Kwanini Zitto anatukana Serikali nzima na anaachwa tu?

Kwanini Zitto anatukana Serikali nzima na anaachwa tu?

Katika moja ya vitu vinavyoonesha ujinga, kimoja wapo ni simplification.

Kwamba, ukihoji kusakamwa Mtanzania anayetumia haki yake ya kikatiba kujieleza, kwa kutaka kuangalia facts, basi wewe unaungana na beberu.

Kitu cha kwanza kuelewa ni kwamba, mimi sijaungana na mtu, mimi natetea dhana.

Simple minds discuss people, average minds discuss events, great minds discuss ideas.

Mimi simjadili mtu, simjadili Zitto, sijadili mabeberu, sijadili tukio hili, mimi nakwenda mbali zaidi.

Najadili idea, najadili free speech Tanzania, najadili constitutional rights za Mtanzania, najadili ikiwa serikali ni inaongozwa na washamba, factually, na mtu akasema serikali inaongozwa na washamba, mtu huyo atakuwa katukana au kasema ukweli tu?

Hujajibu hoja, unaleta viroja vya mabeberu.

Habari za mabeberu naweza kukwambia ni narrative inayotumiwa sana na watawala kuwafunga macho wanaotawaliwa ili wanaotawaliwa waone mbaya wao ni huyo beberu, wasione mabaya yanayofanywa na mtawala wao hapo Ikulu.

Huyo Magufuli ni beberu mkubwa sana.

Ni beberu kwa sababu anaendekeza ubabe wa kufungia uhuru wa kisiasa, vyama vya siasa vinakosa uhuru wa kikatiba wa kufanya mikutano.

Ni beberu hata kuongea vizuri hajui, baba mzima mwanamme anatishia kupiga shangazi za watu, yani mwanamme mzima kakosa wanaume wenzake kupigana nao aende kupiga shangazi za watu?

Ni beberu anachota fedha bila bajeti, ananunua vitu bila tender.

Ni beberu ameingilia biashara ya korosho, mpaka mapato ya mazao ya kilimo yameshuka kwa asilimia 55 kwa mwaka mmoja tu unaoishia Agosti 2019. Ripoti ya Bank of Tanzania ya Oktoba 2019 imeonesha hilo. Hizi wala si habari za The Economist.

Sasa unapowasema mabeberu, mbona huyo beberu Magufuli unamsahau?
Nimekukubali Mkuu, poleole wataelewa tu hawa washamba
 
Back
Top Bottom