Kwaresma Sio mpango wa Mungu, ni mihemko tu ya kibinadamu

Kwaresma Sio mpango wa Mungu, ni mihemko tu ya kibinadamu

JUMATANO YA MAJIVU NI UPAGANI

Ni “siku ya kwanza ya Kwaresima kama kitendo cha toba, matawi ya mitende yaliyotunzwa kutoka “jumapili ya matawi” ya mwaka uliopita yanachomwa mpaka kuwa majivu na yanawekwa kwa umbo la msalaba juu ya kipaji cha uso wa kila mmoja katika siku hiyo.” -(Webster’s Dictionary, Carnival).
Siku ya jumatano ya majivu, ni siku ya kwanza ya kipindi cha kwaresima, na katika siku hiyo watu huwa wanapakwa majivu kwenye vipaji vya nyuso zao–Jiulize mwenyewe Je ni wapi katika Biblia unaweza kuona desturi kama hii? Hata kipindi cha Yesu na mitume wake walipomega mkate, hawakuwahi kuanza na kitendo cha kupakana majivu.

Kwaresima ni kipindi cha kufunga na toba cha siku 40 kinachoanza katika siku ya “Jumatano ya majivu” na kinaendelea mpaka siku ya pasaka. Kwaresima haionekani popote katika Biblia, hata Yesu na mitume walipomega mkate walikuwa hawajawahi kufunga kwanza siku-40 za Kwaresima. Historia inasema…
“Lakini ungetakiwa kujua, kwamba kadri kanisa la awali lilivyoshikilia ukamilifu bila kuharibika, uadhimishaji wa Kwaresima haukuwepo.” -Johannes Cassianus, First Conference Abbot Theonas, chapter 30.
Lakini baada ya mitume na Wakristo wote wa mwanzo kufaliki, kanisa Katoliki liliingiza uadhimishaji wa kipindi cha Kwaresima na kudai kwamba kinawakilisha siku-40 alizofunga Yesu jangwani. Lakini kwa vyovyote, Kwaresima ya siku-40 za kufunga kabla ya pasaka, ilisherehekewa na wapagani wa zamani kwa ajili ya jua. Historia inatuambia…
“Siku-arobaini za kipindi cha toba ziliazimishwa zamani katika kutoa heshima kwa miungu ya kipagani Osiris, Adonis na Tamuzi” -John Landseer, Sabaean Researches, pp. 111, 112.
“Siku arobaini za toba za Kwaresima moja kwa moja zilikopwa kutoka kwa waabudu miungu ya Babeli. Kwaresima kama hiyo ya siku arobaini, katika majira ya vuli ya mwaka, bado inaadhimishwa na wa-Yezidis au wapagani waabudu-shetani wa Koordistan, ambao wameirithi kutoka kwa walimu wao wa mwanzo, wababeli. Kwaresima kama hiyo ya siku arobaini ilifanywa katika majira ya vuli na wamexico wapagani…Kwaresima kama hiyo ya siku arobaini iliadhimishwa huko Misri.” -Alexander Hislops, The Two Babylons, p 104-105.
“Kipindi cha siku arobaini za toba na sala ambacho huanzia siku ya Jumatano ya majivu na huandaa kwa ajili ya maadhimisho ya pasaka. Ingawa awali kilidumu chini ya wiki moja, wakati wa karne ya saba ikawa inawakirisha siku arobaini alizotumia Kristo jangwani. Wakati kilipoanzishwa mwanzo na kanisa Katoliki, baadhi ya watu walifanya muda mwingi pamoja na ubaguzi wa Jumapili. Hivi sasa wengi “huacha” siku moja au mbili wakati wa kipindi hiki.
“Neno “Kwaresima” (“Lent”) linatoka katika kingeleza cha zamani “Lencten” ambalo humaanisha “Majira ya vuli.” Liliundwa na kanisa Katoliki kati ya mwaka 525 B.K, chini ya uongozi wa padri Dionysus mdogo, Kwaresima ni kipindi cha siku-40 kutoka Jumatano ya majivu hadi Pasaka, ambacho huwekwa pembeni kwa ajili ya kufunga na kutafuta toba. Maadhimisho hayo hayapatikani katika Biblia, hivyo hayakutambuliwa na Yesu, mitume, au kanisa la Kikristo la mwanzo. Hata hivyo, siku za leo, kwa kawaida kinamaanisha “kuacha” kitu fulani, kwa kawaida baadhi ya tabia mbaya, au hata kufuta kabisa, ili kumpendeza Mungu. Kipindi hiki…kwa hakika asili yake ni Babeli, kama asili ya siku ya mwaka ambayo iliheshimu kifo na ufufuo wa Tamuzi; na badaye iliadhimishwa huko Misri kumheshimu Osiris, mwana wa Isis, ambaye alikuwa marudio ya Tamuzi.
“Wakati Nimrodi alipokufa, alifanywa mungu jua, harafu Semiramis [mke wake] alikuwa na mwana wa haramu aliyeitwa Tamuzi, ambaye yeye alidai kuwa ni mwana wa Nimrodi. Alisema kwamba alikuwa “mzao aliyeahidiwa wa mwanamke” (Mwanzo 3:15) na akataka kwamba wote yaani yeye na Tamuzi waabudiwe. Tamuzi akafanyiwa ishara ya ndama wa dhahabu. Semiramis akajulikana kama “malikia wa mbinguni,” na alikuwa ishara ya miungu wa kike wote wa kipagani waliokuja baadae. Mwakilishi wake anaweza kuonekana katika ibaada ya Maria ya kanisa la Romani Katoliki ambaye huitwa “mama wa kanisa” “malikia wa mbingu na nchi,” na “malikia wa ulimwengu.” Majina haya hayawezi kurejea kwa Maria, Mama wa Yesu, kwa sababu hakuna sehemu yoyote kwenye Biblia inapozungumzia mamlaka ya Maria kwa jinsi hiyo.
Somo Zuri sana Kwa wasiojua kuwa wanaabudu sanamu
 
Kwa hiyo kinakuuma nini? We fuata yako ya wakatoliki waachie wakatoliki.

Unataka wote muende mbinguni kutatosha? Na unataka moto uishe bila kutumika? Yani waandae moto miaka na miaka toka agano la zamani mpaka sasa halafu ukose wateja?
Kwenye uzi wangu kuna popote nimewataja Wakatoliki?
 
Wewe kobaz,

1. Nitajie Dini ya kwanza toka dunia iumbwe.
2. Nitajie dini ya kwanza kuwa na utaratibu wa kufunga kutwa nzima na jioni kula (kuna watu walikuja miaka 1300 baadae wakaiga)
3. Nitajie dini iliyokuwa na utaratibu wa kufunga mwezi mzima na mwisho wa mfungo kunakuwa na sikukuu (kuna watu walikuja miaka 1300 baadae wakaiga)
Huyo kobazi atakujibu
 
Back
Top Bottom