Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Amani iwe nanyi wadau.
Sasa nimeanza kuamini kuwa kumbe suala la ICC ni tishio kubwa kwa serikali ya awamu ya Tano, pamoja na kebehi za Wanalubumba humu.
Sasa nimeamini kuwa viongozi wa serikali ya awamu ya Tano wanaiogopa kweli ICC na sasa wameanza kutapatapa.
Kwanini nasema hivi?
Kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi balozi za nchi za Ulaya na Marekani walitoa madai ya kukiukwa kwa Haki za binadamu na msingi ya demokrasia katika uchaguzi wa Tanzania. Walitaka mamlaka za Tanzania kuchukua hatua baada ya wapinzani kunyanyaswa na kukamatwa hovyo na polisi na kwenye baadhi ya maeneo kuuwawa. Serikali haikuwai kutoa tamko kuonyesha wanafanyia kazi madai hayo zaidi ya kuwapuuza tu.
Baada ya kutokea tuhuma za kuua watu na kupanga kuwauwa wapinzani serikali pia ilitulia tuli na kuwadharau wapinzani Ila baada ya kuona ushahidi na maombi yamepelekwa ICC sasa tumeanza kuona kuweweseka kwa upande wa serikali kusiko kawaida.
Nini Kimetokea baada ya Maombi Kupelekwa Icc juu ya kuichunguza Tanzania na ICC kukiri kupokea maombi?
1. Polisi Zanzibar waliitisha kikao na kusema Kuna askari amekamatwa na kuuwawa. Taarifa hizi hazikuwai kutolewa popote kipindi cha uchaguzi na wala kipindi balozi za Marekani na Ulaya zilipotoa matamko.
2. Leo IGP Simon Sirro Kaitisha kikao na kusema wameanzisha uchunguzi chini ya DCI ya matumizi yaliyozidi nguvu Zanzibar na kwenye uchaguzi, akasema anamuomba Lissu arudi ili wampe ulinzi pamoja na Lema na akasema watu waliokufa ni wawili tu.
Kwanini haya yote sasa hivi?
Kwa wataalamu tumeona hii ni defensive mechanism ya polisi kuonesha kuwa kwanza polisi nao waliuwawa na pili wanafanyia kazi malalamiko hivyo hakuna haja ya ICC kuchunguza. Hii ni kwa sababu ili icc ianze uchunguzi ni lazima ithibitike kuwa vyombo vya ndani haviwezi au vimeshindwa kushughulikia hayo matatizo.
Napenda kutoa pole kwa polisi kwa sababu haya yote yanayofanyika inaonekana kuwa sasa viongozi hawa wa Tanzania wame-panic na wanajaribu kufunika kombe wakati ni too late tayari.
Napenda niwape polee sana maana kama ni kisu, kimeshagusa mfupa. Watulie tu.
Mods Naomba msiunganishe huu uzi maana unajitegemea kimaudhui