Kweka arudishwa rumande, kesi kutajwa Oktoba 29

Kweka arudishwa rumande, kesi kutajwa Oktoba 29

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mfanyabiashara na mkazi wa Bunju A, Laurence Kweka (48), amerejeshwa rumande baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, akikabiliwa na shtaka la kumuua mkewe, Jane Urassa.

Kweka amefikishwa mahakamani hapo leo Alhamisi, Oktoba 15, 2026, na kusomewa shtaka moja la mauaji katika kesi namba 23407 ya mwaka 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kemilembe Josiah.

Soma Pia:
Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa ameondolewa mahakamani hapo na kurejeshwa rumande, huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Oktoba 29, 2026, kwa ajili ya kutajwa
 
Si inasemekana kuna shughuli maalum ya kumbukumbu siku hiyo
 
uendeshaji wa kesi za mauaji tz ni wa kipuuzi sana, usishangae mwamba akasota rumande mwaka ndo akasomewa PI, na mwaka tena ndo ikaanza kusikilizwa.
Usidharau kazi za wenzio:
1) Usalama wake, MTUHUMIWA, kwa muda mrefu ujao utakuwa bora zaidi akiwa chini ya ulinzi!
2) Uchunguzi bado unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuangalia afya ya akili ya mtuhumiwa
3) NA MENGINE MENGI TUNAYOYAJUA NA TUSIYOYAJUA!
 
Hasira hasara!
"HASIRA HASARA", Ukiwa ndani mahabusu hurusiwi kuingia na saa wala viatu, kwahiyo unakuwa hujui ni saa ngapi!?,akitokea afande anasikiliza mpira muda wa jioni ndo unahisi tayari saa 10 na kuendelea, giza likiingia kuja kuona mwanga tena akilini ni kama siku 3. Kule pasikie tu. Bora jela waliohukumiwa wanatoka nje wanaangalia TV, wanacheza mpira ila mahabusu hapafai. Kuna madai jamaa anaumwa kansa, kuna uwezekano akakata moto kabla kesi haijafika popote, kibaya zaidi aliua akajipeleka mwenyewe, ni ngumu kukana kosa. Na kuna wapumbavu humu wanamshangilia wanamuona mwamba ila reality ni alifanya upumbavu wa hali ya juu. Bora kuonekana fala ukaendelea na maisha ya uraiani, kuliko kuonekana shujaa halafu unalala sakafuni, unachanganywa na vibaka kwa muda usiojulikana. Kule hapafai pasikie tu.
 
Uaidharau kazi za wenzio:
1) Usalama wake, MTUHUMIWA, kwa muda mrefu ujao utakuwa bora zaidi akiwa chini ya ulinzi!
2) Uchunguzi bado unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuangalia afya ya akili ya mtuhumiwa
3) NA MENGINE MENGI TUNAYOYAJUA NA TUSIYOYAJUA!
ndo upuuzi wenyewe huo, et usalama wa mtuhumiwa? uchunguz wa afya ya akili ndo uchukue mwaka mzima, kuna uchunguz gan unatakiwa kwa kesi ya kweka zaid ya afya ya akili?
 
Back
Top Bottom