Kweli ICC inatisha. Hadi Sirro kasema watampa Lissu ulinzi

Kweli ICC inatisha. Hadi Sirro kasema watampa Lissu ulinzi

Kitendo cha Lissu kusindikizwa na mabalozi wa nchi tatu Airport ni kielelezo tosha kwamba Serikali haiaminiki tena mbele ya Jumuia ya kimataifa.

Yaani raia wa Tanzania ndani ya nchi ya Tanzania asindikizwe airport na mabalozi wa nchi tatu za ulaya kwa pamoja - nini tafsiri yake.
Na jeshi la UN
 
Wakati anapigwa risasi hizo zisizo na idadi walikuwa wapi, wao si ndo walinzi wa raia na mali zao.

Wanamdanganya.
 
Leo, Sirro anaadhirika mbele ya vyombo vya habari. Naona siku yake inawadia na ningeomba kama ICC wangelikuja Tanzania asap kusudi ya kufanya uchunguzi kamilifu kabla hawaja potezwa mashahidi husika. Lazima Sirro, na vibaraka wengine wa NEC na ZEC wajibu dhuluma waliofanyia watanzania.

Tuko ngangari na nimejiahidi kuwa watakapo fikishwa mahakamani na mimi nitahakikisha naenda ubelgiji. Lazima watokomezwe kwa uhuni wao.
 
Mama d mkuu si ulishasema mnasubili wito , unakuja sio mda ,Mambo mazito Sana haya,Sina kinyongo Kama mwa if mwenzangu nauli nitakuchangia, ila hakuna namna mkuu ,
Hakunaga kesi inayosikilizwa upande mmoja mkuu. Nikienda Mimi nawe utaenda na watakaotuita ndio watoa nauli

Ningefurahi sana kama hiyo kesi ingekuepo twende ila ndio hivyo tena
 
Waziri wa Mambo ya nje ana kazi nzito hadi anasaidiwa na Polisi

hiii nchi bwana nadhani sasa mfumo utajifunza namna ya kuilinda nchi na hawararuhusu tena kushikiwa akili zao na mtu mmoja mjinga
Yaaani wameshindwa kushauri na kutekeleza kila wanachoambiwa bila reasoning ... yaani leo Tanzania imekua maarufu na kielelezo ya WIZI WA KURA
HIVI angeruhusu majimbo yote ambayo wapinzani wameshinda watangazwe na angalau kura za urais za uhalisia angekosa nini ....unataka ushindi wa 100% wa nini ? hata ukiwaambia watoto wako wakupigie kura hawatakupa 100%

Huwezi kuuwa upinzani namna hiyo ...
 
Leo, Sirro anaadhirika mbele ya vyombo vya habari. Naona siku yake inawadia na ningeomba kama ICC wangelikuja Tanzania asap kusudi ya kufanya uchunguzi kamilifu kabla hawaja potezwa mashahidi husika. Lazima Sirro, na vibaraka wengine wa NEC na ZEC wajibu dhuluma waliofanyia watanzania.

Tuko ngangari na nimejiahidi kuwa watakapo fikishwa mahakamani na mimi nitahakikisha naenda ubelgiji. Lazima watokomezwe kwa uhuni wao.

willison Mahera anaenda Uganda kumsaidia Museveni kuiba kura ....mzeee wa ushindi wa kishindo

Thomas Mihayo yeye kapewa Vodacom ajitulize nayo kama sehemu ya Ahsante
 
hiii nchi bwana nadhani sasa mfumo utajifunza namna ya kuilinda nchi na hawararuhusu tena kushikiwa akili zao na mtu mmoja mjinga
Yaaani wameshindwa kushauri na kutekeleza kila wanachoambiwa bila reasoning ... yaani leo Tanzania imekua maarufu na kielelezo ya WIZI WA KURA
HIVI angeruhusu majimbo yote ambayo wapinzani wameshinda watangazwe na angalau kura za urais za uhalisia angekosa nini ....unataka ushindi wa 100% wa nini ? hata ukiwaambia watoto wako wakupigie kura hawatakupa 100%

Huwezi kuuwa upinzani namna hiyo ...

Mithali : Mlango 28​

16 Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana;Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.
 
Kwahiyo wenyewe wanatumia twitter wakiwa ofisini tu? Hawajichanganyi na watu wengine huko maeneo twitter ilipozuiliwa? Usiwe mpuuzi namna hii dada yangu.
Kwa hiyo unaamini Chamwino na mji wa serikali hakuna Wi-fe, TCCL broadband ninahakika ofisi nyingi wanatumia na Wi-fe ipo yakutosha

Moja ya kazi ya Wi-fe ni kuficha IP adress hivyo restriction website itafunguka bila wasi hata hiyo twitter, naamini TCCL hawajazuia mkongo wa Taifa kuifikia twitter bali waliounganishwa na mkongo huo kama Isp's( voda,Tigo n.k) ili watupe sisi wa mobile device hao ndio wamebana usichoelewa nini yani .

Kuingia twitter sio lazima VPN kuna wi-fe ,Opera na Google unaweza kuingia twitter yako nadhani utakuwa umeelewa.

Mimi ni jogoo tafadhali.
 
Umeelewa hoja yangu we mataga? Ama unakurupuka tu kama polepole?
 
Amani iwe nanyi wadau.

Sasa nimeanza kuamini kuwa kumbe suala la ICC ni tishio kubwa kwa serikali ya awamu ya Tano, pamoja na kebehi za Wanalubumba humu.

Sasa nimeamini kuwa viongozi wa serikali ya awamu ya Tano wanaiogopa kweli ICC na sasa wameanza kutapatapa.

Kwanini nasema hivi?
Kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi balozi za nchi za Ulaya na Marekani walitoa madai ya kukiukwa kwa Haki za binadamu na msingi ya demokrasia katika uchaguzi wa Tanzania. Walitaka mamlaka za Tanzania kuchukua hatua baada ya wapinzani kunyanyaswa na kukamatwa hovyo na polisi na kwenye baadhi ya maeneo kuuwawa. Serikali haikuwai kutoa tamko kuonyesha wanafanyia kazi madai hayo zaidi ya kuwapuuza tu.

Baada ya kutokea tuhuma za kuua watu na kupanga kuwauwa wapinzani serikali pia ilitulia tuli na kuwadharau wapinzani Ila baada ya kuona ushahidi na maombi yamepelekwa ICC sasa tumeanza kuona kuweweseka kwa upande wa serikali kusiko kawaida.

Nini Kimetokea baada ya Maombi Kupelekwa Icc juu ya kuichunguza Tanzania na ICC kukiri kupokea maombi?

1. Polisi Zanzibar waliitisha kikao na kusema Kuna askari amekamatwa na kuuwawa. Taarifa hizi hazikuwai kutolewa popote kipindi cha uchaguzi na wala kipindi balozi za Marekani na Ulaya zilipotoa matamko.

2. Leo IGP Simon Sirro Kaitisha kikao na kusema wameanzisha uchunguzi chini ya DCI ya matumizi yaliyozidi nguvu Zanzibar na kwenye uchaguzi, akasema anamuomba Lissu arudi ili wampe ulinzi pamoja na Lema na akasema watu waliokufa ni wawili tu.

Kwanini haya yote sasa hivi?
Kwa wataalamu tumeona hii ni defensive mechanism ya polisi kuonesha kuwa kwanza polisi nao waliuwawa na pili wanafanyia kazi malalamiko hivyo hakuna haja ya ICC kuchunguza. Hii ni kwa sababu ili icc ianze uchunguzi ni lazima ithibitike kuwa vyombo vya ndani haviwezi au vimeshindwa kushughulikia hayo matatizo.

Napenda kutoa pole kwa polisi kwa sababu haya yote yanayofanyika inaonekana kuwa sasa viongozi hawa wa Tanzania wame-panic na wanajaribu kufunika kombe wakati ni too late tayari.

Napenda niwape polee sana maana kama ni kisu, kimeshagusa mfupa. Watulie tu.

Mods Naomba msiunganishe huu uzi maana unajitegemea kimaudhui

kwanza nakupa pole kwa kua taburalasa, pili kwa kua ni chadema wameongea probably ni shudu! anyway ebu pitia hii link kidogo ujue politics za dunia zikoje

Back
Top Bottom