ROHO=UKAMILIFU.
Mkuu wangu, labda nifikishe tafakari hii kwenu. Roho ni UKAMILIFU (sio perfectness). Kinachofanya uitwe binadamu, mnyama, kiti, ulimwengu, maji, upepo, n.k. Tofauti ni kwamba, zipo roho hai na roho mfu pia, yaani ukamilifu katika viumbe hai na ule wa viumbe visivyokuwa hai.
Anaitwa binadamu, kuku au panga, ni kwa sababu vimefikia ukamilifu wao wa kuitwa hivyo. Chuma bado kwa muhunzi ni chuma tu, kikishatoka ni jembe, panga au kisu,n.k.
Katika viumbe hai(wanyama), uhai ndio the most valuable element ya ku-determine Ukamilifu wa hicho kiumbe!
Wakati katika viumbe visivyokuwa hai mambo kama size, shape, number, ...hu-determine ukamilifu wa kitu. Jabali, jiwe, kokoto, mchanga, vumbi... Mti, mbao, kiti,n.k. Mbao zinafikia UKAMILIFU fulani ziitwe meza au kiti au kabati, n.k.
Nimewasilisha!
Anaita sasa!