Kweli ICC inatisha. Hadi Sirro kasema watampa Lissu ulinzi

Kweli ICC inatisha. Hadi Sirro kasema watampa Lissu ulinzi

IGP anatekeleza majukumu Yake wapi kasema anaogopa ICC? Hilo beberu lenu Amsterdam linawajaza ujinga Kama lilivyofanya kabla ya uchaguzi na Sasa baada ya uchaguzi.
Jipeni moyo HAKUNA lolote Trump mwenyewe yuko Kama Lissu tu eti kaibiwa akiambiwa ukweli hakuna aliyeiba kura anafukuza kazi. Nyumbu hovyo kabisa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jamaa umepanik kweli kweli, kunywa maji basi
 
Nyumbu ni nyumbu tu.
kwanza kabla ya uchaguzi mlianza kututishia Armsatdam,mkaja na Jaffrey Smith,mkaja tena na kaulizenu za"mabalozi wamesema"
baada ya uchaguzi mkaanza na kauli za maandamano nchi nzima likabuma,mkaanza na kauli za"E.U wamesema".sasa mmeamia na ICC.
Rais JPM keshaapishwa,watanzania wanachapa kazi na maisha yanaendelea.
 
Kitendo cha Lissu kusindikizwa na mabalozi wa nchi tatu Airport ni kielelezo tosha kwamba Serikali haiaminiki tena mbele ya Jumuia ya kimataifa.

Yaani raia wa Tanzania ndani ya nchi ya Tanzania asindikizwe airport na mabalozi wa nchi tatu za ulaya kwa pamoja - nini tafsiri yake.
You're right, lile tukio limetuvua nguo kabisa kabisa...!!
Ni aibu sana
 
Amani iwe nanyi wadau.

Sasa nimeanza kuamini kuwa kumbe suala la ICC ni tishio kubwa kwa serikali ya awamu ya Tano, pamoja na kebehi za wanalumbumba humu.

Sasa nimeamini kuwa viongozi wa serikali ya awamu ya Tano wanaiogopa kweli ICC na sasa wameanza kutapatapa.

Kwanini nasema hivi?
Kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi balozi za nchi za Ulaya na Marekani walitoa madai ya kukiukwa kwa Haki za binadamu na msingi ya demokrasia katika uchaguzi wa Tanzania. Walitaka mamlaka za Tanzania kuchukua hatua baada ya wapinzani kunyanyaswa na kukamatwa hovyo na polisi na kwenye baadhi ya maeneo kuuwawa. Serikali haikuwai kutoa tamko kuonyesha wanafanyia kazi madai hayo zaidi ya kuwapuuza tu.

Baada ya kutokea tuhuma za kuua watu na kupanga kuwauwa wapinzani serikali pia ilitulia tuli na kuwadharau wapinzani Ila baada ya kuona ushahidi na maombi yamepelekwa ICC sasa tumeanza kuona kuweweseka kwa upande wa serikali kusiko kawaida.

Nini Kimetokea baada ya Maombi Kupelekwa Icc juu ya kuichunguza Tanzania na ICC kukiri kupokea maombi?

1. Polisi Zanzibar waliitisha kikao na kusema Kuna askari amekamatwa na kuuwawa. Taarifa hizi hazikuwai kutolewa popote kipindi cha uchaguzi na wala kipindi balozi za Marekani na Ulaya zilipotoa matamko.

2. Leo IGP Simon Sirro Kaitisha kikao na kusema wameanzisha uchunguzi chini ya DCI ya matumizi yaliyozidi nguvu Zanzibar na kwenye uchaguzi, akasema anamuomba Lissu arudi ili wampe ulinzi pamoja na Lema na akasema watu waliokufa ni wawili tu.

Kwanini haya yote sasa hivi?
Kwa wataalamu tumeona hii ni defensive mechanism ya polisi kuonesha kuwa kwanza polisi nao waliuwawa na pili wanafanyia kazi malalamiko hivyo hakuna haja ya ICC kuchunguza. Hii ni kwa sababu ili icc ianze uchunguzi ni lazima ithibitike kuwa vyombo vya ndani haviwezi au vimeshindwa kushughulikia hayo matatizo.

Napenda kutoa pole kwa polisi kwa sababu haya yote yanayofanyika inaonekana kuwa sasa viongozi hawa wa Tanzania wame-panic na wanajaribu kufunika kombe wakati ni too late tayari.

Napenda niwape polee sana maana kama ni kisu, kimeshagusa mfupa. Watulie tu.

Mods Naomba msiunganishe huu uzi maana unajitegemea kimaudhui
Mkuu,

Wewe sio mtalaamu wa uchambuzi wa kauli ila ni shabiki wa itikadi kinzani zilizotopea hasa unaposikia Lissu na Polisi (You are absolutely too much addicted with stereotype passion and pseudo politics that impairs independent personal analytical decision)

Kwanza madai yako ni speculative, biased and polarized in favour of your preference. Huwezi kudai kwamba eti kusema polisi itampatia huyo mkimbizi deko kwamba nni defensive mechanism ili ICC isiendelee na mpango wenu wa ndoto ya mchana.

In security iwhat was appealed by IGP is termed as a "Bed Bugs Sweet Trap"

Mwenye masikio na asikie, mwenye macho na aone, mwenye ufahamu na afahamu, mwenye maarifa na ang'amue.
 
Hivi wakishakutwa na hatia watuhumiwa watasokotwa kwa adhabu ipi.!
 
Mkuu,

Wewe sio mtalaamu wa uchambuzi wa kauli ila ni shabiki wa itikadi kinzani zilizotopea hasa unaposikia Lissu na Polisi (You are absolutely too much addicted with stereotype passion and pseudo politics that impairs independent personal analytical decision)

Kwanza madai yako ni speculative, biased and polarized in favour of your preference. Huwezi kudai kwamba eti kusema polisi itampatia huyo mkimbizi deko kwamba nni defensive mechanism ili ICC isiendelee na mpango wenu wa ndoto ya mchana.

In security iwhat was appealed by IGP is termed as a "Bed Bugs Sweet Trap"

Mwenye masikio na asikie, mwenye macho na aone, mwenye ufahamu na afahamu, mwenye maarifa na ang'amue.
So unamaanisha wanataka wam trap then wamsepeshe kuzimu?
 
Back
Top Bottom