Kwanini Zitto anatukana Serikali nzima na anaachwa tu?

Kwanini Zitto anatukana Serikali nzima na anaachwa tu?

SONGOKA

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
1,836
Reaction score
1,846
Mara kadhaa Zitto amekuwa akikejeli na kutukana serikali ya awamu ya tano tena kwa maneno ya kebehi na dharau bila uoga wowote wakati akijua kuwa serikali ni pamoja na sisi wananchi wote wa nchi hii. Maneno yake maarufu anayotumia kuitukana serikali na nchi kwa ujumla ni "mazwazwa" na "washamba"

Hivi hiki kiburi cha kutuita wananchi wa Tanzania na viongozi wetu tuliowachagua kuwa ni MAZWAZWA na WASHAMBA Zitto unakipata wapi?

Serikali kwanini mnamruhusu Zitto kutukejeli na kututusi wananchi na watanzania wote? Sisi watanzania tuliowachagua hao viongozi na kuiweka Serikali ya awamu ya tano madarakani tutakuwa katika nafasi gani kama viongozi tuliowachagua wanadhalilishwa eti ni WASHAMBA na MAZWAZWA,

brother Zitto jisitiri na sisi tukusitiri,
 
SONGOKA,
Watu wa Pwani huwatania watu wa bara kwa kuwaita " Watu Washamba" kwa kifupi Washamba

Na watu wa bara huwatania watu wa Pwani kwa kuwaita masleki yaani Goigoi

Hizo ni lugha tu labda kama wewe siyo mtani ndio utaona kama matusi lakini watu wa Pwani hawana kitu kinachoitwa matusi lakini watu wa bara wana kitu kinaitwa " mchezo wa matusi " lakini ukikuwa mchezo huo hualalishwa tena kwa sherehe kubwa!
 
Wewe mwananchi unalalamika wakati wengine tunafurahi kwakuwa Zitto kawa sauti ya wengi wasio na sauti.

Ukiambiwa zwazwa au mshamba hata siku moja sio tusi, labda kama huelewi maana ya hayo maneno.

Halafu Katiba ya nchi ibara ya 18 imetoa uhuru wa kutia maoni jitahidi kuwa mvumilivu.
 
SONGOKA,
Ndio maana zitto anawaita MAZWAZWA na WASHAMBA ,kama unaona ametukana mpelekeni mahakamani. Sasa Kadege kamoja kangepokelewa hata na mkuu wa wilaya lakini serikali nzima inaenda Mwanza na kutumia Mabilioni ya Tsh sasa sio USHAMBA NA UZWAZWA huo? Hizo Bilioni mnazotumia kutapakanya kupokea ndege tungejenga Zahanati au Hospital ngapi za 300m?
 
Back
Top Bottom