Kweka arudishwa rumande, kesi kutajwa Oktoba 29

Namlaumu kwann hakutaka kuwasumbua polisi japo kidogo.

Kuna Chaka moja nipo huku Kuna miamba inasemekana ilifanya matukio huko town ikaja kujificha huku yani haina simu Wala haibebi electronics yoyote maisha Yao ni kama ya early stone age
 
Kuacha kila kitu na kwenda kuanza maisha mapya yangekuwa ni maamuzi mazuri zaidi!!
 
Kweka akipata wakili mzuri, hawezi fungwa zaid ya miaka 15
Hakuna cha wakili mzuri, huyu kaua na kujisalimisha, afya ya akili inatokea wapi!?,angeua akakutwa jalalani anakula uchafu wa jalalani na kuokota makopo waweza kusema afya ya akili. Hizo kesi kwa bongo hawanaga haraka nazo, hukumu wanayo tayari ila kama ana ela kwenye akaunti au ndugu zake wana ela itacheleweshwa cheleweshwa wawachukulie ela, mwishowe atahukumiwa miaka mingi au maisha jela. Akibahatika atatoka huko mbeleni kwa msamaha wa kiongozi atakayekuwepo. Akija kutoka atakuta magari yote yanatumia umeme na mtoto wake wa miaka minne ameshaolewa. Sio kesi nyepesi, alifanya upumbavu sana.
 
wewe wasema
 
Kuacha kila kitu na kwenda kuanza maisha mapya yangekuwa ni maamuzi mazuri zaidi!!
Kabisa, tena inaonekana anajiweza kiuchumi, unasahau na kuanza upya kwa amani, inauma lakini baada ya kujichanganya kwa muda unasahau. Kisaikolojia kwa hali ya kiuchumi aliyofikia ya kumiliki ghorofa na bastola, kuchanganywa mahabusu na vibaka kwa muda usiojulikana kwa kesi nzito kama ile na inasemekana anaumwa, kuna uwezekano akajiua hukohuko mahabusu akipata upenyo wa kufanya hivyo. Hasira hasara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…