Kweli kweli wameiba! Je, tupo tayari kwa vikwazo (Sanctions)? Nani ataathirika: Mimi na Wewe au Mwanasiasa?

Kwa tàarifa yako mataifa makubwa haya hayategemei taarifa za Lisu au waangalizi bali wanategemea taarifa za inteligensia zao tu. Wanajua hata ikulu kuna nini kwenye mvungu wa kitanda. Ukweli wa yaliyotokea uchaguzi huu hayajifichi kwani tayari mitaani yanatrend. Vituo vingi hawakuhesabu kura vituoni kwani masanduku yalibebwa na vijana wa jkt kabla ya kuhesabiwa na kuna baadhi ya vituo hata wahudumu waliachwa wakapanda boda boda. Tunaelewa sasa kuwa karatasi za matokeo sehemu kubwa zilishajazwa hata kabla ya upigaji wa kura kuisha na wasimamizi wakalazimisha kuyasoma, kama yule wa Arusha aliyesema nanukuu ' Nasoma kama yalivyoandikwa' .
Kwa haya yote yaliyotokea sielewi hata hao washindi wanapata wapi ujasiri wa kupita kwa wapiga kura na kudai wao ndio washindi. Kibaya zaidi hata wasimamao madhahuni wanathubutu kumdanganya Mungu kuwa waneshinda na sijui wanaweza kufanya maombi ya shukurani nafsi zao zisiwasute.
 
Mbona unatumia nguvu nyingi sana kupingana na ukweli? Hata kama mfumo unakufaidisha ni bora ungekaa kimya kwa madudu tuliyofanya uchaguzi huu. Ni aibu kwa mtu yeyote mwenye utu wake.
Halafu asivyo kuwa na aibu, eti asilimia 80 wamemkubali JPM. Huko ni zaidi ya kujitoa ufahamu!
 
Afu wazee mbona twitter yangu tangu jana haifunguki nikaifuta nikadownload upya bado tu hata kulog in inasumbua .Kuna mwingine ana shida hii?
 
1.Kwanini mlizuia matokeo ya urais kubandikwa vituoni?
2.Kwanini mlizima mitandao?
3.Kwanini tallying centre mmekamata watu wakijumlisha matokea mmewabambikizia kesi ya kukutwa na mabomu na mpaka sasa mmemficha Mazrui?
 
Raisi uliyepo madarakani unaibiwaje kura?
Kwa hiyo na Marekani watawekewa nikwazo na dunia au siyo jomba...si Trump anahisi na anasema ameibiwa kura..kaenda mahakamani..Joe Biden atawekewa vikwazo sijui na nchi gani Sasa...hahahaha
 
Mbona kama umepanic?
 
Bora tuteseke kwa muda ,hamna mtu mwenye mamlaka na hii nchi
 
Umesema kwa upole na weledi, umemuelimisha taratibu kwa kiswahili rahisi kabisa.
Kama hajaelewa tena tumuache tukanunie cement 35,000
 
Wakati Makonda anawekewa vikwazo uliwekwa ushahidi gani?
Mabalozi wa nchi tatu kumsindikiza mtu mmoja bado unajiaminisha ya kuwa mtu huyu ni mkulima wa viazi wa Lushoto?

Kama Taifa kuna mahali tumeteleza inabidi tuache kujidanganya.
Diplomasia yetu imepinduka kidogo katika miaka hii mitano ni lazima tukae vizuri na tujirekebishe ila bahati mbaya unafiki umetujaa na hakuna wa kuwaambia viongozi wetu kuwa suruali imetoboka mahali.Kikwete anajua dhahiri repercussion ya mrengo tunaochukua.
 
1.Kwanini mlizuia matokeo ya urais kubandikwa vituoni?
2.Kwanini mlizima mitandao?
3.Kwanini tallying centre mmekamata watu wakijumlisha matokea mmewabambikizia kesi ya kukutwa na mabomu na mpaka sasa mmemficha Mazrui?
Kwakawaida mawakala wanakuwa na form wanazo sign baada ya kuhesabu kura.
tuonesheni hizo tofauti Kati ya mawakala wenu na tume hata kwa matokeo ya ubunge na udiwani itapendeza.
Hizo zingine ni blah blah tu
 
Kwakawaida mawakala wanakuwa na form wanazo sign baada ya kuhesabu kura.
tuonesheni hizo tofauti Kati ya mawakala wenu na tume hata kwa matokeo ya ubunge na udiwani itapendeza.
Hizo zingine ni blah blah tu
Kuna uzi hapa wa ushuhuda,unaweza kuutafuta!
 
Yaani wazungu watuwekee vikwazo mwaka 2020 duu, kweli alili ni mali, kwamba wao peke yao ndo wanaendesha dunia au? Tena wakijadai kuweka vikwazo tunaenda na nchi za Asia, CHINA, INDIA, n.k

China alikuwa rafiki mkubwa wa Zimbabwe wakati wa vikwazo, kaangalie hali ya Zimbabwe ndio ujue wazungu ndio wenye hii dunia.
 
Kwani kudai haki Ni kuwachagua cdm? Vipi kwa wale ambao waliichagua ccm hawana haki hiyo?
 
Sidhani vikwazo vitafua dafu sisi ni donor country.tuna Kila kitu wawaulize kenya,
 
Kwahiyo tukiwekewa vikwazo ni kipi ambacho tutafanya wananchi ili kuikataa serikali kivitendo?
 
Sasa unataka Lissu afanye nini? Lissu hawezi kuandamana mwenyewe barabarani. Hiyo ndio option iliyobaki. Lissu hawezi kwenda msituni. Ngoja tu tubinywe labda tutapata akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…