azam moja kwa moja?

Hawa ndio watanzania wamejaa uchawi na umaskini,hapo utakuta anamtolea maneno Mo ukimwambia lipa salary hata mchezaji mmja Domo linalegea
 
Mleta siredi unahitajika huku boss.


Umeandika makala ndefu bila kufanya utafiti upate ukweli.

Umeambulia za USO.
 

Yaan jamaa chenga sana nakumbuka msimu wa 2017-2017 ile mechi ya hisani Kati ya yanga na Azam ilirushwa na ATN sikumbuki ilikuaje wakapewa ile mechi lkn ilirushwa hovyo sana sikuwahi kuona looh......

Et leo hii azam yupo na mitambo ya kisasa kabisa anarusha pas na malalamiko yoyote watu tuongea tu ujinga kwann kapata kwa iyo mnataka turud enz za rtd sio [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimesoma imebidi nicheke tu kwanza naomba acha kufananisha wanachofanya EPL kutaka kukileta fananisha chungwa na chungwa. Hiyo Billion 6 uliyotaja ni ya ndani tu UK kuna international bidding na sponsers wengine ni kama 80% ya bugdet ya Tanzania. Tuache hilo turudi hapa unasema ziko TV nyingi nchini wanataka hebu usitaje nyingi taja moja tu maana nikisema nyingi hutaweza taja moja tu. League hii ilikuwepo kabla hata ya Azam Tv kuanza sasa walikuwa wapi hao? tuseme wapo na unataka wafanye bid je unajuwa bid ina base katika commercial na technical tuache commercial unaweza kusema wako matajiri na nani anavifaa nchi hii wa kuweza kurusha mpira live coverage nchi nzima? ITV, TBC, Wasafi..... tunabaki kuongelea juu juu tu wakati ukweli tunaujuwa AZAM hana mpinzani nchi sio mpinzani wa karibu ni hakuna kabisa. Wewe unadhani ni kuonesha tu huku nyuma kuna gharama za production kuna team kubwa inafanya kazi wewe unawasha TV unapata bidhaa huko EPL production inafanywa na EPL broadcasters wanapewa bidhaa tu iko ready ya kiwango. Nakuhakikishia siku Azam wakija kufunga biashara na ndio siku tutauzika mpira wetu. Miaka 8 nyuma hakuna hata aliyekuwa na habari na league yetu kaja Azam kakuvisha vizuri umependeza kidogo sasa unataka kujifanya mimi level nyingine unaanza kudharau bwana aliyekupendezesha. Mimi nataka utaje kampuni moja tu Tanzania ya kushindana na Azam, kwa taarifa yako hata EPL mwakani wameongeza contract tu kwa Sky na BT bila bidding pia kuna kitu kinaitwa single source justification unaweza kununua sehemu moja ukithibitisha hakuna mtu mwingine anauza bidhaa hii sio kila kitu bidding.
 
Spain espn wana 8 yrs contact
Wakat uholanzinwana 10 yrs

Acha ushamba na roho mbaya we ungetoa hela basi
Nahisi ulilenga ku mu quote mwingine,

Me sina shida na mchakato mzima
 
Tenda ilitangazwa, tatizo wengi hamfuatiliii. Mkisikia kitu kimetangazwa, mnakurupuka na kuongea mashudu. Uwe unauliza kwanza! Hii ishu ilitangazwa mno kwenye vipindi vya michezo na magazeti. Acha kukurupuka, unajiaibisha.
Sisi wabongo kama kawaida yetu alishinda yule Vunja bei ndio watu wanaamka tenda ilitangazwa lini hatukubali utasema tuna billion2. Kama sheria zinatungwa bungeni kimya wakipigwa na rungu la sheria utasikia hii sheria gani mbaya hatuijui. Sasa tender Azam ashindane na kina Agape na TBC 🤣 kwenye technical tu wanakatwa kabla hata ya kufungua commercial.
 
Hata ingetangazwa.
Ungeweka bei gani KUSHINDANA NA bakhresa.
Vitu vingine inabidi muviache Tu vipite
 
Yani huwezi ata kutumia nguvu nyingi kuuliza mtoa mada ni shabiki wa team gani hapa Tanzania, waga mnakurupuka sana ndugu zetu na kufanya baadhi ya washabiki wenzenu ambao ni smart kuonekana nao ni wale wale

Tenda ilitangazwa kupitia vyombo vya habari na kimoja wapo ni TBC, walioomba wakaomba na aliopata ndio huyo sasa, katafute tena data kuwa ligi ya uingereza ina wamiliki wa haki za matangazo wangapi, mwenye haki ni mmoja Tu na anawauzia hao wengine wote kina bein sports,Super sports nk

Lakini pia kuhusu miaka mingi bado huna hoja mkuu, kagugo mkataba wa laliga niwa miaka mingapi, lakini pia Kwa akili ya haraka haraka unazani ni nani ambae angeweza kutoa hela hiyo aliyotoa Azam? Na kuhusu thamani ya pesa kuwa ni ndogo miaka ya badae we hujaona hiyo hela inaongezeka kila msimu? Unajua mkataba wa Kwanza ulikuwa Una thamani ipi? Na huu umeongezeka mara ngapi ya ule wa Kwanza?
 
Namba 2 unakosea.
Ni BT na Sky
Mkuu nakubaliana na ww kabsa na kwamba bt sports yupo lakini hua anaonyesha meschi zisizozidi 58 kwa msimu tu kati ya 380 na, pia mkataba mpya kuna amazon sports wao wanaonyesha mechi zisizozidi 20 tu.

Kwa mechi zingine zote wananunua rights toka sky sports.

Kiufupi hii issue ya tv rights za epl ni ndefu na inahitaji muda kuelezea.

Nakubali mkuu, tuendelee kulijenga taifa na tuepuke wapotoshaji.......
 
Kiuzalendo zaidi Hii tenda walitakiwa wapewe TBC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…